Bila Bashiru na Polepole, Kenani Kihongosi asingekuwa hapo alipo

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Ama kweli mkuki uusafishao kila siku ndiwo wenye kuweza kukujeruhi hapo siku za mbele.

Kenani Kihongosi ni jina lililopendekezwa na Polepole kwa Bashiru ili lipelekwe Ikulu kwa Mamlaka za juu ili pamoja na yote aweze kuwa miongoni wa Wakuu wapya wa Wilaya kupitia nafasi za upendeleo kwa UVCCM na JPM kwa imani yake kwa Bashiru na Polepole-likapitishwa.

Ajabu na isivyotarajiwa Kenani leo kawa wa kwanza kumkandia Bashiru ili aonekane hafai kwa Samia!

Funzo kwa yeyote awaye tuwe na kiasi kwenye tendo lihusulo wema.
 
Kenani anatumikia CCM hamtumikii mtu. Ingekuwa rahisi huyo Bashiru angepeleka jina la mtoto wa Dada yake.
 
Mbona Hapi aligeuka na kuanza kuwatukana wastaafu na kutishia kuwapiga? Au wew Musiba ulisema ulilipiwa mahari na JK lakini baadae ukaanza kumpopoa. Kuimba ni kupokezana Hebu tulieni tusikie maneno ya wimbo unaoimbwa sasa
 
Back
Top Bottom