Big Result Now imefeli kabla ya kuanza

mussy p

Member
Jan 11, 2013
69
98
Mtihani wa kidato cha pili unaendelea kitaifa,Walimu wanaosimamia mtihani huo wakiwa hawajalipwa chochote mpaka sasa na leo ni mwisho kwa shule zenye Masomo 9.

Kwa kweli inatia huruma mwalimu kahudhuria semina hajakutana na soda wala maji, nauli kajilipia, katumia nauli ya wiki nzima kwenda kasimamia kwa kutumia boda boda nauli kwenda na kurudi 6000.

Mi binafsi nimebaki na maswali mengi,

1. Je ni kweli serikali inayodhamira ya dhati ya kuinua kiwango cha ufaulu nchini.

2 kwa nini elimu yetu inafanyiwa siasa.

3 Je Big Result Now ni kwa mpango gani itafanikiwa.

Mpaka sasa ni kimya hakuna kauli yoyote..ILEMELA-MWANZA..
 
Hakuna cha big result wala nn hiyo ni kaulimbiu tu kama nyingine zilizopo na zilizopita mfano kilimo kwanza,maisha bora kwa kila mtanzania...nimbinu za wajanja wachache kutumia kodi zetu na kufungua akaunt za nje.
 
Serikali bado haijaamua kumthamini mwalimu.

Lakini cha ajabu walimu hawa hawa 2015 Watashabikia green party.
 
Hiyo ni empty sloganeering kama kawaida mkuu. Hizo big results zinaanzia sekondari? Mwana filosofia Plato anasema "THE MOST IMPORTANT PART OF EDUCATION IS PROPER TRAINING IN THE NURSERY". Sisi wanatoka praimari hawajui kusoma wala kuandika.
 
KIKWETE hajachagua ELIMU... TUVUMILIE KIDOGO,MUDA WAKE UISHE.. HATUJUI AJAE??
 
Kama Big result now ni kauli kutoka kwa walimu, itafanikiwa! Kama ni kauli toka kwa mabosi wa walimu, hebu tuvute subira halafu tutaona!
 
na siku hz wanazid kutukandamiza yan hakuna kulipwa marupurupu ya kupandshwa daraja ukiuliza wanakwmbia sheria hyo ck hz haipo. sa cjui nan alifuta. manaake mtu umepandshwa daraja mwez wa nne but mshahra umepanda mwz wa nane ukidai ile miez ya nyuma wanatoa majb yanamna hyo
 
yaan Tanzania kama hujaijua basi utapata shida hawa wanaosema big result now wana utekelezaji wa kweli ni maneno tu kuwahadaa Raia ,,wanafiki tu uongo uongo mwingi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom