Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Habari ndugu money stunna,naomba msaada wako katika hili ninamtaji mzuri tu ila sijui wapi pakuanzia katika kufanya biashara hiyo ya kufata vitu uganda hasa viatu,hivyo naomba sana tuwasiliane unisaidie katika hilo,namba yangu "0712269097"...natanguliza shukrani.

Nione private nikusaidie, maana nishaenda huko
 
Mkuu Money Stuna na wadau wengine wenye uzoefu na solo la Uganda zaidi ya nguo, vipi kuhusu biashara zingine kama za stationeries, flash, computer accessories panafaa ukilinganisha na Nairobi?

Kaka kwa experience ndogo ya kwenda Uganda Mara 3 sidhani Kama hizo bidhaa uliotaja zina unafuu kwa Uganda. Bei Ziko juu compared to hapa kwetu Au Nairobi
 
Mimi ni mfanyabiashara nategemea kuanza biashara ya mitumba soko la mitumba Ilala boma. Nategemea kuuza nguo za kitoto na za kike. Naomben ushauri kuhusu mchanganuo mzima. Bei ya belo,gharama za usafiri, malazi, na taratibu za kusafiri.
 
Kuna uzi mmoja walidiscuss kwa kirefu sana kuhusu hii biashara ya kununua mitumba especially from Uganda.
Ngoja nikutafutie huo uzi nikuletee.
Utakusaidia sana na ukiweza utawatafuta waliochangia kwa sababu wengi ni watu wenye uzoefu wa kutosha kwenye hiyo biashara
 
quote_icon.png
By Money Stunna
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea, Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni

Kiresua, Kobe, Domhome and 14 others like this.

Dear Ex.


Reply Reply With Quote Send PM

 
nimesoma comment zenu na nimefaidika sana na yote mliyoyaongea hapo sasa naomba kuongea na Mkuu Moneystunna popote alipo naomba uni PM and i will Pm you back mkuu
 
Useful thread ever.....thanks wote...I salute bu money stunna!....
Kwa wale ambao ndo mara ya kwanza kuuona huu uxi jamani jaribu kupitia uzi wote kabla hujauliza maswali coz kuna baadhi ya maswali yashajibiwa huko nyuma
 
Nione private nikusaidie, maana nishaenda huko

Mkuu Dumelang plz hebu niPM namba zako najaribu kukutumia ujumbe huko PM unagoma cjui kwanini Nina bwana mdogo wangu anataka kufata Viatu huko sasa anataka Mwangaza kwenye maeneo flan nikipata mawasiliano yako au yeyote mwenye uzoefu wahuko Itakuwa msaada tosha namba zangu ni 0764 504 540 Natanguliza shukrani
 
Last edited by a moderator:
yaani wewe unaweza ukawa msaada mkubwa wa mawazo kwangu maana naona hii naweza kuifanya vzr hapa arusha.

Habar wiseboy,mi ni mgeni humu ila nimevutiwa mno na mada hususan kwa post yako nami nahitaj kufanya biashara ya nguo.
 
......ngoja nirud kwenye biashara sasa...kusema ukweli uganda nguo za duka, viatu vya duka, mikoba ya special vinauzwa angalau bei kdogo, ila mtumba mh cjaona faida kwa kweli kwa 7bu zifuatazo
1.nilienda kuchukua nguo ndo ilikuwa mara ya kwanza hvyo ckujua bei ya huku bongo
2.nilitaka kufunguliwa baro na kuchaguliwa grade A tu ya nguo, hvyo mnunuz anabak na makapi, wanaita furges wenyewe
3.kwa 7bu hzo hapo juu nilidondokea pua kwan nakumbuka sket ndefu niliuziwa elf 13, fupi elf 10 gauni ndefu 21elf, gaun fupi 15elf, tops elf 6, kwa mantiki hiyo nilivyorud bongo kusema ukweli hazikulipa kbsaa kwan hzo bei nilizochukulia ndo za kuuzia bongo.
Ila nilichanganya mzigo wa nguo za special zikawa zinalipa mfano skin surual nilichukua kwa elf 6 nauza 12, simple shuz 6elf nauza 12, n.k

habar wiseboy,naomba mawasiliano yako.
 
Back
Top Bottom