Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

Habari wana JF
Naomba kujuzwa kwa mwenye uelewa/uzoefu wa biashara ya ku-export Wanyama hai kama Mbuzi, Ng'ombe, Kondoo nje ya nchi kwa ajiri ya nyama. Ni process gani zinatakiwa kupitia/kufuatwa ili kufanya biashara hii. Nchi yetu ina idadi kubwa ya Wanyama tajwa na zipo nchi ambazo wana mahitaji ya nyama zitokanazo na Wanyama tajwa na wanahitaji kupata bidhaa hii iliyo fresh ila wanaishia kupata nyama za kwenye ma-fridge.
Natanguliza shukurani.
Mkuu commoro na Syshells kuna soko zuri la wanyama hai hasa ng'ombe. Hata hivyo kufanya biashara hiyo huhitaji vibali kadhaa vya serikali, mtaji mkubwa kidogo pamoja na usimamizi mathubuti ya biashasha ili kuepuka uwezekano wa kutapeliwa au wanyama kuathirika kabla ya kufika sokoni au kufika wakiwa wamepungua ubora. Kama unataka kufanya biashara hiyo nicheki PM
 
Mkuu commoro na Syshells kuna soko zuri la wanyama hai hasa ng'ombe. Hata hivyo kufanya biashara hiyo huhitaji vibali kadhaa vya serikali, mtaji mkubwa kidogo pamoja na usimamizi mathubuti ya biashasha ili kuepuka uwezekano wa kutapeliwa au wanyama kuathirika kabla ya kufika sokoni au kufika wakiwa wamepungua ubora. Kama unataka kufanya biashara hiyo nicheki PM
weka hapa na wengine tunufaike mdau maana wazo zuri sana hili aise
 
Mkuu commoro na Syshells kuna soko zuri la wanyama hai hasa ng'ombe. Hata hivyo kufanya biashara hiyo huhitaji vibali kadhaa vya serikali, mtaji mkubwa kidogo pamoja na usimamizi mathubuti ya biashasha ili kuepuka uwezekano wa kutapeliwa au wanyama kuathirika kabla ya kufika sokoni au kufika wakiwa wamepungua ubora. Kama unataka kufanya biashara hiyo nicheki PM
Asante mkuu, nakukuta huko PM.
 
Pm za nini sasa wekeni darasa tufaidike wote hapa
Mkuu si kila kitu kinafaa kumwambia kila mtu na wala si kila mtu anahitaji kujua kila kitu, pia si kila kitu kinafaa kusema kila mahali na ndio maana kukawa na PM. Hata hivyo kama kuna kitu unataka kukijua specifically, unaweza kuuliza na kama kuna ninachojua nitakufahamisha.
 
Nahitaji elimu juu ya biashara ya mbuzi kutoka kwa watu wenye experience na biashara hiyo.
1.ununuaji wa mbuzi Mikoani na kuleta dar es salaam.
2.Mikoa yenye mbuzi wengi.
3.Masoko ya mbuzi dar es salaam na nje ya Tanzania.
4.usafirishaji wa mbuzi
 
Ununuzi wa mbuzi unategemeana na wapi unanunulia kwa mfano handeni kipindi cha kulima wanauzwa mpka 25000 kwa mbuzi, Soko la mbuzi kubwa sanaa dodoma kuna kiwanda kinanunua nyama ya mbuzi, kwa dar ni pugu mnadani na vingunguti
 
Mkuu Biashara zote ni ghalama, na kuongeza thamani ndo mpango mzima, Ukinunua MCHELE KUTOKA MBEYA UKALETA DAR, ili upate faida ni lazima ufanye usanii wa kuchakachua MCHELE wa mbeya unachanganywa na wa Morogoro na hata saa zingine unachanganywa na MCHELE WA NJE YA NCHI KUTOKA PAKSATAN NA THAILAND,

Bila kuongeza thamani huwezi fanya Biashara yenye Tija hata siku moja, na si lazima uanze na mitaji mikubwa mkuu, hii ya kuuza mchele au mahindi kama yalivyo ni unyonyaji na hakuna faida inayo patikana,

Chukulia mfano Kahawa Ya Tanzania au Pamba, PAMBA INAPELEKWA NJE INATENGENEZA NGUO THEN TUNARUDISHIWA KUUZIWA KWA BEI GHALI,

Ni uvivu wetu tu lakini hakuna kisicho wezekana ni kuweka mikakati
na kuwasafirisha ni usaniii mkubwa
 
Mnachozungumza ni kweli kuhusu kununua ng'ombe kwenye minada na kuwanenepesha kasha kuwauza sehemu kwenye soko kubwa kama Dar. Ninarafiki yangu aliwahi kunishirikisha hii biashara ila sikuifanya kutokana na kutingwa..ila ninaeneo la kama eka 20 ambazo niko mbioni kuongeza zifike angalau 50 kwa ajili ya shughuli hizi za kilimo na ufugaji..sasa naanza kupata wazo la kunenepesha ng'ombe pia maana kuna wasukuma na warundi kibao kupata ng'ombe sio ishu tena sometimes wanakupa hadi ng'ombe wa zawadi. Ni fursa kubwa hii
 
mkuu mimi ningekushauri ufanye jambomoja.

- Umefika wakati tuwe tunafanyabiashara zenye tija, biashara zenye faida na biashara ambzao hazina usanii.

- Biashara kama hizi zina usaniimwingi sana
1. Kununua mazao na kwenda kuyauzasehemu nyingine

2. Kununa kuku na kwenda kuziuzasehemu nyingine

3. Kununua ng'ombe na kwenda kuziuzasehemu nyingine

HIZI BIASHARA LAZIMA UWE MSANII WAHALI YA JUU KUWEZA KUZIFANYA NA SI KWAMBA ZINAHITAJI AKILI BALI ZINAHITAJIUSANII.


MFANO:


1. KUNUNUA KUKU NA KUJA KUZIUZA SEHEMUNYINGINE- HAPA HAKUNA ULICHO ONGEZA ZAIDI YA KUWALILIA WANAO KUZIA WAKUZIE BEIYA CHINI NA WEWE UKAUZE BEI YA JUU. HAUJAONGEZA THAMANI YOYOTE ILE KWENYE HAWAKUKU

2. UNANUNUA MAGUNIA YA MAHINDI KUTOKADODOMA NA KUPELEKA DAR- HAPA HAKUNA CHA MAANA ULICHO FANYA ILA USANIIUTAFANYIKA WAKATI WA KUNUNUA UTUMIE NDOO KUBWA ILIYO FANYIWA MODFICATION, NAWEWE WAKATI WA KUUZA LAZIMA UCHANGANYE MAHINDI MAZURI NA MABAYA ULIO NUNUA KWABEI YA CHINI. BILA KUCHANGANYA HAYA MAHINDI HUWEZI PATA FAIDA
- Hapa unakuwa hujaongezea hayamahindi thamani yoyute ile

3. Kwenye swala la ng'ombe nalolinahitaji usanii tu, ukawalilie wanao kuzia il wakupunguzie na wewe upatekafaida.

UMEFIKA WAKATI WA KUFANYA BIASHARA ZAKUONGEZA THANANI

1. Nunua ng'ombe chinja na supplynyama hapa unakuwa umeongeza thamani
-Au fungua kiwanda cha kupaki kabisana kuuzia watu wa supermarket, hapa unakuwa umefanya biashara ya maana sana

2. Nunua mahindi saga na paki unga,hapa unakuwa umeyaongezea hayo mahindi thamani kubwa mno na utapata faida

3. Nunua kuku chinja, pack na uza-
Hii ndo biashara ya kuad value, lakinihii ya kununua mchele kutoka morogoro na kuja kuuza dar inahitaji usanii wakuchanganya mchele wa morogoro na ule wa thailandla sivyo hakuna chachote kile utakacho faidi

NDO MAANA HII BIASHARA HAIHITAJI AKILIBALI USANII WA KUIBIA WATEJA, NA SI ENDELEVU

1. Biashara ya mazao sio lazima ufanye usanii ndio upate faida..mazao yana faida sana tu
2. Sio lazima watu wote wafanye biashara ya kuongezea bidhaa thamani...kwani watu wanavoenda kuleta nguo kutoka China na kuziuza kariakoo wanaongeza nn...lakn faida wanapata
 
HUJANIELEWA, MIMI SIJASEMA HII BIASHARA NI YA KISANII, NIMESEMA LAZIMA UWE MSANII KUFANYA BIASHARA AMBAZO UNANUNUA KITU NA KUJA KUKIUZA KAMA KILIVYO.

- MFANO:

Biashara ya mchele mara nyingi ni usanii mtupu, mtu anachukua mchele wa mbeya anachanganya na wa morogoro ndo anaingiza sokoni, na anafanya hivyo kwa sababu akiuza kama ulivyo itakuwa ni hasara kwake hatapata faida.

- Ndo maana nikasema ni bora tukaja na biashara za kuongeza thamani ambazo zinalipa sana, Ng'ombe unavyo mnunua na kuja kumuuza kama alivyo unakuwa hujamuongezea kitu na mara nyingi lazima huko unako nunua ulie sana ili wakupunguzie kwa sababu na wewe unakuja kumuuza kama alivyo.

- NDO MAANA NIKASEMA BIASHARA NYINGI SANA HATA ZA KUKU WA KIENYEJI MARA NYINGINE HUWA WANA MIX NA ZA KISASA HUMOHUMO, NA HII NI KWA SABABU HAKUNA UTARATIBU WA KUZIONGEZEA THAMANI NDO AZIUZE,

- BIASHARA YA NGOME

1. Yule mchinjaji wa mwisho ndo anae faidi na wala si wewe unae uza ngo'ombe kama ng'ome.
KAMA UNGEKUWA UNANUNUA NA KUZICHINJA NA KUPAKI AU KUUZA NYAMA UNGEPATA
1. NGOZI- HII NI PESA
2. KWATO HIZI NAZO NI DILI SANA
3. PEMBE ZINASOKO LAKE
4. MIFUPA, HII INASOKO LAKE PIA
5. NYAMA NI PESA
6. MENO YA NG'OMBE NI PESA
7. MKIA WAKE, ZILE NYWELE ZA MKIA WAKE NAZO NI PESA
HAPA UNGEWEZA PATA VITU ZAIDI YA 7

SIJAJUA WAUZAJI WA PUGU KAMA WA CHUKULIA MAANANI NA HIZI PRODUCT ZINGINE
Sasa wote wakifanya biashara ya kuchinja nani atanunua ng'ombe na kuleta machinjioni...kuna watu ambao wao wamespecialize kununua hapa hataki hassles za kusafiri kwenda kutafuta ng'ombe huko maporini...ndo mana kuna specialization...na hapo sasa unauliza kama hao wanaochinja wanatilia maanani hyo mikia au ngozi au manyoya...mtu anaspecialize kwenye kile kitu ambacho anaona atakiweza na kitampa faida...sasa wewe udeal na nyama...kongoro mkia ulimi pembe...huwezi kuwa expert wa kutafuta masoko yote hayo..muuliza swali anataka kuspecialize kununua na kuuza ng'ombe kama walivyo kinachoongeza thamani hapo ni kuwatoa sehemu yenye more supply na kuwapeleka sehemu ambayo kuna more demand. Hyo ya kuchinja siyo mbaya ila ni option nyingine na siyo usanii.
 
Mkuu kwani sisi hatuwezi kuwauzia Nyama? ni mpaka tuwauzi ng'ombe mzima? au tunawauzia ng'ombe wachinje wachukue ngozi theni watengeneze viatu waje kutuuzi kwa bei ya ng'ombe?

Masoko ya ng'ombe yako mengi sana hapo kenya tu kuna soko la kufa mtu,

Ila kule kenya wao wanafaidi zaidi kwenye ngozo na product zingine.


HILI LA DUBAI NA QATAR SI LA MCHEZO WAKUU SI RAHISI KAMA MNAVYO FIKILIA, SI SWALA LA KUPAKIA NG'OMBE KWENYE MELI NA KUPELEKA KULE.

HAWA MPAKA WAKUPE KIBALI CHA KUINGIZA NG'OMBE KWAO SI SWALA LA KITOTO NA SI SWALA LA MWAKA MMOJA
WANAANGALIA VITU VINGI SANA, WANAJARI AFYA ZA WATU WAO SI HUKU BONGO TUNALETEWA SAMAKI WA NYUKILIA THEN TUNAAMBIWA NI SALAMA

BAADHI YA VITU WANAVYO CHEKI

1. MAHALI NG'OMBE WANAKO TOKA/SHAMBA/RUNCH
2. UTUNZWAJI WAO
3. MADAWA WANAYO PEWA/ AINA YA MADAWA WANAO TIBIWA NAYO KAMA HAYANA MADHARA
4. CHAKULA WANACHO PEWA

HUWEZI OKOTELEZA NG'OMBE KWENYE MINADA YA SHINYANGA HALAFU UTARAJIE KUWAPELEKA DUBAI, NI NDOTO MKUU, HAPA LAZIMA UWE NA SHAMBA LAKO NA UNAKUWA UNAWATUNZA MWENYEWE NA HAPO NDO UNAWEZA KU EXPORT
NA KIBALI WANATOA WAO SI KWAMBA UNACHUKULIA HAPA DAR KIBALI

WALE WANAANGALIA SANA QUALITY YA NG'OMBE, NA SANA SANA WENYE RUNCH NDO WANAO WEZA KU EPORT HUKO NA SI HAWA NG'OMBE WA KUSWAGA NA KUPIGWA NA FIMBO

- HUWEZI BEBA NG'OMBE KUTOKA SHINYANGA NA TREN AU MALORI AU KWA KUWASWAGA UFIKISHE DAR UTARAJIE KUWAPAAKIA MELI UWAPELEKE DUBAI, UTARUDI NAO
Umenichekesha sana eti NG'OMBE WA KUSWAGWA...
 
Back
Top Bottom