Biashara ya mchele kipindi cha novemba, 2012 na januari - machi, 2013

mchelemchele

Member
Aug 22, 2012
7
2
JAMII MEMBERS HELLO,

HABARI ZA MCHANA WANA JAMII. NAPIGA HODI JAMVINI. POLENI NA HONGERENI KWA KAZI YA KUFAIDISHA JAMII.
NAPENDA KUWATANGAZIA KUWA SISI NI KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI. TUNA UZA TUTAUZA MCHELE KUANZIA MWEZI NOVEMBA, 2012 NA JANUARI, 2013.

TUNATAFUTA WATEJA WAKUNUNUA MCHELE KWA KIPINDI HICHO, MCHELE TULIONAO UNATOSHA KULISHA MAKUNDI MAKUBWA KAMA VILE WANAFUNZI WA VYUO AU SHULE ZA BWENI.

MWENYE HITAJI AWASILIANE KWA

EMAIL: mchelemchele@rocketmail.com

Nawashukuru kwa mawazo na ushauri wenu.

yours,

mchele
 
  • Thanks
Reactions: SMU
shukran mkuu, ungetutajia eneo mlipo na bei ingekuwa vzr zaidi.
 
Mchele huo ni kutoka maeneo gani? Maana unaweza kuwa wa Pakistani ............
 
shukran mkuu, ungetutajia eneo mlipo na bei ingekuwa vzr zaidi.

Nimeweka email mkuu

mchele

Mkuu,

Basi hata namba za simu tu, maana kuna jamaa zetu wengi tu hawaingii kwenye internet.

Mchele huo ni kutoka maeneo gani? Maana unaweza kuwa wa Pakistani ............

Naanza kupata wasiwasi na jamaa huyu mbona info anazotoa ni za kuficha ficha hata physical address imekua ngumu kutoa?

Nina Doubt sana.

Au ndo wadau wameamia kwenye mchele? Baada ya kuona kwenye ajira watu wameshitukia.
 
"...SISI NI KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI..." tangazo lako mbona haliendani na hapo bold? usiri wa nini? nenda katafute mtu wa kuwafundisha jinsi ya kutangaza biashara
 
Ndugu,
uwe na amani sisi tumetoa email inatosha kwa watu makini kama wewe waweza kutuma email. mchele huu unalimwa Tanzania na tumelima wenyewe.
 
"...SISI NI KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI..." tangazo lako mbona haliendani na hapo bold? usiri wa nini? nenda katafute mtu wa kuwafundisha jinsi ya kutangaza biashara

Ndugu,
Najua watu huwa wanapenda sana kukosoa kama wewe hivi, lakini ukweli huwa unabaki pale pale. sisi ni wanakikundi cha ujasiriamali, huu ni utambulisho; shughuli tunayokutangazia ni biashara ya mchele. Anuani ni hiyo email. Kwa watu wenye mahitaji hayo watatutafuta.
Mwisho wa yote tutafanya nao biashara.
mchele
 
Naanza kupata wasiwasi na jamaa huyu mbona info anazotoa ni za kuficha ficha hata physical address imekua ngumu kutoa?

Nina Doubt sana.

Au ndo wadau wameamia kwenye mchele? Baada ya kuona kwenye ajira watu wameshitukia.

Watu watakao hitaji watawasiliana nasi kwa email tuliotoa hapo awali.
 
Watu watakao hitaji watawasiliana nasi kwa email tuliotoa hapo awali.

Mkuu hivi hiyo biashara yako ni ya magendo? hutaki kusema mpo mkoa gani,shamba liko maeneo gani,ofisi zipo eneo gani mawasiliano ya emails hayawezi kukidhi information ninazo hitaji. Unajua kuweka kitu kwenye maandishi sio mchezo.

Nazidi kupata wasiwasi.
 
"...SISI NI KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI..." tangazo lako mbona haliendani na hapo bold? usiri wa nini? nenda katafute mtu wa kuwafundisha jinsi ya kutangaza biashara
kaka Narubongo,landa wewe useme hawa jamaa hawako serious na biashara yao. Kwa majibu yake machache tu unagundua kwama ni usanii tu. Pia nimesema mara nyingi humu kwama marketing ni ngumu sana inahitaji utulivu sana.
 
Hivi unauza mchele huku ukificha taarifa muhimu kiasi hiki, ukiuza dawa za kulevya itakuwaje ?. Kwa staili hii unajiharibia biashara na kuwakimbiza wateja mwenyewe.
 
Back
Top Bottom