Biashara ya kununua shahada Arumeru

kkitabu

Senior Member
Dec 27, 2011
140
47
Habari zenu wana JF, leo tuangalie Biashara ya kununua Shahada za kupigia kura iliyofanywa na CCM ilitoa mchango gani kwa ushindi wa Chadema. Tupia mchango wenu hapa. Natanguliza shukrani
 
Habari zenu wana JF, leo tuangalie Biashara ya kununua Shahada za kupigia kura iliyofanywa na CCM ilitoa mchango gani kwa ushindi wa Chadema. Tupia mchango wenu hapa. Natanguliza shukrani

Ni biashara kichaa, iliwaongezea kura CDM, MAGAMBA wamepata hasara mtaji umekufa!
 
Walinuua za vijana wakizani wazee na wanawake wako upande wao kumbe walibugi step. Ni hasara na fundisho kubwa. Nadhani hawatarudia tena.
 
Inaelekea system admin wa JF ni ccm damu damu kwa sababu kaondoa thread yangu haraka sana ili wana JF wasiweze kutoa mawazo yao
 
Habari zenu wana JF, leo tuangalie Biashara ya kununua Shahada za kupigia kura iliyofanywa na CCM ilitoa mchango gani kwa ushindi wa Chadema. Tupia mchango wenu hapa. Natanguliza shukrani

Hii biashara ya kununua shahada inaendekezwa na NEC kwa kuwa wafanya biasahara wakubwa ni CCM. Lakini NEC ikitaka kukomesha hii biashara ya kununua sahada inaweza.

NEC ichoweza kufanya ni kuruhusu wale wote wasiokuwa na shahada za kupigia kura aidha kwasababu wameuza au wamepoteza kupiga kura. Kama majina yamo kwenye daftari la wapiga kura. NEC iliruhusu mtu siye na shahada kujaza form 13 na baada ya kujaza then anapige kura. Lakini huko Arumeru NEC ilikataa kutumia form 13 kwa wale waliopoteza shahada au kununuliwa na CCM, nafikiri kwa maelekezo ya CCM.

Maana ya kutumia form hiyo ni kwamba kama CCM watanunua shahada, mtu bado anaweza kwenda kupiga kura kwa kujaza form no 13 hivyo itakuwa imekula kwao CCM, kwani watakuwa wamenunu shahada lakini bado wananchi watapiga kura.
 
Kwa kiwango kikubwa imepunguza idadi ya wapiga kura waliojiandikisha.
Waliouza shahada waliona aibu, au kwa heshima waliyonayo kwa walionunua zile shahada hawakujitokeza kujaza fomu namba 17, kitendo ambacho kilipunguza idadi ya wapiga kura.
CCM pia walishindwa kuingiza kura feki ambazo walikuwa wamezipiga kwa kutumia majina ya shahada walizozinunua, kutokana na alertness ya CHADEMA.
 
Back
Top Bottom