BHATOJA - Bob Hisia auiimba kwa lugha ya kisukuma kwa hisia kali.

Nimeusikiliza WIMBO wa Nurudin na Aslay wa KITORONDO unaodaiwa kugushiwa na Diamond Platinum lakini, sijasikia huo wa Diamond unaodaiwa kugushiwa ili kujiririsha.

Naomba anayeweza ku 'upload' Kitorondo wa Platinum ili kujirisha na hoja hii ya ku 'copy' na ku 'paste' anayobambikizwa nayo hivi hivi bila ushahidi wa kutosha.

Mbona huyu mtoto kuna watu wanaonekana kutopenda maendeleo yake. 'My number One' umempandisha kwenye chati maneno yakaja kuwa nao ka 'copy' na ku 'paste.' Huyu mtoto tunzo zote saba alizopata zilitokana na kura za watanzania hawa hawa wanaomjengea hoja kuwa si mzuri wa kihivyo.Jamani kuvuma kwa Diamond Platinum kunatokana na jitihada zake ambazo hata mkuu wa nchi amewahi kuzipongeza.

Mkubali mkatae Diamond Platinum YUKO JUU KIMZIKI.Hata sisi wa enzi hizo tunamkubali msiseme ni vijana tu.
Ndiyo yuko juu tena kwa sana.Wako wengine wazuri kama kina Barnaba,Amini na wengine lakini kwa mchujo wa KIMT Diamond Platinum kadhihirisha ukali wake kimziki.TUKUBALI tusikubali ndiye bingwa msimu huu.
Hili na liwe basi changamoto kwa wengine.Kumbukeni asiyekubali kushindwa si mshindani.
Wimbo wa Nurdin na Aslay huu hapa - :israel:https://www.youtube.com/watch?v=qJtiA6IGnxc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom