Bernard Membe: Polepole apelekwe shule kuijua vyema itikadi ya CCM. Ni ajabu Kamati Kuu kukaa bila Katibu Mkuu

Shonza vs Kubenea,daah watu na vichenchede vyao,Vitu laini.
Tupo sote duniani ila kuna watu wanapata vyakula vitamu jamani,loh
 
Kama anachokisema Membe ni sauti za ''wenye chama'', basi kwa sasa angekuwa ni Rais wa Tanzania. Huyu ambaye hakuvuka hata kwenye tano bora, unataka kuniamisha kuwa sauti yake ni sauti za ''wenye chama''.

Watanzania bana kwa udaku?
Sijawahi kuwa mdaku na kwa bahati nzuri sina tabia ya kuwa mshabiki.

Unasema Membe hakuvuka tano bora?hujawahi kushangaa Makamu Mwenyekiti hakuvuka kwenye mchujo hata wa awali 1995 na akawa Makamu mwenyekiti..!

Kuwa 'Mtu wa chama' haimaanishi lazima upate cheo Serikalini kama qualification.

Kolimba kawa Katibu mkuu na hakuwa na kofia ya chama. Kawawa 'kashushwa' kutoka Uwaziri Mkuu mpaka kuwa Waziri wa kawaida lakini alikuwa 'heavy weight' kwenye chama
 
Kingunge aliwakanya hamku muelewa leo ndo mnakuja kumuelewa safi sana, mtu hajawai kuwa hata balozi wanyumba kumi mnampitisha,,,,taratibu zimekeukwa, mkamnanga mzee wawatu akaamua kukaa pembeni.

Akina Mkapa wakaingia kikaoni na kapelo imeshuka mpa chini uso hauonekani wakihisi wao wameibuka shujaa sasa leo ndo mnafunguka macho nawaambia huu ndo mwanzo baada ya miaka kumi chama hakipo tena. wameanzakina nepi kuisoma namba soon mnafuata...yetu macho tunasubiri viwanda tupige mzigo
 
Hauwezi kureform chama bila ya kujua na kusimamia mifumo ya chama.
bandiko lingeacha uwanja mpana kama pia lingeonyesha athari za anachokosoa. za muda mrefu na muda mfupi na nini kikifanyika itakuwa bora zaidi.
Tatizo mambo haya ya wanasiasa yako kama litmus paper, muda wowote bandiko linaweza kuchenjuliwa ikaonekana ni sauti ya mtu akililia madaraka kwa jina la utetezi wa misingi ya chama.

maoni huru...
 
Huyu kaka yetu akili imemrudia baada ya kutoka kwenye "system". Duh Tanzania nakupenda kwa Moyo wote!

Nchi yetu ya ajabu sana. Mtu akiwa ndani ya system akili zote zinashikiliwa na "Mwenyekiti" au "Raisi".

Siku akitoka nje ya system ndiyo anatoa fikra zake "huru".

Ifike mahali viongozi wote walazimishwe kutoa makala za fikra zao at least kila mwezi ili wananchi tujue mawazo yao.
 
bandiko lingeacha uwanja mpana kama pia lingeonyesha athari za anachokosoa. za muda mrefu na muda mfupi na nini kikifanyika itakuwa bora zaidi.
Tatizo mambo haya ya wanasiasa yako kama litmus paper, muda wowote bandiko linaweza kuchenjuliwa ikaonekana ni sauti ya mtu akililia madaraka kwa jina la utetezi wa misingi ya chama.

maoni huru...

Ni wewe utakaeamua kuona ni nini anataka, mimi nimeona kuna misingi anataka Ccm isimamie hili Ccm ifanane na vyama vya kijamaa.
Wewe umeona analilia madaraka, ni chaguo lako.
 
Mimi sina tatizo na wale wanaoikosoa CCM kwa sababu bila kukosolewa haiwezi kujitathmini, tatizo langu ni hawa wakosoaji wa kinafiki au wanaokosoa baada ya maslahi yao binafsi ndani ya CCM kuzibwa.

Benard Membe wakati akiishi angani na kubadilisha mabegi uwanja wa ndege hakuwahi kuona mapungufu ya CCM ili kuishauri CCM!

Leo yuko kwenye kijiwe ameanza kuona mapungufu ya CCM!

Kwa hiyo Membe wakati akiwa kwenye serikali na kuishi angani hakujua kuwa, ''Siasa ya Ujamaa kwenye vitabu na Soko huria kwenye maisha ya kila siku.Wapi na Wapi?''

Ukichunguza utagundua kuwa msingi wa andiko lake lipo kwenye maneno haya' Tumejiondoa kwenye Open Government Forum ya Umoja wa Mataifa. Yaani hatutaki tufuatwe fuatwe kuhusu Good Governance na haki za binadamu''. Haya mengine ni porojo tu za kuficha lengo lake kuu.

Open Government partnership ilikuwa legacy ya Membe na kundi lake na ndiyo ilimfanya kuishi angani huku akihudhuria mikutano na makongamano ya Open Government partnership.

Kuitetea hoja yake ya Open Government Partnership anataka kutuambia eti Algeria Ethiopia, Angola and et al zenyewe zinaweza kujitoa kwa sababu resources zake zimeshakuwa tapped! Ni resources zipi hizo zilizokuwa tapped ambazo Tanzania hazijakuwa tapped?

Masuala sijui ya Morroco akaihoji AU ambayo imeitambua Morocco na kuipa uanachama wa AU.

Katiba ya CCM katika Ibara ya 122(4) inasema, ‘’Manaibu Katibu Mkuu wa CCM watakuwa ndio wasaidizi wakuu wa Katibu Mkuu wa CCM na watafanya kazi zozote za CCM watakazopangiwa na Katibu Mkuu wa CCM’’.

Maneno ya msingi katika ibara hii ni watafanya kazi zozote za CCM watakazopangiwa na Katibu Mkuu wa CCM.

Tanzania bila unafiki haiwezekani!

Umeandika kichuki zaidi na wivu, kinachokuuma wewe ni jinsi membe alivyokua anasafiri kwenda ulaya una chuki kali sn nyie ndo mnaofurahia watu waishi kama mashetani, akili bure kabisa
 
Sijawahi kuwa mdaku na kwa bahati nzuri sina tabia ya kuwa mshabiki.

Unasema Membe hakuvuka tano bora?hujawahi kushangaa Makamu Mwenyekiti hakuvuka kwenye mchujo hata wa awali 1995 na akawa Makamu mwenyekiti..!

Kuwa 'Mtu wa chama' haimaanishi lazima upate cheo Serikalini kama qualification.

Kolimba kawa Katibu mkuu na hakuwa na kofia ya chama. Kawawa 'kashushwa' kutoka Uwaziri Mkuu mpaka kuwa Waziri wa kawaida lakini alikuwa 'heavy weight' kwenye chama
Umechambua vizuri.Ninakuelewa sana.
 
Kwanini asitoke kifua mbele yeye mwenyewee membe tumuone,! Huo ndo unafiki wenyewe toka mbele na so kujificha nyuma ya keyboard
 
MNAOTAKA MIAKA SABA NDIO MTAJUA WATAKAOPINGA MIAKA SABA YA MKUU NI CCM WENYEWE.CHEO KITAMU!! MAZOEZI YA WALIOKUWA WAMESTAAFU YANAANZA.TANZANIA TAMU!!!
 
Sijawahi kuwa mdaku na kwa bahati nzuri sina tabia ya kuwa mshabiki.

Unasema Membe hakuvuka tano bora?hujawahi kushangaa Makamu Mwenyekiti hakuvuka kwenye mchujo hata wa awali 1995 na akawa Makamu mwenyekiti..!

Kuwa 'Mtu wa chama' haimaanishi lazima upate cheo Serikalini kama qualification.

Kolimba kawa Katibu mkuu na hakuwa na kofia ya chama. Kawawa 'kashushwa' kutoka Uwaziri Mkuu mpaka kuwa Waziri wa kawaida lakini alikuwa 'heavy weight' kwenye chama
Hoja yako hapa ni nini?

Ni Makamu mwenyekiti yupi huyo ambaye hakuvuka kwenye tano bora mwaka 1995?

Kwamba unataka kuniambia Makamu Mwenyekiti ndiye ''mwenye chama''?

Ni wapi nimesema Makamu Mwenyekiti ndiye ''mwenye chama''?
 
Bernad Membe iwapo leo atapotea au kupigwa risasi itakuwa pigo kubwa kwa
wana Ccm wote wanaofikiri bado wanaweza kushawishi direction ya ccm na nchi
naona bado wako in denial....
waamke nyakati zishabadilka...sauti zao hazihitajiki sana now
Hata hivyo mnawakaribisha huko chadomo
 
Ni wewe utakaeamua kuona ni nini anataka, mimi nimeona kuna misingi anataka Ccm isimamie hili Ccm ifanane na vyama vya kijamaa.
Wewe umeona analilia madaraka, ni chaguo lako.
nimesema ni matokeo ya uzoefu wa wwanasiasa wetu inabidi pia kuwasoma pande zote ingawa wote tunaweza tusiwe sahihi. ni kama mtu kusema A akiwa pembeni akijumuishwa anasema ile A ilimaanisha B.
Kuhusu uwepo wa matatizo au hayapo kwa maana ya misingi anayoitetea wahusika aliowalenga wanafahamu zaidi. ILA kwa maoni yangu Mabadiliko hata kama yakihitaji kupolish misingi outdated ideologies ni sawa tu ila yafanyike kupitia change management system ya chama husika sio mtu mmoja maana wenda kuna vitu vinaweza kuwa overlooked.
ila ninachofahamu hakuna pure socialist wala communist party dunianI.
Ndio maana CCP YA MAO ni tofauti kabisa na ya DENG. Hasa kuhusu mahusiano ya kimataifa.
 
Mimi sina tatizo na wale wanaoikosoa CCM kwa sababu bila kukosolewa haiwezi kujitathmini, tatizo langu ni hawa wakosoaji wa kinafiki au wanaokosoa baada ya maslahi yao binafsi ndani ya CCM kuzibwa.

Benard Membe wakati akiishi angani na kubadilisha mabegi uwanja wa ndege hakuwahi kuona mapungufu ya CCM ili kuishauri CCM!

Leo yuko kwenye kijiwe ameanza kuona mapungufu ya CCM!

Kwa hiyo Membe wakati akiwa kwenye serikali na kuishi angani hakujua kuwa, ''Siasa ya Ujamaa kwenye vitabu na Soko huria kwenye maisha ya kila siku.Wapi na Wapi?''

Ukichunguza utagundua kuwa msingi wa andiko lake lipo kwenye maneno haya' Tumejiondoa kwenye Open Government Forum ya Umoja wa Mataifa. Yaani hatutaki tufuatwe fuatwe kuhusu Good Governance na haki za binadamu''. Haya mengine ni porojo tu za kuficha lengo lake kuu.

Open Government partnership ilikuwa legacy ya Membe na kundi lake na ndiyo ilimfanya kuishi angani huku akihudhuria mikutano na makongamano ya Open Government partnership.

Kuitetea hoja yake ya Open Government Partnership anataka kutuambia eti Algeria Ethiopia, Angola and et al zenyewe zinaweza kujitoa kwa sababu resources zake zimeshakuwa tapped! Ni resources zipi hizo zilizokuwa tapped ambazo Tanzania hazijakuwa tapped?

Masuala sijui ya Morroco akaihoji AU ambayo imeitambua Morocco na kuipa uanachama wa AU.

Katiba ya CCM katika Ibara ya 122(4) inasema, ‘’Manaibu Katibu Mkuu wa CCM watakuwa ndio wasaidizi wakuu wa Katibu Mkuu wa CCM na watafanya kazi zozote za CCM watakazopangiwa na Katibu Mkuu wa CCM’’.

Maneno ya msingi katika ibara hii ni watafanya kazi zozote za CCM watakazopangiwa na Katibu Mkuu wa CCM.

Tanzania bila unafiki haiwezekani!
Hata Polepole juzi alinukuliwa na EATV kuwa wakati mh Rais yupo nje ya uongozi wa chama aliweza kubaini mapungufu mengi yalikuwa ndani ya chama kwahiyo ni vyema kuishi na kuskiliza wengine wanakosoa kipi kwa faidi
 
Back
Top Bottom