Bernard Membe: Polepole apelekwe shule kuijua vyema itikadi ya CCM. Ni ajabu Kamati Kuu kukaa bila Katibu Mkuu

Mkuu;
Hoja hujibiwa kwa hoja. Sasa hapa hao BAWACHA umewaona wapi? Pepo kivuruga amekuingia lini?? Si uwaache wenye hekima wamjibu?? Kweli, sikio la kufa halisikii dawa. Mkiisha guswa na kaukweli kidogo tu mnakimbilia kuvuruga mada ili tusielewe. Swali ni kwamba; Ni kikao gani kilimtoa Kinana?? Au ndo unataka kutudokezea kwamba keshakatwa mkia kisailensa!!! Aksante kwa tetesi zako ila tunangojea jibu la swali la Membe. au naye mmeshamkata mkia
Ukweli unauma Sana mimi ni mwanaccm haya yote aliyoyasema ni ya kweli
 
Mimi nasemaje... vyovyote iwavyo iwe source ni Membe mwenyewe ama kuna mtu kujivisha viatu vya Membe, the message is well constructed and has meaning. Membe pengine sasa ana react kutokana na machungu fulani, wacha haya nimeipenda analysis yake ya hali yetu ya kisiasa na kidiplomasia ni hali mbaya sana, huu ndiyo ukweli. Haya ndiyo matatizo ya kumfungua jini alofungwa kwenye chupa, ukadhani jini akitoka atakuwa binadamu. Tuendelee kujadiliana zaidi na zaidi ili tuone how we can yet again contain the devil into the bottle where he deserves to be. Amen.
wamemfungua jini kwenye chupa halafu wanalalamika?
 
Benard Membe ni mwanadiplomasi mwenye heshima yake, tupe source ya alipoandika hayo, makala imetoka wapi!
ungesem ani mwana diplomasia tuu ,hilo la heshima ya pekee achana nalo wewe kijana.Huwa laana zenu waafrica haswa wajamaa ni kuapa na kushudia vitu msivyovijua na vya watu wengine.Kuna wapuuzi waliapa sana kuhusu Lipumba na Mhongo.Kuwa wanahitajika kimataifa ktk issue za uchimi na miamba km uprofessor wao unavyojisibu. viapo vyao vyote ni laana.Hao jamaa hawana thamani yoyote popote nja ya ccm na machinery zao za propaganda. NDio maana sasa hivi wanafanya kazi haramu na sio kumsaidia hata huyo wa ccm ktk kuleta viwanda au uchumi wa gesi.
 
Benard Membe wakati akiishi angani na kubadilisha mabegi uwanja wa ndege hakuwahi kuona mapungufu ya CCM ili kuishauri CCM!
Leo yuko kwenye kijiwe ameanza kuona mapungufu ya CCM!
Kwa hiyo Membe wakati akiwa kwenye serikali na kuishi angani hakujua kuwa, ''Siasa ya Ujamaa kwenye vitabu na Soko huria kwenye maisha ya kila siku.Wapi na Wapi?''!

Unaweza kujiuliza hivyo hivyo kwa Magufuli. Aliyekuwa ndani ya serikali kwa miaka 20. Kila siku anasema kuwepo kwake ndani ya serikali kumemfanya kujua madudu yote, kujua jinsi fedha zinavyoliwa na kuibiwa n.k. Sasa jiulize, alikuwa wapi siku zote kusema hayo madudu mpaka aje kutoa povu sasa hivi? Maagufuli alikuwa msifiaji mzuri wa hao walioishi angani na kubadilisha mabegi airport! Leo anawaponda!

Kama ulivyosema mwisho wa post yako, "Tanzania bila unafiki haiwezekani"

Open Government partnership ilikuwa legacy ya Membe na kundi lake na ndiyo ilimfanya kuishi angani huku akihudhuria mikutano na makongamano ya Open Government partnership.!

Chifu, ebu sahau juu ya Membe na unafiki wake! Wewe unaona ni sawa kwa serikali kujitoa kwenye uendeshaji wa serikali kwa uwazi? Kwanini serikali ifanye mambo yake gizani? Sisi kama walipa kodi tuna haki ya kufahamu yanayoendelea serikalini. Magufuli ana sensible justifications zozote za kujitoa?

Katiba ya CCM katika Ibara ya 122(4) inasema, ‘’Manaibu Katibu Mkuu wa CCM watakuwa ndio wasaidizi wakuu wa Katibu Mkuu wa CCM na watafanya kazi zozote za CCM watakazopangiwa na Katibu Mkuu wa CCM’’.

Maneno ya msingi na muhimu katika ibara hii ni watafanya kazi zozote za CCM watakazopangiwa na Katibu Mkuu wa CCM!

Umesema kazi watakazopangiwa na Katibu Mkuu! Je, tuna uhakika Katibu Mkuu aliwapangia hizo kazi?

Tanzania bila unafiki haiwezekani!

Kabisa! Kuanzia Rais Magufuli hadi wapiga kura.
 
Uchambuzi wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni Mstaafu Bernard Kamilius Membe juu ya mwenendo wa CCM chini ya Mwenyekiti Rais Magufuli na Katibu wa Itikadi na Uenezi H.Polepole.

1. VYAMA BORA.

Sanctity(usafi, utakatifu) Ideology (Itikadi, dira) na Organization( Mfumo.) Cold War iliigawa Dunia kwenye Makundi Mawili. East and West, yaani Wakomunist/ Wajamaa(East) vis a vis Capitalism.(West)(1) Vyama vya nchi za kibepari ni tofauti kabisa na vyama vya Kikomunist/ Kijamaa. Vyama vya kibepari vipo pale kwa ajili ya kuandaa kampeni na fedha kwa ajili ya kushinda uchaguzi ujao.

Mwenyekiti wa Chama hawi Rais. Ni Mtu anachaguliwa na mkutano Mkuu (Congress). Kazi zake ni tatu. 1. Kuandaa mkutano ujao wa Uchaguzi. 2. Kukusanya fedha za uchaguzi.3. Kuendesha mikutano ya Primaries(ya mchujo ).

Wanachama ni mashabiki wowote wa kadi tu wa mrengo huo. Mashabiki ndiyo wanatoa fedha za kumsaidia Mbunge ashinde uchaguzi. Mbunge hatoi fedha ili kupata Ubunge.Ndiyo maana husikii sana maneno ya rushwa.Kwa kifupi vyama vya kibepari havina mifumo kama ya vyama vyetu vya mrengo wa Kikomunist/ Kijamaa. Ni kwenye Mabunge yao tu ndiko vyama vyao huo na mfumo wa Party Caucus na vinajitokeza kupambana na wenzao. Na hata huko Bungeni, Mbunge anaweza ku- cross the party line yaani akaunga hoja ya upande mwingine na bado akabaki kwenye Chama chake.

Wabunge hao huitwa "rebels."(waasi)Hawafukuzani. Vyama cha kibepari havina mfumo unaolingana na Serikali wala kuwa na structure za Politburo, Central Committee au NEC. Wana mikutano ya Congress tu. Vyama cha havishiki hatamu za Uongozi. Rais akichaguliwa wanachama hawana lao tena. Wanawaachia wanachama wao Bungeni. Kwenye ngazi za Mikoa hivyo hivyo.Vyama havishiki hatamu. Hii ni part one.

Part two ndiyo inayotuhusu sisi. Hapa nitachambua sanctity, ideology na organisation na ubora wa vyama vyetu.

2. Vyama Vyetu. Ubora wa vyama vyetu vyenye uasilia wa Ukomunisti/ Ujamaa unategemea ushindi wake kwenye vigezo vitano vifuatavyo:

1. Clarity kwenye Itikadi yake. 2. Historia yake iliyotukuka. 3. Mfumo wake. 4. Wanachama wake. 5. Alama/ nembo za utambulisho wake. 1.Je Chama na Serikali yetu inafuata Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea? Ni kitendawili. Azimio la Arusha lipo? Wenzetu Wachina, Wacuba, Warusi, Wa Algeria, Waangola, wapo very clear! Ni Wajamaa kwa maneno na vitendo na Dunia inawatambua hivyo. Sisi tumeandika siasa yetu ni ya Ujamaa lakini tuna practise Free Market Economics ( soko huria)na Azimio la Arusha ni historia. Tunawashindaje hao vingunge kwa hili. 2. HISTORIA. Hapa ndipo penye nguvu ya CCM. Chama chetu kina historia ya Ukombozi kwa nchi yetu na nchi zinazotuzunguka. Heshima yetu ipo kwenye historia. Yaani Uzamani wetu. Huwezi kufuta Uzamani huo ukaleta Upya. Kufanya hivyo ni kujiua.Hapo tumewapiku wengi isipokuwa Cuba. 3.MFUMO. Wenzetu wana Politburo, Central Committee, NEC na Congress.Na wengi wa wanachama wana kofia mbili mbili.

Wajumbe wa Kamati juu kwa mfano, kuna mawaziri, Mabalozi na makatibu wakuu. Balozi Lukoki wa Angola nchini Tanzania kwa mfano, ni mjumbe wa Kamati juu ya MPLA. Wanafanya hivyo ili kuziongoza na kuzishauri Serikali zao ndani kwa ndani. Hawasubiri vikao. Sisi tunauondoa utaratibu huo. Nafasi yetu ya pili inatokana na nini? Mfumo wetu wa kutenganisha kofia? Aidha wenzetu wana utaratibu wa kusimamisha wagombea bila ya kuwashindanisha na wenzao wa Chama hicho hicho kwa baadhi ya majimbo wanayoamini wabunge wao wanafanya vizuri. Ni yale tu ambayo yana Wabunge lege lege ndiyo wanashindanisha wagombea kutoka Chama kimoja. Faida ya utaratibu huo ni kuleta Umoja ktk Chama, kutambua Wabunge wanaofanya vizuri na utaratibu huo unapunguza tuhuma au vitendo vya rushwa. Sisi hatufanyi hivyo. Tunapambanisha wagombea wetu ktk kila jimbo, vitendo vya rushwa vinakithiri,na wengine wanafitinishwa hata kama hawatoi rushwa n.k. Je hiki ni kigezo kinachotupa sifa Duniani? Wenzetu hawakubaliani nasi kwa hili.

4. WANACHAMA.

Sisi Chama chetu ni Mass party. Yaani "kumbakumba", ni Chama cha wengi na ili uwe mwanachama, wala jina lako haliendi Central Committee kuchunguzwa na kisha kupewa kadi ya Uanachama. Sisi ni matakwa yako. Hata mtu wa chama cha Upinzani kwa kutumwa au kujituma anaweza kujiunga na Chama chetu siku yoyote tena kwa sherehe na nderemo.Wenzetu kamwe hawafanyi hivyo. Utakuwa vetted ( kuchunguzwa kwa kina) kabla ya ombi lako la kutaka kujiunga na Chama kukubaliwa. Je hii ndiyo sifa inayotupa nafasi ya Ubora Duniani? Wenzetu hawakubali.

5. MAVAZI/ NEMBO. Kila Chama hujitambulisha kwa Mavazi na Nembo. Vitu hivi ni muhimu lakini hatushindanishwi navyo. La muhimu hapa ni kujua kuwa upya wa Chama hauwi kwenye mavazi, wala nembo wala watu wapya. Upya wa Chama chochote Duniani upo kwenye Historia yake, Itikadi yake na mfumo wake. Kama vitu hivyo vitatu ni constant ( yaani havibadiliki) badala yake tunabadilisha nembo, mavazi na watu, Chama chetu kitakuwa bado ni kile kile. Hakiwi kipya. Uzamani wa Chama ni kama mvinyo. Mvinyo wa zamani ni mtamu sana na una bei kubwa kuliko mpya. Nirudi kwenye hoja na nimalizie. Chama chetu lazima kiwe clear na Historia yake, Itikadi yake na Mfumo wake.

Historia yetu ipo clear lakini lazima tuiishi! Tukasema nini kuhusu Palestine, na Western Sahara kwa mfano. Vinginevyo tutakuwaje wa pili kwa Ubora? Tumejiondoa kwenye Open Government Forum ya Umoja wa Mataifa. Yaani hatutaki tufuatwe fuatwe kuhusu Good Governance na haki za binadamu. Tutasifiwaje? Pili Itikadi yetu haijawa clear. Tupo kama popo! Hatueleweki kama sisi ni ndege au Wanyama! Siasa ya Ujamaa kwenye vitabu na Soko huria kwenye maisha ya kila siku.Wapi na Wapi? Tukitangaza kuwa sisi tunafuata Siasa ya Ujamaa na tunarudisha Azimio la Arusha, Investors wote watakimbia kama bado hawajaanza. Ni itikadi gani tunayosifiwa nayo? Wenzetu China, Urusi, N.Korea, Cuba, Algeria,Ethiopia na Angola wana resources ambazo zipo tapped tayari na wanajitegemea. Ndiyo maana wametamka na kuyaishi matamko yao ya kufuata itikadi ya kikomunisti. Sisi hatujawa clear! Hatuwezi kuwashinda.

Mfumo wetu lazima uendane na maamuzi ya pamoja. Ni kikao gani kimeamua nini, lini, na kwa nini. Hakuna uamuzi wa mtu mmoja wala usio na kikao cha kikatiba. Kule Nje kwa hao wenzetu, kama Party Secretary General Hayupo kwa sababu yoyote ile, Central Committee haifanyiki siku hiyo.

The Party Secretary General is indispensable. Baada ya yote hayo, najiuliza ni kipi kinachofanya CCM iwe na Ubora wa pili baada ya China? Chama chetu lazima kipeleke vijana viongozi kama ndugu yetu Polepole Urusi, Cuba, N.Korea, Algeria, Angola, na Ethiopia ili kujifunza zaidi kwa faida ya Chama chetu na Taifa kwa ujumla.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
Mwambie tumemsikia!miaka 40 us CCM bado anamawazo ya kuwapeleka watu Algeria....Angola...Cuba...nk wakajifunze?
 
Huyo sijui kama kweli ni Membe otherwise is out of phase by half lamda.
Sijui tatizoni mazoea ya kula bila kunawa anashindwa hata ku copy and paste kama wengine mangumasha.
How such loosy guy happen to be our foreign Minister?Time is over for you Mr.Membe.
Bado huelewi kwanini CCM ilikubali kufanya mapinduzi ya sera ndani ya chama kukumbatia multiparty?
The fall of USSR,IMF,World Bank,President Reagan,na Margaret Thather the milky snather zilifanya mchonga asalimu amri.
CCM haiwezi kutumia chupa na mfinyo ya zamani haitapasua, ni mvinyo mpya na chupa mpya.Yawezekana humtakii mema mwenyekiti wako wa CCM.Wakinadi sera hizo za zidumu fikra za mwenyekiti bila utashi na maono kwa wananchi CCM haitapasua

Kama haitoshi bado unakumbatia baadhi ya mataifa yenye viongozi wajamaa makapi,waliotawala bila ndululu lakini wamejimilikisha mali zote za nchi kwa familia kama Angola.Ni wakwasi wakubwa duniani,yasadikika wanaongoza,wakati wananchi wa Angola wanamaisha ya chini na taabu sana.Kwa hilo wazo tumeishtukia kama mabulungutu uliomwaga Dodoma yaliganda kama vipande vya barafu kali.

Ukitaka kurudi kundini kama mwana mpotovu,tubu kwanza uzandiki wako uliofanya,rudisha mali za umma na visanga vyote vya Libya,yawezekana ukafungwa jela ngumu sijui miaka 50,kama ukitoka hai,waombe msamaha wananchi kwanza.
 
Membe baelezee malimbukeni na washamba kwani hawapendi hii mambo.
 
Ila mrangi tusimuamini sana maembe tusiwe wepesi wa kusahau... Utawala wao ndio umetuletea hii shida tuliyinayo sasa..... Na bado ana vidonda vya kukosa urais
Kwenye haya madongo yake tunapaswa kumwangalia kwa tafakuri
Anaweza akawa ametumwa kama mamluki syo

Ova
 
Uchambuzi wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni Mstaafu Bernard Kamilius Membe juu ya mwenendo wa CCM chini ya Mwenyekiti Rais Magufuli na Katibu wa Itikadi na Uenezi H.Polepole.

1. VYAMA BORA.

Sanctity(usafi, utakatifu) Ideology (Itikadi, dira) na Organization( Mfumo.) Cold War iliigawa Dunia kwenye Makundi Mawili. East and West, yaani Wakomunist/ Wajamaa(East) vis a vis Capitalism.(West)(1) Vyama vya nchi za kibepari ni tofauti kabisa na vyama vya Kikomunist/ Kijamaa. Vyama vya kibepari vipo pale kwa ajili ya kuandaa kampeni na fedha kwa ajili ya kushinda uchaguzi ujao.

Mwenyekiti wa Chama hawi Rais. Ni Mtu anachaguliwa na mkutano Mkuu (Congress). Kazi zake ni tatu. 1. Kuandaa mkutano ujao wa Uchaguzi. 2. Kukusanya fedha za uchaguzi.3. Kuendesha mikutano ya Primaries(ya mchujo ).

Wanachama ni mashabiki wowote wa kadi tu wa mrengo huo. Mashabiki ndiyo wanatoa fedha za kumsaidia Mbunge ashinde uchaguzi. Mbunge hatoi fedha ili kupata Ubunge.Ndiyo maana husikii sana maneno ya rushwa.Kwa kifupi vyama vya kibepari havina mifumo kama ya vyama vyetu vya mrengo wa Kikomunist/ Kijamaa. Ni kwenye Mabunge yao tu ndiko vyama vyao huo na mfumo wa Party Caucus na vinajitokeza kupambana na wenzao. Na hata huko Bungeni, Mbunge anaweza ku- cross the party line yaani akaunga hoja ya upande mwingine na bado akabaki kwenye Chama chake.

Wabunge hao huitwa "rebels."(waasi)Hawafukuzani. Vyama cha kibepari havina mfumo unaolingana na Serikali wala kuwa na structure za Politburo, Central Committee au NEC. Wana mikutano ya Congress tu. Vyama cha havishiki hatamu za Uongozi. Rais akichaguliwa wanachama hawana lao tena. Wanawaachia wanachama wao Bungeni. Kwenye ngazi za Mikoa hivyo hivyo.Vyama havishiki hatamu. Hii ni part one.

Part two ndiyo inayotuhusu sisi. Hapa nitachambua sanctity, ideology na organisation na ubora wa vyama vyetu.

2. Vyama Vyetu. Ubora wa vyama vyetu vyenye uasilia wa Ukomunisti/ Ujamaa unategemea ushindi wake kwenye vigezo vitano vifuatavyo:

1. Clarity kwenye Itikadi yake. 2. Historia yake iliyotukuka. 3. Mfumo wake. 4. Wanachama wake. 5. Alama/ nembo za utambulisho wake. 1.Je Chama na Serikali yetu inafuata Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea? Ni kitendawili. Azimio la Arusha lipo? Wenzetu Wachina, Wacuba, Warusi, Wa Algeria, Waangola, wapo very clear! Ni Wajamaa kwa maneno na vitendo na Dunia inawatambua hivyo. Sisi tumeandika siasa yetu ni ya Ujamaa lakini tuna practise Free Market Economics ( soko huria)na Azimio la Arusha ni historia. Tunawashindaje hao vingunge kwa hili. 2. HISTORIA. Hapa ndipo penye nguvu ya CCM. Chama chetu kina historia ya Ukombozi kwa nchi yetu na nchi zinazotuzunguka. Heshima yetu ipo kwenye historia. Yaani Uzamani wetu. Huwezi kufuta Uzamani huo ukaleta Upya. Kufanya hivyo ni kujiua.Hapo tumewapiku wengi isipokuwa Cuba. 3.MFUMO. Wenzetu wana Politburo, Central Committee, NEC na Congress.Na wengi wa wanachama wana kofia mbili mbili.

Wajumbe wa Kamati juu kwa mfano, kuna mawaziri, Mabalozi na makatibu wakuu. Balozi Lukoki wa Angola nchini Tanzania kwa mfano, ni mjumbe wa Kamati juu ya MPLA. Wanafanya hivyo ili kuziongoza na kuzishauri Serikali zao ndani kwa ndani. Hawasubiri vikao. Sisi tunauondoa utaratibu huo. Nafasi yetu ya pili inatokana na nini? Mfumo wetu wa kutenganisha kofia? Aidha wenzetu wana utaratibu wa kusimamisha wagombea bila ya kuwashindanisha na wenzao wa Chama hicho hicho kwa baadhi ya majimbo wanayoamini wabunge wao wanafanya vizuri. Ni yale tu ambayo yana Wabunge lege lege ndiyo wanashindanisha wagombea kutoka Chama kimoja. Faida ya utaratibu huo ni kuleta Umoja ktk Chama, kutambua Wabunge wanaofanya vizuri na utaratibu huo unapunguza tuhuma au vitendo vya rushwa. Sisi hatufanyi hivyo. Tunapambanisha wagombea wetu ktk kila jimbo, vitendo vya rushwa vinakithiri,na wengine wanafitinishwa hata kama hawatoi rushwa n.k. Je hiki ni kigezo kinachotupa sifa Duniani? Wenzetu hawakubaliani nasi kwa hili.

4. WANACHAMA.

Sisi Chama chetu ni Mass party. Yaani "kumbakumba", ni Chama cha wengi na ili uwe mwanachama, wala jina lako haliendi Central Committee kuchunguzwa na kisha kupewa kadi ya Uanachama. Sisi ni matakwa yako. Hata mtu wa chama cha Upinzani kwa kutumwa au kujituma anaweza kujiunga na Chama chetu siku yoyote tena kwa sherehe na nderemo.Wenzetu kamwe hawafanyi hivyo. Utakuwa vetted ( kuchunguzwa kwa kina) kabla ya ombi lako la kutaka kujiunga na Chama kukubaliwa. Je hii ndiyo sifa inayotupa nafasi ya Ubora Duniani? Wenzetu hawakubali.

5. MAVAZI/ NEMBO. Kila Chama hujitambulisha kwa Mavazi na Nembo. Vitu hivi ni muhimu lakini hatushindanishwi navyo. La muhimu hapa ni kujua kuwa upya wa Chama hauwi kwenye mavazi, wala nembo wala watu wapya. Upya wa Chama chochote Duniani upo kwenye Historia yake, Itikadi yake na mfumo wake. Kama vitu hivyo vitatu ni constant ( yaani havibadiliki) badala yake tunabadilisha nembo, mavazi na watu, Chama chetu kitakuwa bado ni kile kile. Hakiwi kipya. Uzamani wa Chama ni kama mvinyo. Mvinyo wa zamani ni mtamu sana na una bei kubwa kuliko mpya. Nirudi kwenye hoja na nimalizie. Chama chetu lazima kiwe clear na Historia yake, Itikadi yake na Mfumo wake.

Historia yetu ipo clear lakini lazima tuiishi! Tukasema nini kuhusu Palestine, na Western Sahara kwa mfano. Vinginevyo tutakuwaje wa pili kwa Ubora? Tumejiondoa kwenye Open Government Forum ya Umoja wa Mataifa. Yaani hatutaki tufuatwe fuatwe kuhusu Good Governance na haki za binadamu. Tutasifiwaje? Pili Itikadi yetu haijawa clear. Tupo kama popo! Hatueleweki kama sisi ni ndege au Wanyama! Siasa ya Ujamaa kwenye vitabu na Soko huria kwenye maisha ya kila siku.Wapi na Wapi? Tukitangaza kuwa sisi tunafuata Siasa ya Ujamaa na tunarudisha Azimio la Arusha, Investors wote watakimbia kama bado hawajaanza. Ni itikadi gani tunayosifiwa nayo? Wenzetu China, Urusi, N.Korea, Cuba, Algeria,Ethiopia na Angola wana resources ambazo zipo tapped tayari na wanajitegemea. Ndiyo maana wametamka na kuyaishi matamko yao ya kufuata itikadi ya kikomunisti. Sisi hatujawa clear! Hatuwezi kuwashinda.

Mfumo wetu lazima uendane na maamuzi ya pamoja. Ni kikao gani kimeamua nini, lini, na kwa nini. Hakuna uamuzi wa mtu mmoja wala usio na kikao cha kikatiba. Kule Nje kwa hao wenzetu, kama Party Secretary General Hayupo kwa sababu yoyote ile, Central Committee haifanyiki siku hiyo.

The Party Secretary General is indispensable. Baada ya yote hayo, najiuliza ni kipi kinachofanya CCM iwe na Ubora wa pili baada ya China? Chama chetu lazima kipeleke vijana viongozi kama ndugu yetu Polepole Urusi, Cuba, N.Korea, Algeria, Angola, na Ethiopia ili kujifunza zaidi kwa faida ya Chama chetu na Taifa kwa ujumla.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
La MAWAZIRI nimeelewa lakini La MAKATIBU WAKUU kwenye siasa sijalielewa.
 
Andiko zuri, lilijaa ubobevu. Nashawisha kuamini kuwa kwa level ya kufikiri inafana na mtu aliyewahi kuwa Mwanadiplomasia mzoefu na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Lakini bado sijawashawisha na source ya hilo andiko.

hata mimi nashawishika na content, lakini je source?
 
Back
Top Bottom