Benki Kuu: Shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusiwa kutumika nchini

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
1687263055475.png

Benki Kuu ya Tanzani imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusia kutumika nchini, hivyo hakuna Mtu au Kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa kwa malipo yoyote halali na kwamba kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya Tanzania ni kuvunja Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuukumbusha umma kwamba Serikali ilishatoa tamko kuhusu katazo la matumizi ya fedha za kigeni kwa Wakaazi wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma nchini, tamko la kwanza lilitolewa mwezi Agosti 2007 na la pili mwezi Desemba 2017”

“Hata hivyo, katika siku za karibuni imebainika kuwepo kwa ukiukwaji wa tamko hilo, hivyo Benki Kuu inapenda kuukumbusha umma kwamba maagizo yaliyotolewa hapo awali kuhusu matumizi ya fedha za kigeni yanapaswa kuendelea kuzingatiwa kuwa bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania, bei hizi zinajumuisha kodi za kupangisha ardhi, nyumba na ofisi, gharama za elimu, huduma za afya, vifaa tiba na vitendanishi, gharama za usafiri, lojistiki za bandari, vifaa vya kielektroniki na huduma za mitandao ya mawasiliano”

“Bei ambazo walengwa wake Wakuu ni Watalii au Wateja wasio Wakaazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni, bei hizi zinajumuisha gharama za hoteli, usafiri, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa Wageni, usafirishaji kwenda Nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za mizigo bandarini”
 
Pesa ya madafu, milioni moja tu inakukosesha raha kuibeba.

weak currency!
 
Inabidi tuiteme tu hii shilingi haina faida yoyote kwa uchumi wa Tanzania.
Nashauri tuanze kutumia Rial au Dirham
 
Benki Kuu ya Tanzani imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusia kutumika nchini, hivyo hakuna Mtu au Kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa kwa malipo yoyote halali na kwamba kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya Tanzania ni kuvunja Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.
nda Nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za mizigo bandarini”
Wanamaanisha nini?
 
Benki Kuu ya Tanzani imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusia kutumika nchini, hivyo hakuna Mtu au nda Nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za mizigo bandarini”
Mbona serikali inasema imeishiwa Dollar kwenye akiba yake? Mbona watu wanafanya online purchases kwa kutumia USD, GBP, nk?
 
ZAMBIA WALIKUWA NA WEAK CURRENCY KAMA YA HUKO MIAKA YA NYUMA WAKABADILISHA NA KUPUNGUZA 000
SASA HIVI HELA YAO INAFANANA NA RAND YA KWA MADIBA.

KAMA BENKI KUU INAPENDA HIZI HELA, KWANINI WASIPUNGUZE 0 MOJA TU KWENYE NOTI NA WARUDISHE SARAFU YA SHILLINGI 10,20 ILI TUPUNGUZE KUTESEKA NA MANOTI HAYA.

YANI MTU UKITOA MILLION 5 BENKI UNAKOSA AMANI JINSI ILIVYOTUNA MIFUKONI NA KUWAZA KUPORWA NA VIBAKA WAKIDHANI UNA 20Millions
 
1687260852764.png

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema hakuna mtu au kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa shilingi ya Tanzania kwa malipo yoyote halali, kwani ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusiwa kutumika nchini.

Katika taarifa yake imesema Serikali ilishatoa tamko kuhusu katazo la matumizi ya fedha za kigeni kwa wakazi wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma nchini, na kwamba kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya Tanzania ni kuvunja sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

“Benki Kuu inapenda kuukumbusha umma kwamba maagizo yaliyotolewa hapo awali kuhusu matumizi ya fedha za kigeni yanapaswa kuendelea kuzingatiwa kuwa bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania, bei hizi zinajumuisha kodi za kupangisha ardhi, nyumba na ofisi, gharama za elimu, huduma za afya, vifaa tiba na vitendanishi, gharama za usafiri, lojistiki za bandari, vifaa vya kielektroniki na huduma za mitandao ya mawasiliano,” imesema taarifa ya BoT.
 
ila dola jaman
yan ukiw na noti 50 tu za dola 100 ni sawa na manot ya TZ kamzigo kakutosha
 

Benki Kuu ya Tanzani imeukumbusha umma kuwa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo inaruhusia kutumika nchini, hivyo hakuna Mtu au Kampuni yoyote inayoruhusiwa kuikataa kwa malipo yoyote halali na kwamba kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya Taji kwenda Nchi za nje kupitia Tanzania na gharama za mizigo bandarini”
Wafannya biiasahara wanachukulia advantage ya week admistration wanajua mama hana gut. Za kusimamia hayo matamko
 
Back
Top Bottom