Benki ipi na account ipi nzuri kwa sasa?

melech

Member
May 29, 2013
62
25
Amani kwako!

Nataka kufungua account mpya bank, ila naomba nipate ushauri kutoka kwa watu wa profession ya mambo ya banking, kwamba ni benki gani na aina gani ya account nikifungua itakuwa vyema zaidi. Kwa sasa hivi najishuhulisha kwa kazi za kujiajiri mwenyewe, hivyo nikiwa account hii itakuwa ni kwa ajili ya kujikusanyia kile ninachopata kwa kushuhulika huko. Ninaweza nikawa nakusanya humo kwa lengo kuwa kikifika kiwango fulani nikitoe nikipeleke kwenye project nyingine.

Ninajali sana mambo ya makato ya mwezi na ATM charges. Kwa ujumla, najali sana taratibu za bank ambazo 'zinakula' hela yangu humo kama mchwa.

Nadhani kuna mambo mengine pia natakiwa kujali, naomba kuelimishwa. Kisha naomba nishauriwe ni benki gani nzuri na accounts zipi.

Ninaamini hapa watakuwepo watu wenye elimu au uzoefu juu ya hili na nitashukuru kwa elimu hiyo. Lengo langu ni kama nilivyojieleza hapo juu.

Otherwise, M-PESA na Airtel Money ndiyo zili-replace CRDB na NBC kwangu!

Asanteni.
 
NMB wapo vizuri, matawi hadi vijijini, ATM za kutosha, huduma zao pia zimeboreshwa, msongamano wa wateja umepungua baada ya kuongeza matawi zaidi. Hasara yao hawana huduma ya visa card/ master card.

CRDB na wanayo matawi mengi ila hawawazidi NMB, na wenyewe wapo vizuri ila nahisi kwa sasa ni kama vile wamezidiwa wateja, foleni zimezidi zile za NMB hata huduma ya kastama kea sio nzuri tena sababu ya wingi huo wa wateja. Faida yao wana visa / master kadi .

NBC sijawahi kabisa kuwa na akaunti hii benki, sababu sijawahi vutiwa na chochote kweny hii benk, hata hivyo inayo matawi machache na ATM chache kulinganisha na CRDB au NMB. Faida yao pia wana visa/master card.

Vilevile hapo ulipo kama kuna hiz benk ndogo AKIBA bank ,AZANIA bank etc ni nzuri sababu ya uharaka wa huduma zao. Faida yao pia wanatoa mikopo kwa urahisi sana hizi benk ndogo kulinganisha na hizo bank kubwa hapo juu. Hasara wana matawi machache pia na nyingi hazina VISA/ Master kadi.

uzoefu wangu kwa bank hizo ni huo, watakuja wengine kukujuza kuhusu stanbic, standard charted , braclays exim , etc

Makato ya ATM ni lazima sidhan kama kuna benk haichaji kutoa pesa kwenye ATM , pia makato mengine ni ya kila mwezi ya service charge ambayo nayo ni lazima. saving akaunti makato ya kila mwezi ni kidogo kuanzia tsh600, current yanaanzia 5000tsh.
 
Asante sana 'mathematics'.
Ninaona CRDB watanipa advantage ya MasterCard, otherwise NMB wapo vizuri. Labda NMB wataleta MasterCard/VISA in the future.

Asante sana.

yaa mapema mwakani nmb wana launch viza cards na master cards kwa wateja wao.
 
Amani kwako!

Nataka kufungua account mpya bank, ila naomba nipate ushauri kutoka kwa watu wa profession ya mambo ya banking, kwamba ni benki gani na aina gani ya account nikifungua itakuwa vyema zaidi. Kwa sasa hivi najishuhulisha kwa kazi za kujiajiri mwenyewe, hivyo nikiwa account hii itakuwa ni kwa ajili ya kujikusanyia kile ninachopata kwa kushuhulika huko. Ninaweza nikawa nakusanya humo kwa lengo kuwa kikifika kiwango fulani nikitoe nikipeleke kwenye project nyingine.

Ninajali sana mambo ya makato ya mwezi na ATM charges. Kwa ujumla, najali sana taratibu za bank ambazo 'zinakula' hela yangu humo kama mchwa.

Nadhani kuna mambo mengine pia natakiwa kujali, naomba kuelimishwa. Kisha naomba nishauriwe ni benki gani nzuri na accounts zipi.

Ninaamini hapa watakuwepo watu wenye elimu au uzoefu juu ya hili na nitashukuru kwa elimu hiyo. Lengo langu ni kama nilivyojieleza hapo juu.

Otherwise, M-PESA na Airtel Money ndiyo zili-replace CRDB na NBC kwangu!

Asanteni.

Kama unajali sana cost NMB wapo vzr na watakufaa kuhusu visa na masttercard kwa mtu kawaida haina faida yoyote mi nimekuwa na visa card 4rm 2010 na master card lkn sijawahi zitumia, fungua account NMB huta regret kwa makato ya ajabu ajabu
 
Kwa kuongezea walau kwa uchache tu pale alipoishia mathematics, Kuna benki nyingine kama Mkombozi Commercial Bank, FBME, BancABC, Access Bank, DTB, Eco Bank, FNB, FINCA, Maendeleo Bank, Tanzania Women Bank, Covenant Bank, Efatha Bank na nyinginezo, hizi ni benki ndogo kwa maana ya matawi. Na faida kubwa ya hizi benki ni uharaka wa huduma na urahisi wa kupata mikopo.
Uzoefu unaonyesha benki ndogo ziko effective sana linapokuja suala zima la huduma ukilinganisha na hizi kubwa kubwa. Mengine yameshaongelewa.
Ushauri: Fungua account kulingana na unyeti wa shughuli zako. Kama utakuwa unaitumia account hiyo countrywide ni bora kuangalia benki hizi kubwa zilizoainishwa na Mathematics hapo juu ila kama misele yako inaishia Chalinze nakushauri uangalie uwezekano wa kufungua account kwenye hizi benki ndogo ambazo nyingi zina matawi hapa Dar.
Wasalaaaam
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Upcoming!
Ushauri wako ni mzuri, nafikiri nitakwenda huko. Nitahitaji kufanya online transactions in the near future, na kwa kuwa kuna mtu kasema NMB wataleta hizo, basi ni chaguo zima. Narudia kukushukuru.

Kama unajali sana cost NMB wapo vzr na watakufaa kuhusu visa na masttercard kwa mtu kawaida haina faida yoyote mi nimekuwa na visa card 4rm 2010 na master card lkn sijawahi zitumia, fungua account NMB huta regret kwa makato ya ajabu ajabu
 
Hekimatele,
Asante sana kwa ushauri wako mzuri. Mimi sipo Dar hivyo ushauri wako wa kufungua account kwenye hizi benki kubwa naona utanifaa zaidi. Asante sana.
Wasalaam.

Kwa kuongezea walau kwa uchache tu pale alipoishia mathematics, Kuna benki nyingine kama Mkombozi Commercial Bank, FBME, BancABC, Access Bank, DTB, Eco Bank, FNB, FINCA, Maendeleo Bank, Tanzania Women Bank, Covenant Bank, Efatha Bank na nyinginezo, hizi ni benki ndogo kwa maana ya matawi. Na faida kubwa ya hizi benki ni uharaka wa huduma na urahisi wa kupata mikopo.
Uzoefu unaonyesha benki ndogo ziko effective sana linapokuja suala zima la huduma ukilinganisha na hizi kubwa kubwa. Mengine yameshaongelewa.
Ushauri: Fungua account kulingana na unyeti wa shughuli zako. Kama utakuwa unaitumia account hiyo countrywide ni bora kuangalia benki hizi kubwa zilizoainishwa na Mathematics hapo juu ila kama misele yako inaishia Chalinze nakushauri uangalie uwezekano wa kufungua account kwenye hizi benki ndogo ambazo nyingi zina matawi hapa Dar.
Wasalaaaam
 
NMB wapo vizuri na kama ni mfanya biashara wana access ya mikopo mingi na kwa uharaka ikiwa na riba ndogo,pia kama biashara zako ni za ndani basi huitaji hizo Master card na Visa sababu ukizitumia pia zinakuongezea gharama tu,NMB wana matawi kila sehem na ndo Bank pekee inayomiliki ATM yake binafsi Tanzania
 
Back
Top Bottom