Bendera ya Kenya jengo la Burj Khalifa iliwekwa 2019, ni nani amemuongopea Rais wetu kuwa imewekwa karibuni?

Ngoja nikueleweshe

Raisi amesema baada ya malumbano ya bandari huku kwetu, wenzetu(Kenya) walikimbilia hukohuko na bendera yao ikawekwa kwenye jengo kama yetu ilivyowekwa, hivyo wametumia fursa.

Hii haikuwa kweli, bendera ya Kenya jengo la Burj khalifa haujawekwa hivi karibuni, iliwekwa 2019 siku yao ya Uhuru.

Mimi simkosoi raisi kwa hili maana najua huenda hivi vitu havijui, nakosoa watu waliompa hii taarifa.
Sawa humkosoi Ile umeeleza vyema mapungufu yake.
Hivi mtu ana resources kibao at her disposal halafu anaongea vitu kama mtu wa hovyo wa mtaani asiyejua lolote
 
Duh! kimsingi hawezi kujua kila taarifa, hawa wasaidizi wanaomlisha taarifa fake wanachukuliwa hatua gani? maana kumdanganya au kumpotosha rais ni jambo serious.
 
Unajuaje kama amedanganywa na sio yeye kuamua kutudanganya?

Hilo halishangazi (politicians ni waongo by nature) Kinachoshangaza ni kwa Rais kuona hii ni Big Deal !??? Yaani kwamba kule ukiweka bendera yako ndio SI Unit ya kufanikiwa ?!!!!

Nakuacha na Qoute ya Obama kuhusu Politicians and Lies
“Politicians have always lied but it used to be if you caught them lying, they’d be like, ‘oh man.’ Now they just keep on lying.”
EeenHeee Heeeee!

Wewe mkuu 'Lojikos', nawe unakuwa 'politician'?

Mbona unadanganya?

Hivi Ombama kweli anaweza kuyasema hayo maneno kama ulivyoyanukuu?

Mimi nakataa, katakata.
Lakini naomba unielewe ninachozungumzia hapa: sikatai kwamba Obama alizungumzia swala hilo, ila siyo kwa maneno kama ulivyoyawasilisha hapa.
 
Huenda ipo hivyo, swali litabaki je wanamdanganya kwenye haya tu au kuna makubwa zaidi? Kama hili lililo wazi wamedanganya vipi kwenye huo mkataba?
Na huenda ni hao hao waliokuwa wakimdanganya Magufuli,au hii imekuwa ndio tabia yetu "rasmi" ya kujipendekeza na kusema uongo na ulaghai ili tu mkono uende kinywani?!
 
Leo na mimi acha niwaseme washauri wa raisi, imekuwa ipi wanamueleza raisi kuwa bendera imewekwa hivi karibuni wakati bendera ya Kenya iliwekwa 2019??

Raisi amesema sisi tunalumbana huku jirani wenzetu nao wameenda huko na bendera ikawekwa kama sisi tulivyowekwa.

Ni nani wamemueleza bendera imewekwa hivi karibuni? Mmechukua spinning na utani wa mtandaoni wakiwatania wakenya mkahisi ni ya hivi karibuni?

Naamini hili suala kuna waliomshauri mama aligusie bila kujua hili ni la miaka imepita
View attachment 2687987
Nimejiuliza mara mbili mbili, kwamba hata kama imewekwa leo. Je ina faida ipi kwetu ama kwao kama Taifa.?
 
Leo na mimi acha niwaseme washauri wa raisi, imekuwa ipi wanamueleza raisi kuwa bendera imewekwa hivi karibuni wakati bendera ya Kenya iliwekwa 2019??

Raisi amesema sisi tunalumbana huku jirani wenzetu nao wameenda huko na bendera ikawekwa kama sisi tulivyowekwa.

Ni nani wamemueleza bendera imewekwa hivi karibuni? Mmechukua spinning na utani wa mtandaoni wakiwatania wakenya mkahisi ni ya hivi karibuni?

Naamini hili suala kuna waliomshauri mama aligusie bila kujua hili ni la miaka imepita
View attachment 2687987
Mkataba lazima uwe rafiki, vigezo, vipengele na masharti. Pia muhimu kuhusu vizazi, watoto, wajukuu ŵetu.

Usijali nchi nyingine inafanya nini? Hoja za kitoto.
 
Back
Top Bottom