KWELI Kwa nchi za jirani na Tanzania Hakuna bendera ya nchi hizo iliyowahi kuwekwa jengo la Burj Khalifa baada ya Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna wakati jengo la Burj Khalifa lilisambaa mtandaoni likiwa na bendera ya Tanzania na Picha ya Rais, lakini kwa siku za hivi karibuni nimeona tena mitandaoni kuna picha za bendera za majirani zetu zikiwa kwenye jengo hilohilo.

Mjadala wa bendera za nchi za Afrika mashariki kuwekwa kwenye jengo la Burj Khalifa umeshika kasi zaidi mitandaoni leo 14/07/2023 baada ya Rais Samia kudokeza kuwa ipo nchi jirani bendera yake imewekwa pale baada ya kuwapo kwa malumbano ya mkataba wa bandari nchini.

Ukweli wa jambo hili upi?

1689383019235.png

Je, picha za majirani zetu ziliwekwa baada ya Tanzania kuwekwa?
 
Tunachokijua
Burj Khalifa ni Jengo Refu Zaidi Duniani, jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2004 na kufunguliwa rasmi Jan 4 mwaka 2010 huko Dubai na mwanzoni likiitwa Burj Dubai likiwa na urefu wa mita 829.8 sawa na futi 2,716.5

Tanzania imezungukwa na nchi jirani 8 ambazo ni, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DR Congo, Zambia, Malawi na Mozambique.
_128846390_bbcm_tanzania_country_profile_map_020323.jpg
Baada ya kuona taarifa ya kuwekwa kwa bendera za Tanzania pamoja na nchi za jirani JamiiForums ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa, kwa nchi zilizojirani na Tanzania ni nchi 2 tu (Kenya na Uganda)ambazo bendera zake zimewahi kuwekwa kwenye jengo la Burj Khalifa ambapo na Tanzania inakuwa nchi ya Tatu katika ukanda huu.

Je, ziliwekwa lini?

Kenya
Bendera ya nchi ya Kenya ilionekana kulipanda jengo refu zaidi duniani Burj Khalifa tarehe 12, 12, 2019 siku ya uhuru wao wakiadhimisha kutimiza miaka 55 ya uhuru .

F1AT0-mX0AQAPwd


Uganda
Bendera ya Uganda imewahi kuwekwa mara 2 katika jengo la Burj Khalifa.

Mara ya kwanza iliwekwa 9, Oktoba 2019 wakiwa wanaadhimisha miaka 57 ya uhuru wa wa Uganda. Wizara ya mambo ya ndani ya Uganda iliweka picha ikionesha bendera yao ikionekana kwenye jengo hilo Lighting at the Burj Khalifa
F1AgQfSWIAAl3Fj
Mara ya pili bendera ya Uganda iliwekwa kwenye jengo la Burj Khalifa tarehe 3, Oktoba 2021. Bendera ya Uganda iliwekwa wakati Dudai ikiadhimisha maonesho ya Dubai,(Dubai Expo 2021 ambayo yalikuwa yafanyike 2020 yakaahirishwa kutokana na COVID 19)
93d9de60-b573-4462-9e41-1f9992b44744.jpg

Tanzania
Mwaka 2022 Februari 28 jengo la Burj Khalifa liliitangaza bendera ya Tanzania kwa dakika 3 , iliyokuwa imewekwa na picha ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hii ni baada ya ziara ya siku 3 ya Rais Samia iliyoanza Februari 24, 2022 huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushiriki maonyesho ya Expo 2020 na kumalizika 28, Februari 2022 ambapo alirejea nchini Tanzania.

FM02cfoXMAI9nVX.jpg:large
Msemaji Mkuu wa Serikali alipost kwenye ukurasa wake rasmi akionesha picha ya jengo la Burj Khalifa likiwa limepambwa kwa bendera ya Tanzania. Tanzania, Burj Khalifa - Dubai
burji-jpg.2134743

Hivyo basi, JamiiForums imethibitisha Tanzania ndiyo nchi ya mwisho kwa nchi za Afrika Mashariki kuwekwa kwenye jengo la Burj Khalifa ambapo iliwekwa tarehe 28, 02,2022, hakuna nchi yoyote ya jirani ambayo bendera yake iliwekwa tena baada yake.

Hivyo taarifa za kuwekwa kwa bendera za majirani baada ya Tanzania hazina ukweli.
Kwahiyo Mhe. Rais kadanganywa na wasaidizi wake nayeye bila fact check kaja kwenye media kulisema tena kutunanga kwamba tunaleta malumbano kuhusu uwekezaji.

Mhe. Rais hajaona hoja za wanaohoji ila kaona malumbano tu?

Mungu atupe uhai kila jambo litakuwa wazi baada ya miaka kadhaa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom