Bazoka

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Jul 20, 2008
777
49
Waheshimiwa naomba kupatiwa jina halisi la kiswahili la bazoka au big G. Maana haya yote ni majina yaliyotolewa na makampuni yanayotengeneza bidhaa hii.
 
Kwa Arusha naona jina bazoka ndio maarufu zaidi, aidha wengi utumia Big G kwa aina zote za chew gum mkoani hapo... Kama linatumika basi ni kwa sehemu chache sana mjini humo..

Ama kwa Singida sijapata kabisa kusikia matumizi ya ubani wa kutafuna, labda katika miaka hii, kwani nilipita huko kitambo kidogo.
 
Ubani wa kutafuna

Nadhani maneno 'Bazoka' , 'Bigijii' na 'Chingamu' (chewing gum!) yamepata mashiko zaidi baina ya wazungumzaji wa kiswahili wa sasa kuliko neno 'ubani wa kutafuna'.

Ni kweli ni maneno ya kukopa/kutohoa - tena ni mali za makampuni (trade marks/names) - lakini, lugha ndivyo ilivyo. Wanajamii wakikubalina neno basi linakuwa sehemeu ya lugha yao.Hakuna ubaya katika hilo! Kuna maneno mengine mengi tu ya jinsi hii ambayo nayo yamepata mashiko japokuwa ni trademarks/names: bukta (Bukta),themosi (Thermos), katapila (Caterpillar), sheli (Shell) nk
 
Back
Top Bottom