BAVICHA kuitisha maandamano ya kitaifa kumg'oa Dr. Slaa!

Status
Not open for further replies.
Mkuu hapo ndipo penye shida. Kila siku utasikia huyu kanunuliwa ama yule kanunuliwa. Imefika hatua hata viongozi wa juu wa BAVICHA tunaambiwa wamenunuliwa.Hivi ni rahisi hivyo kuwanunua viongozi ama wanachama?

Hao siyo kama wamenunuliwa bali ni unnder cover agents wameamua kujilipua na kujionyesha rangi zao halisi.
 
huna sera wewe wakati wewe hapo ulipo unawaza utakula lini badala ya kusema watanzania wajitambue na kuondoa dhana ya umimi, CCM NI CHAMA AMBACHO KINA SERA ZAKE NA ITAKADI ZAKE HATA CDM WANA SERA ZAKE CHA MUHIMU NI MM NA WEW KUKUBALI KUFUATA SHERIA ZILIZOPO
 
Nakushukuru sana kwa kubainisha ukweli huo ndicho nilikuwa nataka useme ili watu hapa wajue wana kimeo wanachoshughulika nacho.



Endelea kwani kazi unayoifanya ina faida hata kama wewe mwenyewe si riziki.
nashukuru naendela na kuelimisha jamii tasa kama yako wewe
 
Mkuu hapo ndipo penye shida. Kila siku utasikia huyu kanunuliwa ama yule kanunuliwa. Imefika hatua hata viongozi wa juu wa BAVICHA tunaambiwa wamenunuliwa.Hivi ni rahisi hivyo kuwanunua viongozi ama wanachama?

Usishangae mkuu,watu wenye uwezo mdogo wa kutafakari mambo na ambao hawajui kusoma alama za nyakati hukimbilia kuwaambia watu wenye tafakuri kwamba wamenunuliwa.munalazimisha slaa kumiliki kadi ya nyinyiemu ionekane si tatizo kweli hizo ni akili za kimapinduzi au ukosefu wa akili.binafsi natofautiana na slaa na wote wanaomuunga mkono ktk hili.
 
Najaribu kuconnect dot na hoja ya zitto alipowaita wazee 'VIBABU' napata jawabu kuwa yupo nyuma ya hili.sijui unawezaje usimhusishe zitto ktk hili. Kwanini wasiangalie matendo yake? Mbona zitto ana kadi moja ya CDM lakini anapendwa na CCM (adui) lakini dr. Slaa ana pamoja na kuwa na kadi ya CCM lakini hawalali kwa ajili yake?

mbona na nyinyi babu and his company zitto anawanyima sana usingizi?
Hamuishi kumtaja taja kashawaambia hahusiki na huo ndo ukweli wenyewe.
Zitto yuko busy na report ya mabilioni ya uswiss na maandalizi yakuingia ikulu maana ndie rais wa moyoni mwetu.
 
Mnadanganya watu wazima nyie, mnapoteza muda. Slaa ni jembe na ataendelea kuwa jembe. Kuwa na kadi ya CCM si hoja kabisa, kwani mlitaka arudishe kadi CCM, hiyo imebaki kuwa kumbukubu yake. Matendo ya Slaa hayaoneshi kuwa ni mamruki, Lyatonga Mrema na Mbatia hao ni sawa maana hata vitendo vyao vinaonesha
 
Huyu kijana(magafu)alikuwa mwendesha madampa ya mgodi wa GGM na amefukuzwa miezi 3 iliyopita kwa wizi wa mafuta..chadema kuweni makini mnapowapa majukumu makubwa vijana wenye njaa kama hawa
 
CCM na serikali yake wanatumia gharama kubwa na mbinu za kila aina kudhoofisha upinzani ila wananchi tumechoka na haudanganyiki tena. Ni bora hizo gharama wangezielekeza katika shughuli za maendeleo ya jamii ili hata baada ya kutoka madarakani wawe na la kuonyesha. Mabadiliko ni lazima, watake wasitake.
 
Inatia aibu kama vijana wa Chadema mnaweza kununulika kirahisi kiasi hicho.

Mtu yeyote ambaye hajui anachokijua au anachokisema ni rahisi kununuliwa maana anadanganyika hata pale ambapo hapaswi kufanya hivyo. Kwanza niulize Dr Slaa ameipata hiyo kadi lini: kabla ya kuwa mwanachadema au baada? Na je, kuwa na kadi ndiyo kuwa mwanachama au kuwa mwanachama ni fufanya shughuli za chama? Kanuni za CCM zinasema nini kuhusu uanachama? Hawa vijana hamnazo kabisa! Badala ya kujadili mambo ya msingi wanaongea punda - halafu inaonekana kama waliofukuzwa Chadema ndio hao wenye hilo kundi la Salvatory Magafu.
 
vijana wanaojiita chadema na kuimba nyimbo zoooote za ccm na kubeba vibwagizo vya nape nnauye, wanafanya press conference jijini mwanza muda huu kutukana harakati za mabadiliko nchini. Wanapambana kuzuia upepo. Mtawasikia kesho kwenye majira, jambo leo, habari leo na mtanzania.

Yupo eddo mwamalala, adams chagulani na wengine. Kuna mtumishi mmoja wa serikali, ofcourse ana asili ya ugamba, ndiye anayetoa mshiko kwa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mbeya zilizoandikwa na vyombo vya habari juzi na leo, huyo eddo kwanza si mjumbe wa mkutano mkuuu kama alivyowa fix waandishi wetu hapa mjini, hata wakashindwa kumuuliza maswali ya msingi kama vile kwa nini hakufanyia press conference yake mbeya, pili alishafukuzwa uanachama na taarifa kupelekwa makao makuu.

Ndiye aliyeshirikiana na watu wa uwt kushusha bendera za chadema usiku wa manane kule mbozi, wakati wa ziara ya makamu wa rais, bilal. Bahati nzuri, lile tukio lili backfire, wakalazimika kuzirudisha mchana kweupe wakati walishusha usiku. Ilikuwa ni baada ya wananchi wa mbozi kuchachamaa. Majuzi pia alibambwa akigawa vifaa vya uenezi vya chama cha ndc.

Wakati vijana makini wanatumia nguvu na akili zao kueneza chama, kuna vijana 'kumi' wapumbavu wanafanya kazi ya kuvuruga harakati. Jambo ambalo ni sawa na kucheza na utelezi wa kwenye jiwe la kisimani 'lugoga'.

Topic yao kubwa waliyoagizwa na lumumba ambao ndiyo waliwaandalia press ya dar es salaam, ni kuhusu suala la kipuuzi la kadi ya ccm.

Vijana hawa hawajui kuwa mapambano haya ni mpango wa mwenyezi mungu, si suala la bahati mbaya. Watakuwa na maisha mabaya sana kwa matokeo ya kasi hii ya kumsaidia ibilisi wanayoifanya.

mfukuzeni na huyo tena
 
katika hili babu hachomoki.kakalia kuti kavu.

Of course, kwa watu ambao ni hamnazo sioni ajabu maana what they are doing is their best - they cannot do better than that. Kwa hiyo, kuwategemea kuonesha akili haiwezekani! Na kama watamwondo Dr Slaa kwa mambo ya kijinga hivyo, chama kitakufa maana sababu hizo hizo zitaendelea kuelekezwa kwa viongozi wengine hadi chama kusambaratika zaidi.
 
Muumini safi Hivi kwa nini huwezi kutoa hoja kwa kufikiri? Kuhama chama siyo usaliti. Kuacha upadri siyo usaliti. Ndoa kuvunjika siyo usaliti. Kinyume chake ndiyo usaliti - mfano, kubaki ndani ya chama usichokiamini ni usaliti; kuishi ndoa ambayo kimsingi haipo na haikupi fulfilment ni usaliti; kubaki padri usiyendana na kanuni zake ni usaliti. Alichokifanya Dr Slaa ni kufanya uamzi wa uhuru bila ya kumwogopa mtu.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom