basi wewe ni mtanzania....

stevoh

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
2,921
1,104
Ukiwa kama mtoto wa kitanzania kati
ya haya hujawahi kufanya hata moja?
1. Je hujawahi kujisuguli chupi ukiwa
unaoga badala ya brash?
2. Hujawahi kucheza kibaba au
kimama? 3. Hujawahi kusingizia unaumwa ili
usiende shule?
4. Hujawahi kulilia nguo za sikukuu
wewe?
5. Hujawah kugoma kuoga?
6. Hujawahi kulilia soda ya mgeni? 7. Hujawah jifutia kamasi shati la shule
wakati upo primary?
NAJUA KATI YA HAYA KUNA ZAIDI YA 1
AMBAYO UMEWAHI FANYA. Basi ondoa
shaka wewe ni mtanzania halisi...
 
Wewe, hiyo ya kwanza mbona mimi nafanya kila siku. Chupi niliyovaa ndo brash yangu. Naipiga Mshindi kwanza then naisukumia detol ili initakatishe poa, then naisuza na kuianika tayari kusubilia round nyingine
 
Wewe, hiyo ya kwanza mbona mimi nafanya kila siku. Chupi niliyovaa ndo brash yangu. Naipiga Mshindi kwanza then naisukumia detol ili initakatishe poa, then naisuza na kuianika tayari kusubilia round nyingine

Amaizing
 
kama hujawahi kudondoka kwenye mti....wewe ni msomali.....
 
kupita njia ya kipori tukiwa primary ili tuokote mabibo, furu, ukwaju na mabungo! lol, mashati ya shule yalikuwa yanakoma, tulikuwa tunadundwaje sasa na mama?? nawasalimu wote mliosoma mlimani primary enzi za mndolwa! naimisigi sana ile shule!
 
Hujawahi kutoka na mfupa wa paja la kuku na punje za ubwabwa hadi nje kwa wenzako na kuanza kuwaringishia?
Doridori dori samwela!!
Si Mtz wewe.
 
Hahahahaa nilivokua darasa la kwanza na la pili nilikua sipendi shule hivyo nilikua najisingizia ugonjwa kila wiki..darasa la tatu ndo nilianza kupenda shule baada ya kuona mwalimu akifundisha naelewa..
 
Back
Top Bottom