Basi jipya la Simba halina hadhi

Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,768
2,750
Mimi ni shabiki simba damu na nimekuwa mmoja kati ya watu wanaopigania simba ipate basi jipya lenye hadhi ya simba kwa muda mrefu. Nimefika mbali mpaka kutoa ushauri kwa mo apunguze bonus za mamia ya mamilioni anayotoa kwa mechi moja ili zielekezwe kununua basi lenye kiwango kama timu kubwa za afrika na ulaya (post zimo humu J).

Basi jipya lilivyofika nilifurahi kuona maoni yetu yanafanyiwa kazi na kuwa basi hili aina ya tata ni kiwango cha mbele hii ni sababu siku ile niliona video zake youtube nje na ndani ikiwa kuna siti za 1 by 2, space kubwa, hapo hapo kuna meza, tv kila siti, choo, fridge, jiko kama ndege first class angalia kuanzia dk 3:41

Kumbe zilikuwa picha za kuchonga na hili lijamaa linaongea limeshuhudia kwa macho kwakweli serikali iendelee kudhibiti huu uhuru wa habari, unatumika vibaya na wajinga kama huyu.

Leo nimeangalia video halisi ya basi, angalia hapo chini. Ni basi la hovyo hata likipaki stendi ya Kongwa abiria wanalinyanyapaa hawapandi ..bora yutong lirudi, hivi kweli achilia mbali scania tumeshindwa hata kununua zhongtong double difu au hata shabiby luxury za 1 by 2 na kuleta hili takataka? Nimesikitika sana kwa hadaa hizi za mo

Ww shabiki hupandi inakuuma nini? Je umesikia malalamiko toka kwa wachezaji wanaopanda? Kama angelalamika mchezaji tungeamini halifai
 
Umetumwa na FCC nini, nyie ndio mnaokwamisha mpira wetu, tutaendelea kuitwa kichwa cha mwendawazimu kila uchwao!! Hii nchi haiji kusonga mbele katika mpira, siasa ndiyo mpira wetu , umbeya wa mitandaoni ndiyo mpira wetu, hatuji songa maisha
 
Mkuu inaonyesha umeumia san next time wakiwa na mpango wa kununua watakutaarifu uwe consultant wao wa ununuz wa magar yenye viwango
 
Mimi ni shabiki simba damu na nimekuwa mmoja kati ya watu wanaopigania simba ipate basi jipya lenye hadhi ya simba kwa muda mrefu. Nimefika mbali mpaka kutoa ushauri kwa mo apunguze bonus za mamia ya mamilioni anayotoa kwa mechi moja ili zielekezwe kununua basi lenye kiwango kama timu kubwa za afrika na ulaya (post zimo humu J).

Basi jipya lilivyofika nilifurahi kuona maoni yetu yanafanyiwa kazi na kuwa basi hili aina ya tata ni kiwango cha mbele hii ni sababu siku ile niliona video zake youtube nje na ndani ikiwa kuna siti za 1 by 2, space kubwa, hapo hapo kuna meza, tv kila siti, choo, fridge, jiko kama ndege first class angalia kuanzia dk 3:41

Kumbe zilikuwa picha za kuchonga na hili lijamaa linaongea limeshuhudia kwa macho kwakweli serikali iendelee kudhibiti huu uhuru wa habari, unatumika vibaya na wajinga kama huyu.

Leo nimeangalia video halisi ya basi, angalia hapo chini. Ni basi la hovyo hata likipaki stendi ya Kongwa abiria wanalinyanyapaa hawapandi ..bora yutong lirudi, hivi kweli achilia mbali scania tumeshindwa hata kununua zhongtong double difu au hata shabiby luxury za 1 by 2 na kuleta hili takataka? Nimesikitika sana kwa hadaa hizi za mo

Inawezekana yeye ni mwakilishi wa tata, na limetoka kwa ajili ya matangazo ya biashara, ili wewe na Mimi kama wawekezaji ktk biashara ya usafirishaji tukanunue kama basi la Simba
 
Mkuu, hii ni moja ya post niliyoweka baada ya basi jipya kuja

Niwatoe hofu tata wana gari za kila kiwango kulingana na bajeti yako.

Turudi kwenye biashara katika sports industry: Simba ni brand kubwa sana tz na nje kwasasa, tata wanabranch nyingi tz mpaka mikoani.

Nategemea kuwa simba wameingia mkataba na tata ili kuitangaza tata, na hilo basi simba wamepewa ili watangaze aina hiyo ya mabasi nchini. Kwahiyo simba amepewa fedha na basi. Nikisikia basi limenunuliwa basi nitaendelea kuamini kuna watu wananufaika nyuma ya pazia.

Mfano Manchester United ilipoingia mkataba na audi kila mchezaji alipewa gari aina ya audi na fedha kwa timu.
 
Basi jipya la simba halina hazi
IMG_20210319_140530.jpg
 
Back
Top Bottom