Bashungwa Amsimamisha Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Eng. Andrea Kasamwa kwa kushindwa kusimamia urejeshwaji wa miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi na kupelekea barabara kuu zinanounganisha wilaya hiyo na maeneo mengine kufungwa.

Waziri Bashungwa akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi ameshuhudia urejeshwaji wa barabara ya Liwale - Nangurukuru iliyosombwa na maji ikisimamiwa na Mtaalam mwenye taaluma ya Falsafa kwa kusaidiwa na Wananchi wakati Mkandarasi akiwa hayupo eneo la Kazi.

Bashungwa amechukua hatua hiyo leo tarehe 06 Machi 2024 wakati akikagua mindombinu ya barabara katika Wilaya ya Liwale na kutoridhishwa na usimamizi wa kazi inayofanywa na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Lindi.

“Haiwezekani sisi tutoke Dodoma hadi huku Liwale kutokana na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara iliyopo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amelazimika kutoa Helikopta yake tufike huku, lakini hapa site hakuna Mkandarasi, mnaweka mtu aliyesoma falsafa kusimamia kazi ya ujenzi wa barabara”, ameeleza Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Mohamed Besta, kuleta Wataalam na kuhakikisha ndani ya siku nne barabara zote kuu na madaraja yanayounganisha Wilaya ya Liwale na maeneo mengine katika mkoa huo ambayo hayapitiki yawe yamefunguliwa na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Kadhalika, Waziri Bashungwa amesema Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha ya kumtafuta Mkandarasi wa kujenga barabara ya Masasi - Nachingwea - Liwale km 175 kwa kiwango cha lami ili kumaliza changamoto inayoendelea kujitokeza ya kufungwa kwa barabara.

Bashungwa ameeleza kuwa Serikali itaanza kujenga kwa awamu barabara ya Nangurukuru - Liwale yenye urefu wa kilometa 230 kwa kiwango cha lami ambapo amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi kutenga fedha na kumtafuta Mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi kipande cha kilometa 10 kwa kiwango cha lami.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack amesema ataendelea kufuatilia kwa ukaribu kazi zote ikiwemo urejeshwaji wa miundombinu katika Mkoa huo hasa Wilaya ya Liwale, Nachingwea na Ruangwa na hatasita kumchukulia hatua Mkandarasi na Mtaalam yoyote anayeshindwa kutekeleza majukumu yake ilasavyo

Naye, Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka ameishukuru Serikali kwa kuanza kuchukua hatua za kurejesha mawasiliano ya barabara kutokana na changamoto kubwa ya barabara na madaraja yanayounganisha wilaya ya Liwale na maeneo mengine kujaa maji na kupelekea kufungwa hadi sasa.

WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.21.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.23.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.27.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.29.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.31.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.33.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.34.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.25.36.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-06 at 14.26.05.jpeg
 
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, mhandisi Andrea Kasamwa kwa kushindwa kusimamia urejeshwaji wa miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Liwale mkoani hapa na kusababisha barabara kuu zinanounganisha wilaya hiyo na maeneo mengine kufungwa.

Waziri Bashungwa akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi ameshuhudia urejeshwaji wa Barabara ya Liwale - Nangurukuru iliyosombwa na maji ikisimamiwa na mtaalam mwenye taaluma ya falsafa kwa kusaidiwa na wananchi wakati mkandarasi akiwa hayupo eneo la Kazi.

Bashungwa amechukua hatua hiyo leo wakati akikagua mindombinu ya barabara katika Wilaya ya Liwale na kutoridhishwa na usimamizi wa kazi inayofanywa na TANROADS Mkoa wa Lindi.

“Haiwezekani sisi tutoke Dodoma hadi huku Liwale kutokana na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara iliyopo, Rais Samia Suluhu Hassan amelazimika kutoa helikopta yake tufike huku, lakini hapa site hakuna mkandarasi, mnaweka mtu aliyesoma falsafa kusimamia kazi ya ujenzi wa barabara”, alisema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS mhandisi Mohamed Besta, kuleta wataalam na kuhakikisha ndani ya siku nne barabara zote kuu na madaraja yanayounganisha Wilaya ya Liwale na maeneo mengine katika mkoa huo ambayo hayapitiki yawe yamefunguliwa na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
 
Does it mean kuwa huyo engineer alikuwa na resources zote za kufanya hicho anachokilalamikia bashungwa akakaa nyumbani /ofisini bila ku/umia resources hizo kuondoa tatizo? IMPOSSIBLE!
 
Siku nne aisee nyie zaidi ya Japan
kwenye tetemeko barabara ilivunjika ikajengwa kwa siku 6
 
Hiyo barabara ya Masasi - liwale mwaka wa tatu sasa bungeni inasemwa hela ishatoka ila haijengwi mpaka leo why? Wilayani Liwale bidhaa mhimu kama unga, petrol, cemend nk. Zimeisha na wananchi hawajui lini zitarejea wapo ka yatima
 
Siku nne aisee nyie zaidi ya Japan
kwenye tetemeko barabara ilivunjika ikajengwa kwa siku 6
Tunamshukuru waziri, angalau kwa kufika kwake sasa barabara ya Nangurukuru - Liwale inapitika maana hali ilikuwa mbaya, kwenda dsm ilikuwa lazima uvuke mto kwa kuogelea kisha ng'ambo ndo upande gari ya dsm huku ukiwa umeloa chapa chapa
 
Tunamshukuru waziri, angalau kwa kufika kwake sasa barabara ya Nangurukuru - Liwale inapitika maana hali ilikuwa mbaya, kwenda dsm ilikuwa lazima uvuke mto kwa kuogelea kisha ng'ambo ndo upande gari ya dsm huku ukiwa umeloa chapa chapa
Aisee, poleni sana kwa yote
 
Hahaaaaa tumeahidiwa lami na mh. Waziri, mama katoa kibunda iwekwe lami, Tunashukuru kama haitakuwa siasa basi tutakuwa tumefika mwisho wa mateso ya masika
Lakini ni haki yenu, hawa wanasiasa wanajiona kama wanatoa mifukoni mwao
Eti mpaka waombwe
Lakini kwa kuwa uchaguzi umekaribia wataweka 😄
 
Back
Top Bottom