Bashe, Shigela washukiwa; UVCCM wawarushia tuhuma nzito

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
*Kijana UVCCM awarushia tuhuma nzito
*Awapa siku 21 watuhumiwa wang’oke

Na Mwandishi Wetu - Mtanzania
shigela.jpg
malisa.jpg

HusseinBashe.jpg



MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Agustino Matefu, ameibuka na kusema tayari ana majina manane ya wana CCM walio kwenye orodha ya kupewa barua za kujivua uongozi.

Matefu, ambaye aliwashambulia baadhi ya wanasiasa wakongwe ndani ya CCM, alitaja orodha hiyo alipozungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Hadees, jijini Dar es Salaam, jana.

Aliwataja wanachama walio kwenye orodha ya kuadhibiwa kuwa ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.


Wengine ni Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa Beno Malisa; Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Martin Shigela; Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isack; na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Hussein Bashe.


Kijana huyo alisema amechukua uamuzi wa kuzungumza suala hilo kama mchango wake kwenye mtafaruku na mgongano wa mawazo ya kimageuzi unaoendelea ndani ya CCM.


Ingawa hakusema kama alichokizungumza ni cha UVCCM Mkoa au ni mawazo yake binafsi, alisema wao kama vijana wanaunga mkono mabadiliko yanayoendelea ndani ya CCM.


Alisema wanapinga siku 90 walizopewa watuhumiwa wa ufisadi kwa maelezo kwamba ni nyingi mno. Badala yake, alisema UVCCM wanawapa watuhumiwa hao siku 21 wawe wameachia nafasi walizonazo, vinginevyo umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam utachukua hatua kali.


“Haiwezekani wakapewa siku 90 kama wapangaji, tunawapa siku 21, kwani hawa ni wezi wa rasilimali zetu kwa kuwa tumechoka kudanganywa na vi-mia mbili vyao, na muda huo ukifika wakiwa hawajaachia nafasi hizo jiji hili litakuwa halitoshi, kwani hatuna ugomvi na mtu zaidi ya kutetea maslahi ya chama chetu,” alitamba Matefu.


Alisema kuwa ndani ya UVCM kuna mafisadi 100 wanaofadhiliwa na watuhumiwa wakuu wa ufisadi.

Aidha, alisema kuwa kutokana na UVCCM kushindwa kumshauri vizuri aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, hata kufikia chama kupoteza mwelekeo, ni busara sasa wakajipima na kukaa pembeni ili wengine waongoze.


Aliongeza kuwa makada wa chama hicho wanatambuliwa kwa uongo, unafiki na kujipendekeza kulikojaa uchu wa madaraka, huku wakikumbatiwa na mmoja wa wanasiasa wakongwe ndani ya CCM.
 
Kama mkuu wa nchi anafahamu ni mafisadi pasipo shaka, kwa nini hawashitakiwi na serikali anayoiongoza? na badala yake wanataka tu kuwaondoa kwenye chama? K wa wenye akili tunafahamu huu ni usanii na mind games tu kuwahadaa wananchi. Wfunguliwe kesi mahakamani maana inaonekana hata mkuu wa nchi anao ushahidi kuwa ni mafisadi.
 
ulikuwa wapi muda wote matefu? umetokea wapi? matefu, we ni nani?
 
Augustine Matefu anatetea MASLAHI YA CHAMA CHAKE CHA CCM na si maslahi ya taifa.
Binafsi namwona anatafuta mpenyo wa kumaliza chuki binafsi na baadhi ya makada wake.
 
Mungu atakusaidia ulicho dhurumiwa kitarudi ''What goes around comes around"waambie karibuni uswazi,tena kibongobongo ukishatoka tu kwenye channel [Mfumo] waliokuzunguka wote wanakutosa uwezi amini,hapo ndipo uwanakubali wabongo.
 
Kama mkuu wa nchi anafahamu ni mafisadi pasipo shaka, kwa nini hawashitakiwi na serikali anayoiongoza? na badala yake wanataka tu kuwaondoa kwenye chama? K wa wenye akili tunafahamu huu ni usanii na mind games tu kuwahadaa wananchi. Wfunguliwe kesi mahakamani maana inaonekana hata mkuu wa nchi anao ushahidi kuwa ni mafisadi.

Miye nasubiri kwa hamu sana nione itakuwaje watakapopewa hizo barua akina RA, EL na AC. Kimsingi, mkuu wa nchi na serikali yake walipaswa wawachunguze hao watu na kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi. Lakini watakapotoka kwenye chama (kama ni kweli) sinema itakuwa imeishia hapo.
 
hivi hiki chana kina uongozi kweli hiki?mbona ni kama club ya pombe kina mtu anaongea tu..Hivi wewe JK haya yote unayajua au ndo uko bize unakula kahawa na visheti msoga kwa maza...
 
Safi sana kijana, baada ya kuwashughulikia hawa kisheria, Umoja wa Wanawake na ule wa Wazazi ujiandae. Bila shaka operation vua magamba haitaacha kitu, kila jiwe ligeuzwe.
 
Safi sana kijana, baada ya kuwashughulikia hawa kisheria, Umoja wa Wanawake na ule wa Wazazi ujiandae. Bila shaka operation vua magamba haitaacha kitu, kila jiwe ligeuzwe.
Akina mama mvueni gamba Sophia Simba,naye ni kati ya wapiga filimbi maarufu wa mafisadi si ajabu naye ni fisadi ,kwani ukiwa na rafiki mvuta bangi nawe unakuwa mvuta bangi
 
ahahah!! wanatafunana!! alikuwa wapi huyu jamaa tangu zama?? Hakuna cha magamba hapa, bali kambi moja inashinda dhiidi ya nyingine. Kama ni uchafu wote ni wachafu, hakuna msafi, nionavyo mimi.,
 
Kwa hiyo anatuambia kwamba siku zote walikuwa wanadanganywa na vi-mia mbili? P***fu!
Huyo muungwana kakiri mambo ya rushwa hadharani, pccb wako wapi kuchunguza maana hizi ni tuhuma nzito instead anapewa front page headlines Tanzania kiboko.
 
Huyo muungwana kakiri mambo ya rushwa hadharani, pccb wako wapi kuchunguza maana hizi ni tuhuma nzito instead anapewa front page headlines Tanzania kiboko.

hivi PCCB ipo bado? na wafanyakazi wake wanalipwa mishahara? kutakuwa na makosa gani kuifuta/kuiondoa hii taasisi?
 
Hivi huyu Benno Malisa si ndo swahiba namba moja wa Irizimoja jamani kama mtoto wa muheshimiwa ana hasili ya ufwiswadi lazima na yeye yumo ktk mlolongo maana anaonekana kujipendekeza kwa huyu mtoto wa komredi sana, haaaaya weeee
 
Back
Top Bottom