Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,032
- 2,769
Mradi huu ni maono ya waziri Hussein Bashe, unaongozwa kwa mahesabu makali sana, tulijua kundi la kwanza litakaa field miezi miwili au mitatu kisha wagawiwe mashamba yao kama walivyokuwa wameahidiwa ili waende wakayasimamie wenyewe lakini mpaka sasa wamewashikilia na kuwaweka pamoja huu ni mwaka sasa unakaribia kuisha hakuna vijana wengine waliochukuliwa zaidi ya walewale.
Mambo yamekuwa mengi sasa wamekuja na mpya kwamba hawa vijana lazima wapitie JKT, du Bashe bwana, huko shambani kuna vita? Nilijua watawezeshwa kwa kupewa mikopo ya matrekta ili kila aende akafanye uzalishaji kwenye maeneo yao na kwenda kufundisha wengine.
Nilijua watakopeshwa mitaji ya kuwawezesha kununua vitendea kazi vitavyowafanya kulima kwa ubora zaidi naona sasa wapo JKT, mara mashamba darasa, nk. Ni lini watapewa mikopo waende wanaendesha kilimo mlichowafunza kila mtu kwa kujisimamia mwenyewe? Mtawaatamia mpaka lini?
Mtawagawia lini mashamba yao na kuwaacha huru walime kwa manufaa yao? Kila darasa lina mwisho vipi hii basheagriculture haina uhitimu ili waanze wengine? Haya sawa