Basena out Simba SC

Kama hii habari ni ya kweli huu utakuwa upuuzi mkubwa ila nimemsikia Rage asubuhi katika PB ya Clouds akisema matokeo yoyote kati ya Simba Vs Yanga sio kipimo cha ubora wa mpira wetu.
 
Klabu ya simba leo imemfuta kibarua kocha wao Moses Basena baada ya kufungwa na Yanga bao 1 - 0 katika mchezo wa ligi kuu.
Aidha pia Emanuel Okwi na Godfrey Kaburu wamesimamishwa na uongozi huo kwa mda usiojulikana
Tarifa nilizonazo ni kuwa kamati ya utendaji wa Simba inakutana Ijumaa kujadili, pamoja na masuala mengine, mechi yao na yanga. sasa huo uongozi uliomfungia Basena ni uongozi gani? Au kwa kuwa ameondoka kwenda kwao ndo inahesabika kuwa kafukuzwa?
 
hahahahaha...ila nachojua mm kuwa Kocha Basena..kaenda kwao anadai mama yake mgonjwa(..inawezekana kisingizio)....ila kaburu na Okwi wamekwa kiporo...subiri tucheze mechi kesho ..mtapata jibu kamili
 
hahahahaha...ila nachojua mm kuwa Kocha Basena..kaenda kwao anadai mama yake mgonjwa(..inawezekana kisingizio)....ila kaburu na Okwi wamekwa kiporo...subiri tucheze mechi kesho ..mtapata jibu kamili
Tunasubiri....
 
Kwa hali hii mpira wa kibongo hauta kaa ubadilike na kuwa mafanikio,ni mpira wa majungu na ni mpira wa kufikirika.hakuna mafanikio yoyote katika kila jambo kama halitaoanishwa na mipango ya kimaendeleo na kisha kuwa na dhamira ya kweli ya kuitekeleza mipango hiyo.
siku zote watanzania kwenye soka tunawaza ni jambo la kufundishwa leo na kesho upate ushindi.haya mambo ndo yalipelekea kutokuendelea na Maximo kocha ambae alishaamsha ari ya soka kwa wachezaji na washabiki wa soka.lakini kwa sababu ya kufikirika tukaona hatufai.leo Besena kaharibu nini?au kama kipimo cha kujua soka ni kumfunga yanga tu?
Mambo ya kiswahili siku zote silaha yake ni majungu na matokeo ya majungu huwa ni kutokufanikiwa siku zote.nashukuru timu yangu ilishashuka daraja na nimeridhika kabisa,si nyingine ni PAMBA ya mwanza.
 
Upuuzi mtupu? Kwahiyo kipimo cha ubora wa kocha ni kufungwa au kufunga Yanga?
Hiyo ndo soka ya kibongo: ni kudesa kila kitu;
Yanga walimsajiri Timbe kutoka Uganda na Simba nao wakamtafuta Basena kutoka Uganda:
Yanga walimtimua Timbe 2011 na Simba nao wanamtimua Basena 2011
'''''Sizani kama tutafika'''''
 
klabu ya simba leo imemfuta kibarua kocha wao moses basena baada ya kufungwa na yanga bao 1 - 0 katika mchezo wa ligi kuu.
Aidha pia emanuel okwi na godfrey kaburu wamesimamishwa na uongozi huo kwa mda usiojulikana

mwenyekiti wa simba sc. Ni
mpuuzii na hovyo kabisa
 
Basena amejiharibia mwenyewe. Alipanga timu mbovu na fomesheni mbovu. Iwapo angepanga timu vizuri Yeboyebo wangelala mapema sana. Huyo Okwi nasikia ni rafiki sana wa Ridhiwani na amekuwa akimpa pesa nyingi ili anapocheza na Yanga asifunge magoli. Mwenye taarifa zaidi kuhusu huyu dogo atumwagie.

Hapo kwenye red;

1. Kachukue team wewe.
2. Unataka kumchagulia Okwi marafiki?
3. Una ushahidi kuhusu hizo pesa alizopewa?
 
Kwa hali hii mpira wa kibongo hauta kaa ubadilike na kuwa mafanikio,ni mpira wa majungu na ni mpira wa kufikirika.hakuna mafanikio yoyote katika kila jambo kama halitaoanishwa na mipango ya kimaendeleo na kisha kuwa na dhamira ya kweli ya kuitekeleza mipango hiyo.
siku zote watanzania kwenye soka tunawaza ni jambo la kufundishwa leo na kesho upate ushindi.haya mambo ndo yalipelekea kutokuendelea na Maximo kocha ambae alishaamsha ari ya soka kwa wachezaji na washabiki wa soka.lakini kwa sababu ya kufikirika tukaona hatufai.leo Besena kaharibu nini?au kama kipimo cha kujua soka ni kumfunga yanga tu?
Mambo ya kiswahili siku zote silaha yake ni majungu na matokeo ya majungu huwa ni kutokufanikiwa siku zote.nashukuru timu yangu ilishashuka daraja na nimeridhika kabisa,si nyingine ni PAMBA ya mwanza.

inategemea na malengo na perspective yako, angalia klabu kama chelsea au real madrid wao kocha akiboronga huwa wanafanya nini?au wao nao wamejaa majungu na umbea je na wao ni waswahili?

je, unajua basena wakati anaajiriwa alipewa mkataba wa muda gani?uliza ndio ujibiwe

sisi wapenzi wa simba tunaohudhuria mechi tunaiona timu yetu, timu hii ni nzuri sana katika miaka 3 au 4 iliyopita kwani kila eneo lina wachezaji wazuri, kipa ni mzuri, mabeki, viungo ndio usiseme na washambuliaji hali kadhalika, lakini ijapo kuwa timu ilikuwa inashinda timu haina coordination, ni sawa na man city enzi ya mark hughes au hata sasa kwa mancini, timu ni nzuri lakini kocha wa man city sio bora enough kwa ile timu, hilo ndilo lililopo Simba, kwani timu hii kwa ukamilifu wa wachezaji na angekuwa ni phiri, timu hii isingekuwa inashinda bao 1-0, maana ni kweli simba inaongoza ligi lakini ni juhudi zaidi za wachezaji kkwani wao hawachezi kitimu, sasa mwenye jukumu la kuunganisha timu ni nani kama sio kocha?

basena kwanza naamini hata viongozi wa simba wenyewe wanajua walilamba galasa, hana uzoefu wa kufundisha klabu kubwa huko kwao,yeye alikuwa kocha msaidizi uganda atafundishaje Simba klabu kubwa kuliko yoyote iliyopo kwao Uganda?mimi japokuwa siungi mkono maamuzi ya yeye kutimuliwa sasa lakini nafahamu kabisa Simba hatuna kocha, yule ni mchemfu, kwanza sisi tuna kawaida ya kujaza viungo wengi na kucheza pasi zaidi yeye juzi kapunguza viungo kwa kuwafanya waende winga na kuacha nafasi kati yanga wajitutumue, na ukitaka kujua kakariri hata sub zake kikianza kipindi cha pili tu, ndio anamwingiza haruna moshi kwenye mechi zote karibuni anafanya hivyo, ile na african lyon, ruvu na hii na yanga, sasa hapa ina maana ni wakati wa half time tu ndo anaona boban aingie au wakati upi?

basena bado hana hadhi ya kufundisha simba , na akiendelea si ajabu hata ubingwa tukakosa
 
Mimi ndo maana sipendi mpira wa bongo naona ni ujinga mtupu. Timu zote kubwa uingereza zimefungwa magoli mengi wala sijasikia kocha kufukuzwa wala nn.wanajipanga na kusonga mbele.Torres alikosa goli la wazi walipocheza na man na hakuambiwa chochote iweje okwi kukosa goli.simba waache mambo ya kijinga.
 
Basena amejiharibia mwenyewe. Alipanga timu mbovu na fomesheni mbovu. Iwapo angepanga timu vizuri Yeboyebo wangelala mapema sana. Huyo Okwi nasikia ni rafiki sana wa Ridhiwani na amekuwa akimpa pesa nyingi ili anapocheza na Yanga asifunge magoli. Mwenye taarifa zaidi kuhusu huyu dogo atumwagie.

siku zote mfa maji haishi kutapatapa... Yaani we badogo unaota basena angepanga hivi ingekuwa hivi, angemweka fulani tusingefungwa... angepanga kikosi hiki yanga wangelala mapema na blabla kibao poleni weee!! Hata hivyo mmeshachelewa limebaki neno 'ingekuwa hivi...'
 
mi nadhani hapo suala ni kufungwa na Yanga tu, koz mbona mechi zote ndio alivyokuwa akikipanga kikosi chake na kilikuwa kinashinda na wachezaji hao hao?
Simba wameamua kuwaiga Yanga kwa kumtimua maana Yanga walianza kuleta makocha wazungu Simba nao wakaleta, Yanga wakamuajiri Sam Timbe nao wakaenda Uganda kumuajiri Moses Basena..nahisi nao kwa sasa wataenda tafuta mzungu kamaYanga walivyomleta Papic
 
Basena hajafungiwakuwa mwelewa, kocha haitaji kamati ya utendaji ili afukuzwe kazi haya mwenyekiti peke yake ana uwezo wa kumfukuza, au mwenyekiti wa benchi la ufundi..
Basena kaftukuzwa kazi jana rasmi, hiyo ya mama yake mgonjwa ni danganya toto, kwa nini asingemalizia mechi ya leo na Moro United ndio akaenda kwa mama yake kumuuguza?
kwa nini aondoke yeye na kocha msaidizi wake?
Simba imempa ajira Selemani Matola kama kocha wa simba
 
Kamwaga alisema Basena ameenda Uganda kwasababu mama yake ni mgonjwa. Hata hivyo uongozi ulihitaji taarifa ya mchezo, je hiyo taarifa ilipelekwa na kujadiliwa? je maamuzi hayo yamezingatia taarifa iliyotolewa? Mimi siamini taarifa yako, inweza kuwa ni uzushi tu.
 
Basena hajafungiwakuwa mwelewa, kocha haitaji kamati ya utendaji ili afukuzwe kazi haya mwenyekiti peke yake ana uwezo wa kumfukuza, au mwenyekiti wa benchi la ufundi..
Basena kaftukuzwa kazi jana rasmi, hiyo ya mama yake mgonjwa ni danganya toto, kwa nini asingemalizia mechi ya leo na Moro United ndio akaenda kwa mama yake kumuuguza?
kwa nini aondoke yeye na kocha msaidizi wake?
Simba imempa ajira Selemani Matola kama kocha wa simba

ok tupe basi sababu walizotoa ili kuhalalisha kumfukuza Basena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom