Barua ya wazi kwenda kwa Askofu Kardinali Pengo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
pengo.jpg

Tumsifu yesu kristu! Baba Cardinal sisi waamini tunakuelewa sana unaposema tumuunge mkono Mh. Sana Rais wetu nasi tupo nyuma yako na tutatii.

Ila kuna kitu huenda watu hawakuelewi, Je! Ni kwamba udhalimu unaofanywa na serikali hii wewe baba huuoni? Na kama unauona umechukua hatua gani kumsaidia Mh. Rais ili atende kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu? Angalau baba Askofu Augustine Shao wa Zanzibar amegusia kuhusu madhila yatupatayo.

Kama hukumbuki yaliyotokea mwaka huu hata moja huligusii na umekuwa kipaumbele kumpinga anaeonyesha kukerwa mfano umempinga waziwazi Askofu Severine NiweMugizi alipotoa maoni yake ukasema hayo ni maoni yake na sio maoni ya kanisa sasa hayo uliyoyasema tuchukulie ni maoni yako au ya Kanisa? Kama ni ya kanisa umeyatoa kwenye kikao gani na ni nani amekutuma? Kama ni yako binafsi mbona umekuwa mwepesi kupinga wanaotoa maoni yao?

Alphonse Mawazo kauwawa na wanaohisiwa ni wanachama wa chama tawala, Ben Saanane amepotea mpaka leo haonekani, Tundu Lisu kashambuliwa mchana kweupe, ofisi za mawakili zimevamiwa, kituo cha clouds media kilivamiwa, mwandishi wa gazeti la mwananchi kapotea, Mh. Nape katolewa bastola hadharani, viroba vyenye maiti zinaokotwa kila siku baharini, kwenye chaguzi ndogo tumesikia watu wameuwawa na kuumizwa na wao ndiyo wamekamatwa na kupelekwa mahabusu, Nauli za viongozi wa chama tawala za kuwaambia wafuasi wao wawapige wapinzani kwa kuwa polisi na magereza ni yao wasiogope wataenda kuwachukulia dhamana na Mh. Rais kawaambia watendaji wake ole wake atakaemtangaza mpinzani kashinda na umeona katika viti 43 ccm wamepoteza kimoja tu lakini mkuu wa mkoa kaomba radhi maana yake kuheshimu Uhuru wa watu kuamua kama unavyotuasa waamini ni kosa.! Na mengineeeengi.

Haya yoote baba mpendwa Muadhama huyaoni au huyasikii? Mbona hujakemea maana yanalitafuna taifa chini kwa chini. Kila mtu ameacha taaluma yake na kufuata maagizo. Polisi wakikamata mtu ananyimwa dhamana ukiuliza ni maagizo kutoka juu maana yake hawana sheria wala miongozo ni maagizo toka juu.

Sijakusikia ukikemea watu wasiojulikana, Kuna maswali tunakutana nayo tunakoishi mbona wakati wa Kikwete hukusita kukemea kauli za viongozi ikiwemo ile aliyoisema Mbinga kuhusu uingizaji dawa za kulevya kuhusu viongozi wa dini kuhusika! Na alikuwa sahihi maana alisema Mbele yenu ili mlichukue mjichunguze na mlifanyie kazi lakini ulimshukia mtoto wa watu mpaka watu wanajiuliza ulimfanyia vile sababu ni muislam? Hata katiba mpya makanisa kwa umoja wenu mliungana na kutoa matamko yote yalisomwa makanisani tena wakati wa ibada mbona sasa kimya au sababu raisi alikuwa muislam na sasa ni mkristo tena mkatoliki? Amesema wazi hatawabolea watu wa mwanza na hata baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyume cha sheria kaziacha kisa wale walimpa na wale walimyima kura sasa hiyo kauli ingekuwa imetolewa wakati wa kikwete ungekaa kimya kweli!

Kikwete huyu namkumbuka wakati wa Ramadhani akiwa na swaum aliingia kanisani na mkewe kuliunga kanisa katika msiba wa Askofu Mayalla. Alikuja Mbinga kumsimika Askofu Ndimbo lakini hukumuacha salama hata alipoteleza kama binadamu. Mh. Magufuli mkatoliki safi tena mseminari tokea ameingia nakumbuka matokeo matatu ya kiaskofu, kuwasimikika maaskofu wa shinyanga na Geita na maziko ya Askofu wa TUNDURU-Masasi. Sikumbuki kama kuna alilowahi kuhudhuria. Lakini baba muadhama upo kimya!!!!!!

Tunaomba washauri wa Mzee muelezeni ukweli Baba Muadhama hali sio shwari baina yetu na waumini wa dini nyingine na hata Madhehebu mengine juu ya misimamo ya Cardinal.

Ushauri huu nautoa kwa Baba Askofu mkuu Muadhama Cardinal Polycarp Pengo. Kutokana na mahubiri yake nami ni muumini wa kanisa hilo tokea tarehe 25/01/1975 nilipobatizwa.

Mungu mbariki Baba Askofu wetu, Kanisa letu takatifu! Rais wetu mpendwa na viongozi waandamizi wake wote.
Mungu ibariki Tanzania.

Mwanahabari Huru
 
Pengo katika ubora wake.
Mtumishi wa kweli wa Mungu huchukiwa na Mamlaka, kwa kusimamia ukweli. Ukiona kiongozi wa dini anapendwa na mamlaka za dunia basi ujue mbinguni amehesabiwa dhambi.

ANGALIZO: madhaifu ya Pengo yabaki kuwa ya Pengo pekee yake.
 
View attachment 660766
Tumsifu yesu kristu! Baba Cardinal sisi waamini tunakuelewa sana unaposema tumuunge mkono Mh. Sana Rais wetu nasi tupo nyuma yako na tutatii.
Ila kuna kitu huenda watu hawakuelewi, Je! Ni kwamba udhalimu unaofanywa na serikali hii wewe baba huuoni? Na kama unauona umechukua hatua gani kumsaidia Mh. Rais ili atende kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu? Angalau baba Askofu Augustine Shao wa Zanzibar amegusia kuhusu madhila yatupatayo.

Kama hukumbuki yaliyotokea mwaka huu hata moja huligusii na umekuwa kipaumbele kumpinga anaeonyesha kukerwa mfano umempinga waziwazi Askofu Severine NiweMugizi alipotoa maoni yake ukasema hayo ni maoni yake na sio maoni ya kanisa sasa hayo uliyoyasema tuchukulie ni maoni yako au ya Kanisa? Kama ni ya kanisa umeyatoa kwenye kikao gani na ni nani amekutuma? Kama ni yako binafsi mbona umekuwa mwepesi kupinga wanaotoa maoni yao?
Alphonse Mawazo kauwawa na wanaohisiwa ni wanachama wa chama tawala, Ben Saanane amepotea mpaka leo haonekani, Tundu Lisu kashambuliwa mchana kweupe, ofisi za mawakili zimevamiwa, kituo cha clouds media kilivamiwa, mwandishi wa gazeti la mwananchi kapotea, Mh. Nape katolewa bastola hadharani, viroba vyenye maiti zinaokotwa kila siku baharini, kwenye chaguzi ndogo tumesikia watu wameuwawa na kuumizwa na wao ndiyo wamekamatwa na kupelekwa mahabusu, Nauli za viongozi wa chama tawala za kuwaambia wafuasi wao wawapige wapinzani kwa kuwa polisi na magereza ni yao wasiogope wataenda kuwachukulia dhamana na Mh. Rais kawaambia watendaji wake ole wake atakaemtangaza mpinzani kashinda na umeona katika viti 43 ccm wamepoteza kimoja tu lakini mkuu wa mkoa kaomba radhi maana yake kuheshimu Uhuru wa watu kuamua kama unavyotuasa waamini ni kosa.! Na mengineeeengi.

Haya yoote baba mpendwa Muadhama huyaoni au huyasikii?
Mbona hujakemea maana yanalitafuna taifa chini kwa chini. Kila mtu ameacha taaluma yake na kufuata maagizo. Polisi wakikamata mtu ananyimwa dhamana ukiuliza ni maagizo kutoka juu maana yake hawana sheria wala miongozo ni maagizo toka juu.
Sijakusikia ukikemea watu wasiojulikana,
Kuna maswali tunakutana nayo tunakoishi mbona wakati wa Kikwete hukusita kukemea kauli za viongozi ikiwemo ile aliyoisema Mbinga kuhusu uingizaji dawa za kulevya kuhusu viongozi wa dini kuhusika! Na alikuwa sahihi maana alisema Mbele yenu ili mlichukue mjichunguze na mlifanyie kazi lakini ulimshukia mtoto wa watu mpaka watu wanajiuliza ulimfanyia vile sababu ni muislam? Hata katiba mpya makanisa kwa umoja wenu mliungana na kutoa matamko yote yalisomwa makanisani tena wakati wa ibada mbona sasa kimya au sababu raisi alikuwa muislam na sasa ni mkristo tena mkatoliki? Amesema wazi hatawabolea watu wa mwanza na hata baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyume cha sheria kaziacha kisa wale walimpa na wale walimyima kura sasa hiyo kauli ingekuwa imetolewa wakati wa kikwete ungekaa kimya kweli!
Kikwete huyu namkumbuka wakati wa Ramadhani akiwa na swaum aliingia kanisani na mkewe kuliunga kanisa katika msiba wa Askofu Mayalla. Alikuja Mbinga kumsimika Askofu Ndimbo lakini hukumuacha salama hata alipoteleza kama binadamu. Mh. Magufuli mkatoliki safi tena mseminari tokea ameingia nakumbuka matokeo matatu ya kiaskofu, kuwasimikika maaskofu wa shinyanga na Geita na maziko ya Askofu wa TUNDURU-Masasi. Sikumbuki kama kuna alilowahi kuhudhuria. Lakini baba muadhama upo kimya!!!!!!
Tunaomba washauri wa Mzee muelezeni ukweli Baba Muadhama hali sio shwari baina yetu na waumini wa dini nyingine na hata Madhehebu mengine juu ya misimamo ya Cardinal.

Ushauri huu nautoa kwa Baba Askofu mkuu Muadhama Cardinal Polycarp Pengo. Kutokana na mahubiri yake nami ni muumini wa kanisa hilo tokea tarehe 25/01/1975 nilipobatizwa.

Mungu mbariki Baba Askofu wetu, Kanisa letu takatifu! Rais wetu mpendwa na viongozi waandamizi wake wote.
Mungu ibariki Tanzania.

Mwanahabari Huru

Mfa maji haishi kutapa tapa, sasa mmeanza kumuingiza Karidinali wetu kwenye ujinga wenu, lichama lenu linakufa, mmeliuwa wenyewe sasa mnaanza kutafuta mchawi, wachawi wenu ni Mbowe, Tundu Lisu na Lowasa, hivyo achana na Kardinali wetu!
 
Viongozi wengine Kama akina Pengo wanaomuona mh Rais Kama Mungu asiyekosea na kushindwa kumpa ushauri ndio wanaochangia kwa asilimia kubwa kuzidi kumpoteza rais wetu kwakuwa hawezi kujua ni wapi anapofanya vizuri,wapi anapokosoea na wapi ajirekebishe,Wao kila kitu ni kumpigia makofi.
 
Mkuu hivi hujui kama Kardinali Pengo na Mufti wa Bakwata ni watu wanaochaguliwa na serikali siyo waumini. Na ndiyo maana hata siku moja hawatokuja kuisema serikali kwa ubaya wowote itakaofanya au kuikosea. Serikali ndiyo huwa inapendekeza na awe Mufti au Kardinal.... behind the scene!
 
View attachment 660766
Tumsifu yesu kristu! Baba Cardinal sisi waamini tunakuelewa sana unaposema tumuunge mkono Mh. Sana Rais wetu nasi tupo nyuma yako na tutatii.
Ila kuna kitu huenda watu hawakuelewi, Je! Ni kwamba udhalimu unaofanywa na serikali hii wewe baba huuoni? Na kama unauona umechukua hatua gani kumsaidia Mh. Rais ili atende kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu? Angalau baba Askofu Augustine Shao wa Zanzibar amegusia kuhusu madhila yatupatayo.

Kama hukumbuki yaliyotokea mwaka huu hata moja huligusii na umekuwa kipaumbele kumpinga anaeonyesha kukerwa mfano umempinga waziwazi Askofu Severine NiweMugizi alipotoa maoni yake ukasema hayo ni maoni yake na sio maoni ya kanisa sasa hayo uliyoyasema tuchukulie ni maoni yako au ya Kanisa? Kama ni ya kanisa umeyatoa kwenye kikao gani na ni nani amekutuma? Kama ni yako binafsi mbona umekuwa mwepesi kupinga wanaotoa maoni yao?
Alphonse Mawazo kauwawa na wanaohisiwa ni wanachama wa chama tawala, Ben Saanane amepotea mpaka leo haonekani, Tundu Lisu kashambuliwa mchana kweupe, ofisi za mawakili zimevamiwa, kituo cha clouds media kilivamiwa, mwandishi wa gazeti la mwananchi kapotea, Mh. Nape katolewa bastola hadharani, viroba vyenye maiti zinaokotwa kila siku baharini, kwenye chaguzi ndogo tumesikia watu wameuwawa na kuumizwa na wao ndiyo wamekamatwa na kupelekwa mahabusu, Nauli za viongozi wa chama tawala za kuwaambia wafuasi wao wawapige wapinzani kwa kuwa polisi na magereza ni yao wasiogope wataenda kuwachukulia dhamana na Mh. Rais kawaambia watendaji wake ole wake atakaemtangaza mpinzani kashinda na umeona katika viti 43 ccm wamepoteza kimoja tu lakini mkuu wa mkoa kaomba radhi maana yake kuheshimu Uhuru wa watu kuamua kama unavyotuasa waamini ni kosa.! Na mengineeeengi.

Haya yoote baba mpendwa Muadhama huyaoni au huyasikii?
Mbona hujakemea maana yanalitafuna taifa chini kwa chini. Kila mtu ameacha taaluma yake na kufuata maagizo. Polisi wakikamata mtu ananyimwa dhamana ukiuliza ni maagizo kutoka juu maana yake hawana sheria wala miongozo ni maagizo toka juu.
Sijakusikia ukikemea watu wasiojulikana,
Kuna maswali tunakutana nayo tunakoishi mbona wakati wa Kikwete hukusita kukemea kauli za viongozi ikiwemo ile aliyoisema Mbinga kuhusu uingizaji dawa za kulevya kuhusu viongozi wa dini kuhusika! Na alikuwa sahihi maana alisema Mbele yenu ili mlichukue mjichunguze na mlifanyie kazi lakini ulimshukia mtoto wa watu mpaka watu wanajiuliza ulimfanyia vile sababu ni muislam? Hata katiba mpya makanisa kwa umoja wenu mliungana na kutoa matamko yote yalisomwa makanisani tena wakati wa ibada mbona sasa kimya au sababu raisi alikuwa muislam na sasa ni mkristo tena mkatoliki? Amesema wazi hatawabolea watu wa mwanza na hata baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyume cha sheria kaziacha kisa wale walimpa na wale walimyima kura sasa hiyo kauli ingekuwa imetolewa wakati wa kikwete ungekaa kimya kweli!
Kikwete huyu namkumbuka wakati wa Ramadhani akiwa na swaum aliingia kanisani na mkewe kuliunga kanisa katika msiba wa Askofu Mayalla. Alikuja Mbinga kumsimika Askofu Ndimbo lakini hukumuacha salama hata alipoteleza kama binadamu. Mh. Magufuli mkatoliki safi tena mseminari tokea ameingia nakumbuka matokeo matatu ya kiaskofu, kuwasimikika maaskofu wa shinyanga na Geita na maziko ya Askofu wa TUNDURU-Masasi. Sikumbuki kama kuna alilowahi kuhudhuria. Lakini baba muadhama upo kimya!!!!!!
Tunaomba washauri wa Mzee muelezeni ukweli Baba Muadhama hali sio shwari baina yetu na waumini wa dini nyingine na hata Madhehebu mengine juu ya misimamo ya Cardinal.

Ushauri huu nautoa kwa Baba Askofu mkuu Muadhama Cardinal Polycarp Pengo. Kutokana na mahubiri yake nami ni muumini wa kanisa hilo tokea tarehe 25/01/1975 nilipobatizwa.

Mungu mbariki Baba Askofu wetu, Kanisa letu takatifu! Rais wetu mpendwa na viongozi waandamizi wake wote.
Mungu ibariki Tanzania.

Mwanahabari Huru
Eti Mwanahabari Huru ??? Kumbe ni mwanahabari wa chadema!! Kwenda huko!! Sera zimedoda sasa una hangaika tu!!
 
Pengo ni kiongozi wa kisiasa katika kanisa, mnafiki na wa kujipendekeza.
Kiongozi asiyejali mateso ya waumini wake (wananchi), huyo sio kiongozi wa kiroho hata kidogo labda wa itikadi ile ya mashetani. Hata biblia imeonyesha mifano mingi tu ya jinsi manabii walivyosema na waamini wao kuhusu falme mbali mbali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom