Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe: CHADEMA Isikubali kuonewa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,503
51,098
Ndugu Freeman!
Mara nyingi umesikika ukitaka sana siasa za uungwana, siasa za akupigaye shavu la kushoto basi mgeuzie la kulia. Hilo ni jambo zuri lakini hiyo falsafa yako inafanya kazi katika nchi za watawala ambao ni sober minded, siyo katika nchi ambayo watawala wameamua liwalo na liwe kwenye kusimika mifumo ya dhulma, uonevu ukandamizaji na kufanya lolote ilimradi waendelee kubaki madarakani hata kama si kwa ridhaa za wananchi.

Ndugu Mbowe
Tone yako ya kupenda maridhiano watawala wanaitafsiri kama uoga.

Huu uonevu mnaofanyiwa na watawala wa kunyimwa haki zenu za kufanya siasa kinyume cha katiba mtaendelea kufanyiwa mpaka siku mtakapoamua kusema sasa inatosha!

Ndugu Mbowe, Huu ni muda sasa wa kuvunja confidence hii ya watawala ambayo kimsingi wameshajiaminisha kuwa hamna uwezo, wala guts za kufanya chochote. Hii chain mkiifanikiwa kuivunja mtakuwa katika position nzuri za kuadvance haki zenu za kisiasa nchini.

Huu ni muda muafaka wa kuraise stake katika utawala wa nchi hii ili waone kuwa kutawala kinyume cha sheria na katiba ni kitu chenye gharama, kwa hiyo lazima ufanye yafuatayo:

1. Ni muda muafaka sasa wewe kuhimiza Wafuasi wako wasitii maagizo batili
Toa maagizo yako kwenye machinery nzima ya chama chako, Viongozi na wanachama wa chama chako wasitii maagizo haramu ya watawala katika maeneo yao. Kwa mfano kama Wamezuia mikutano, wewe waagize wafanye mikutano. Wewe usijali wala kuhofu maagizo yako yatafanyiwa kazi kwa kiwango gani, lakini wewe toa agizo la kichama, vikao na mikutano ifanyike. Katika hili kuna watakaofanikiwa kufanya hiyo mikutano kuna watakaoshindwa kwa sababu mbalimbali, lakini ni lazima tuvunje hii chain ya utii haramu wa maagizo haramu yaliyo kinyume cha sheria

2. Ni lazima CHADEMA iendelee kuwin huruma ya wananchi
Haya matendo mnayofanyiwa ya uonevu na ukandamizaji, wananchi wanayaona. Sasa ni muda muafaka wa kuyadocument vizuri, kuyaamplify ili wananchi wengi wayaone. Uonevu ambao watawala wanawafanyia kama mtaweza kuwashitakia, uungwaji mkono utakuwa ni mkubwa, na utaendekea kukua siku baada ya siku

3. Ndugu Mbowe ni muda wa Uongozi wa CHADEMA kusacrifice zaidi
Ndugu Mbowe, kama nilivyokueleza huko juu, kuna ulazima wa kuvunja chain hii ya uonevu, hili halitifanyika bila uongozi wa CHADEMA kujitoa mhanga(kusacrifice), Ni lazima uongozi wa CHADEMA uitishe mikutano ya wazi ambayo ni ya haki kisheria, ikizuiwa kinyume cha sheria Viongozi wa CHADEMA wasitii, Kubalini kusacrifice hata Jela lakini haki yenu kama Chama muipate. Na hii mikutano isiwe one day event, itisheni hii mikutano mara kwa mara mpaka watawala waone kuwa gharama za kupambana na CHADEMA ni kubwa kuliko kutenda haki.

Ndugu Mbowe, Hii chain ya nyie kuonewa hamtaivunja mpaka msacrifice, muwe tayari kwenda jela kwa ajili ya course hiyo

4. Ni lazima CHADEMA itumie fursa za serikali ya CCM kuboronga kwenye uchumi ili kuvuna sapoti ya wananchi
Ndugu Mbowe, Kimsingi, CCM wanajua measures zao za kiuchumi ni unpopular kwa wananchi, pia wanajua legitimacy yao ya kisiasa kwa wananchi ni ndogo sana, kwa hiyo wanachokifanya ni kujaribu kwa nguvu zote kuweka ukuta baina yenu na wananchi ili msiwape hao watawala kibano cha kisiasa. Ni lazima message yenu sasa muiegemeze katika ugumu wa maisha ambayo wananchi wanapitia na kwenye fact kuwa tumefika hapa kwa sababu ya utawaka mbovu wa CCM na wananchi hawana wawakilishi waliotokana na ridhaa zao. Tumieni kila opportunity, tengenezeni talking points za matatizo ya kiuchumi muzisambaze hadi huko chini kwa viongozi wenu wa ngazi za chini ili waweze kuwaeleza wananchi kwa ufasaha kabisa madhila ya utawala wa CCM kwenye maisha yao, na namna CCM inavyopekekea wao kuwa na maisha Magumu

5. Ni muda muafaka wa kumuomba kila mwanachadema afanye kazi ya kusambaza ujumbe wa Chama
Ndugu Mbowe, CCM wanadhani wanaweza kudhibiti moto wa CHADEMA kwa kuthibiti uongozi ambao uko structured, kwamba wakidhibiti let say viongozi wa matawi, mashina, kanda na viongozi Taifa basi wataweza kukithibiti Chama. Sasa ni muda muafaka wa Chadema kutoa muongozo kwa kila mwanachama na shabiki na Chadema kufanya kazi za chama za kusambaza jumbe na sera za chama. Agiza kila mtu, afikishe ujumbe na sera za chama kwa marafiki, kwa majirani n. k. Yaani kwenye suala la kusambaza jumbe za CHAMA isiwe muda wote centralized bali nyakati kama hizi ngumu mnazozuiwa kuorganise iwe ni decentralized. Hii itawezesha ujumbe kufika pale ambapo watawala hawataki mfike!

6. Ni lazima kuionyesha sura halisu ya Rais Samia, ajulikane kabisa kuwa naye anaenjoy "urahisi wa Udikteta" na anachukia "ugumu wa demokrasia"
Demokrasia siyo kazi nyepesi, inahitaji kutumia akili zaidi, kujizuia zaidi, kuwa na subira zaidi, maridhiano zaidi. Sasa hayo ni mambo magumu kuliko udikteta ambao madikteta hawataki kuumiza kichwa sana kwenye utawala, wao wanataka kutumia miguvuguvu tu
Sasa Samia inaonekana kabisa anataka kufuata njia za Mtangulizi wake, hataki tabu, anataka kutawala kwa mteremko. Lakini wakati huohuo anataka kuudanganya ulimwengu kuwa yeye ni mwanademokrasia, Hataki kuitwa "DICTATOR". Sasa CHADEMA isikubali kumpa hii blank cheque, kama anafanya Udikteta aitwe dikteta, asakamwe kwa udikteta wake.
Na hapa naungana na John Heche, Acheni kumuita Samia MAMA. hii inampa soft power, na moral authority ambayo connotation ya mama inabeba. Kiufupi kama anavunja katiba ya nchi basi haistahili kuendelea kutumia hilo jina mama, muiteni kwa jina lake halisi, kama ni dikteta basi aitwe Dikteta.

7. Madai ya Katiba mpya ni turufu inayopaswa kutumika kwa nguvu zote
Ndugu Freeman, katika vitu ambavyo wananchi wengi wanakubali, bila kujali mirengo yao ya kisiasa ni katiba mpya. Hii ni turufu kubwa ambayo hata CCM wanashindwa waihandle vipi. Sasa ni muhimu sana nyie kuiframe agenda hii kuwa ni kwa ajili ya masilahi ya wananchi zaidi, katika kufanya hivyo nashauri nyie kama chama mkae muandae points za namna gani Katiba mpya inagusa maisha ya watu moja kwa moja. Hizi talk points zisambazwe kwa makada wenu wote nchi nzima. Lengo hapa ni kuondoa ile spin kuwa nyie mnapigania katiba mpya kwa ajili ya madaraka tu.

Elezeni faida za bunge na mahakama huru, elezeni katiba mpya inapambanaje na ufisadi, elezeni katiba mpya ina uhusiano gani na maji yao, elimu ya, afya yao. Namna hii mtaweza kuwashawishi wananchi wawe active zaidi na zaidi katika kuidai na kuilszimisha serikali ya CCM ilete hiyo katiba mpya. Msiishie tu kuzungumzia ishu ya tume huru ya uchaguzi na madaraka ya rais jinsi yasivyo fair bali onyesheni jinsi vitu hivyo vinavyopelekea maisha ya watu kuwa magumu zaidi.

Mwisho kabisa ndugu Mbowe napenda kukwambia kuwa sasa ni muda muafaka wa kuraise joto la kisiasa nchini, lipandisheni kwa kugomea amri haramu. Fanyeni mikutano hata kama imezuiwa kinyume cha sheria. Hawa hawana mabomu, wala askari wa kutosha wa kuweza kupambana na HAKI

Chairman, mmeonewa kiasi cha kutosha, mmenyanyaswa kiasi cha kutoshao sasa fanya jambo, tumechoka!
 
Matukio ya ukaidi na kuto kutii sheria na utaratibu kwa maksudi yanayo fanywa na Chadema ni jambo baya sana kwa mustakbali wa vyama vya upinzani vyote.

vyama vingine vya upinzani ni lazima vikemee vikali tabia za kihuni na zenye nia ya kuvuruga amani ya nchi yetu kwani tabia hiyo inayo fanywa na Chadema inachafua taswira ya vyama vingine vya upinzani ambavyo vinaendesha siasa zao kistaarabu.

Mbowe amesikika mara kadhaa akichochea maandamano yasiyo halali, n.k nadhani ni wakati sasa kwa Msajili wa vyama Kukifuta hiki chama cha Chadema kwa maslahi ya Amani ya nchi yetu.

Amani ya nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko Chadema.
 
Pole kwa ujumbe,hoja unayo isipokuwa umejiondoa kwenye vita unayoshawishi itumike.

No 2 Mbowe usitangaze kitu chochote, bali endelea kutoa elimu ya chama chako na elimu ya uhitaji wa katiba.

Muda utafika wananchi wataamua ukweli ni upi na njia gani itumike.
 
Pole kwa ujumbe,hoja unayo isipokuwa umejiondoa kwenye vita unayoshawishi itumike. No 2 Mbowe usitangaze kitu chochote,Bali endelea kutoa elimu ya chama chako na elimu ya uhitaji wa katiba. Muda utafika wananchi wataamua ukweli ni upi na njia gani itumike.
Wewe kwani kipofu?

Hakuna neno vita hapo, bali ni kukataa kutii amri haramu
 
Inashangaza sana, Chadema wakilazimisha kufanya mambo yanayotambulika kisheria wanaonekana wanafanya fujo, hii mentality mbovu imejaa kwa viongozi wote wa CCM na wanachama wao lazima iondolewe, wajue wana wajibu wa kutii sheria za nchi kwani sheria zipo kwa ajili yetu sote.
 
Mbowe, msaanii tu wafuasi wake nyie Pro-Chadema JF na kule Twitter kina kigogo na kundi, unakumbuka Mbowe aligombea urais akapata kura laki 4, mnajazana ujinga tu kama una uchungu ingia barabarani.

Chama chochote kishike dola mambo ni hayo hayo wacha Samia akupigeni spana hamtaki kumuheshimu na mnamzonga,ndio Kwanza miezi minne mnampanda kichwani
 
Ndugu Freeman!

Mara nyingi umesikika ukitaka sana siasa za uungwana, siasa za akupigaye shavu la kushoto basi mgeuzie la kulia. Hilo ni jambo zuri lakini hiyo falsafa yako inafanya kazi katika nchi za watawala ambao ni sober minded, siyo katika nchi ambayo watawala wameamua liwalo na liwe kwenye kusimika mifumo ya dhulma, uonevu ukandamizaji na kufanya lolote ilimradi waendelee kubaki madarakani hata kama si kwa ridhaa za wananchi.

Ndugu Mbowe
Tone yako ya kupenda maridhiano watawala wanaitafsiri kama uoga.

Huu uonevu mnaofanyiwa na watawala wa kunyimwa haki zenu za kufanya siasa kinyume cha katiba mtaendelea kufanyiwa mpaka siku mtakapoamua kusema sasa inatosha!

Ndugu Mbowe, Huu ni muda sasa wa kuvunja confidence hii ya watawala ambayo kimsingi wameshajiaminisha kuwa hamna uwezo, wala guts za kufanya chochote. Hii chain mkiifaniisha mtakuwa katika position nzuri za kuadvance haki zenu za kisiasa nchini.

Huu ni muda muafaka wa kuraise stake katika utawala wa nchi hii ili waone kuwa kutawala kinyume cha sheria na katiba ni kitu chenye gharama, kwa hiyo lazima ufanye yafuatayo:

1. Ni muda muafaka sasa wewe kuhimiza Wafuasi wako wasitii maagizo batili.

Toa maagizo yako kwenye machinery nzima ya chama chako, Viongozi na wanachama wa chama chako wasitii maagizo haramu ya watawala katika maeneo yao. Kwa mfano kama Wamezuia mikutano, wewe waagize wafanye mikutano. Wewe usijali wala kuhofu maagizo yako yatafinywa kazi kwa kiwango gani, lakini wewe toa agizo la kichama, vikao na mikutano ifanyike. Katika hili kuna watakaofanikiwa kufanya hiyo mikutano kuna watakaoshindwa kwa sababu mbalimbali, lakini ni lazima tuvunje hii chain ya utii haramu wa maagizo haramu yaliyo kinyume cha sheria

2. Ni lazima CHADEMA iendelee kuwin huruma ya wananchi.

Haya matendo mnayofanyiwa ya uonevu na ukandamizaji, wananchi wanayaona. Sasa ni muda muafaka wa kuyadocument vizuri, kuyaamplify ili wananchi wengi wayaone. Uonevu ambao watawala wanawafanyia kama mtaweza kuwashitakia, uungwaji mkono utakuwa ni mkubwa, na utaendekea kukua siku baada ya siku

3.Ndugu Mbowe ni muda wa Uongozi wa CHADEMA kusacrifice zaidi

Ndugu Mbowe, kama nilivyokueleza huko juu, kuna ulazima wa kuvunja chain hii ya uonevu, hili halitifanyika bila uongozi wa CHADEMA kujitoa mhanga(kusacrifice), Ni lazima uongozi wa CHADEMA uitishe mikutano ya wazi ambayo ni ya haki kisheria, ikizuiwa kinyume cha sheria Viongozi wa CHADEMA wasitii, Kubalini kusacrifice hata Jela lakini haki yenu kama Chama muipate. Na hii mikutano isiwe one day event, itisheni hii mikutano mara kwa mara mpaka watawala waone kuwa gharama za kupambaba na CHADEMA ni kubwa kuliko kutenda haki.

Ndugu Mbowe, Hii chain ya nyie kuonewa hamtaivunja mpaka msacrifice, muwe tayari kwenda jela kwa ajili ya course hiyo

4. Ni lazima CHADEMA itumie fursa za serikali ya CCM kuboronga kwenye uchumi ili kuvuna sapoti ya wananchi.

NNdugu Mbowe, Kimsingi, CCM wanajua measures zao za kiuchumi ni unpopular kwa wananchi, pia wanajua legitimacy yao ya kisiasa kwa wananchi ni ndogo sana, kwa hiyo wanachokifanya ni kujaribu kwa ngubu zote kuweka Ukuta baina yenu na wananchi ili msiwape kibano cha kisiasa. Ni lazima message yenu sasa muiegemeze katika ugumu wa maisha ambayo wananchi wanapitia na kwenye fact kuwa tumefika haa kwa sababu wananchi hawana wawakilishi waliotokana na ridhaa zao. Tumieni kila opportunity, tengenezeni talking points za matatizo ya kiuchumi muzisambaze hadi huko chini kwa viongozi wenu wa ngazi za chini ili waweze kuwaeleza wananchi kwa ufasaha kabisa madhila na ya utawala wa CCM kwenye maisha yao, na namna CCM inavyopekekea wao kuwa na maisha Magumu

5. Ni muda muafaka wa kumuomba kila mwanachadema afanye kazi ya kusambaza ujumbe wa Chama.

Ndugu Mbowe, CCM wanadhani wanaweza kudhibiti moto wa CHADEMA kwa kuthibiti uongozi ambao uko structured, kwamba wakidhibiti let say viongozi wa matawi, mashina, kanda na viongozi Taifa basi wataweza kukithibiti Chama. Sasa ni muda muafaka wa Chadema kutoa muongozo kwa kila mwanachama na shabiki na Chadema kufanya kazi za chsna za kusambaza jumbe na sera za chama. Agiza kila mtu, afikishe ujumbe na sera za chama kwa marafiki, kwa majirani n. k. Yaani kwenye suala la kusambaza jumbe za CHAMA isiwe muda wote centralized bali nyakati kama hizi ngumu mnazozuiwa kuorganise iwe ni decentralized. Hii itawezesha ujumbe kufika pale ambapo watawala hawataki mfike!

6. Ni lazima kuionyesha sura halisu ya Rais Samia, ajulikane kabisa kuwa naye anaenjoy "urahisi wa Udikteta" na anachukia "ugumu wa demokrasia"

Demokrasia siyo kazi nyepesi, inahitaji kutumia akili zaidi, kujizuia zaidi, kuwa na subira zaidi, maridhiano zaidi. Sasa hayo ni mambo magumu kuliko udikteta ambao madikteta hawataki kuumiza kichwa sana kwenye utawala, wao wanataka kutumia miguvuguvu tu
Sasa Sania inaonekana kabisa anataka kufuata njia za Mtangulizi wake, hataki tabu, anataka kutawala kwa mteremko. Lakini wakati huohuo anataka kuudanganya ulimwengu kuwa yeye ni mwanademokrasia, Hataki kuitwa "DICTATOR". Sasa CHADEMA isikubali kumpa hii blank cheque, kama anafanya Udikteta aitwe dikteta, asakamwe kwa udikteta wake.
Na hapa naungana na John Heche, Acheni kumuita Samia MAMA. hii inampa soft power, na moral authority ambayo connotation ya mama inabeba. Kiufupi kama anavunja katiba ya nchi basi haistahili kuendelea kutumia hilo jina mama, uiteni kwa jina lake halisi, kama ni dikteta basi aitwe Dikteta.

7. Madai ya Katiba mpya ni turufu inayopaswa kutumika kwa nguvu zote

Ndugu Freeman, katika vitu ambavyo wananchi wengi wanakubali, bila kujali mirengo yao ya kisiasa ni katiba mpya. Hii ni turufu kubwa ambayo hata CCM wanashindwa waihandle vipi. Sasa ni muhimu sana nyie kuigrame agenda hii kuwa ni kwa ajili ya masilahi ya wananchi zaidi, katika kufanya hivyo nashauri nyie kama chama mkae muandae points za namna gani Katiba mpya inagusa maisha ya watu moja kwa moja. Hizi talk points zisambazwe kwa makada wenu wote nchi nzima. Lengo hapa ni kuondoa ile spin kuwa nyie mnapigania katiba mpya kwa ajili ya madaraka tu. Elezeni faida za bunge na mahakama huru, elezeni katiba mpya inapambanaje na ufisadi, elezeni katiba mpya ina uhusiano gani na maji yao, elimu ya, afya yao. Namna hii mtaweza kuwashawishi wananchi wawe active zaidi na zaidi katika kuidai na kuilszimisha serikali ya CCM ilete hiyo katiba mpya. Msiishie tu kuzungumzia ishu ya tume huru ya uchaguzi na madaraka ya rais jinsi yasivyo fair bali onyesheni jinsi vitu hivyo vinavyopelekea maisha ya watu kuwa magumu zaidi.

Mwisho kabisa ndugu Mbowe napenda kukwambia kuwa sasa ni muda muafaka wa kuraise joto la kisiasa nchini, lipndisheni kwa kugomea amri haramu. Fanyeni mikutano hata kama imezuiwa kinyume cha sheria.
Hawa hawana mabomu, waka askari wa kutosha wa kuweza kupambana na HAKI

Chairman, mmeonewa kiasi cha kutosha, mmenyanyaswa kiasi cha kutoshao sasa fanya jambo, tumechoka!
Mh Mbowe chukua ushauri huu, Kama mbwai mbwai
 
Inashangaza sana, Chadema wakilazimisha kufanya mambo yanayotambulika kisheria wanaonekana wanafanya fujo, hii mentality mbovu imejaa kwa viongozi wote wa CCM na wanachama wao lazima iondolewe, wajue wana wajibu wa kutii sheria za nchi kwani sheria zipo kwa ajili yetu sote.
Hata mimi nashangaa, kuna watu Wanataka Chadema itii tu amri ambazo siyo za haki.

Chadema wakiikubali hii hali maana yake ni kuwa kamwe hakitopata fursa ya kuwafikia wwnanchi ipasavyo na kutafuta kuungwa mkono.

CCM wanataka kuilimit Chadema isikue
 
Matukio ya ukaidi na kuto kutii sheria na utaratibu kwa maksudi yanayo fanywa na Chadema ni jambo baya sana kwa mustakbali wa vyama vya upinzani vyote.

vyama vingine vya upinzani ni lazima vikemee vikali tabia za kihuni na zenye nia ya kuvuruga amani ya nchi yetu kwani tabia hiyo inayo fanywa na Chadema inachafua taswira ya vyama vingine vya upinzani ambavyo vinaendesha siasa zao kistaarabu.

Mbowe amesikika mara kadhaa akichochea maandamano yasiyo halali, n.k nadhani ni wakati sasa kwa Msajili wa vyama Kukifuta hiki chama cha Chadema kwa maslahi ya Amani ya nchi yetu.

Amani ya nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko Chadema.
Hivyo unaona mazuri yanatofanywa na maharami pekee.
 
Utopolo tupu! Wewe umejificha nyuma ya keyboard unataka Mbowe akanyee debe tena? Ulimsaidia nini wakati ule ananyea debe mkuu?
 
Hata mimi nashangaa, kuna watu Wanataka Chadema itii tu amri ambazo siyo za haki.

Chadema wakiikubali hii hali maana yake ni kuwa kamwe hakitopata fursa ya kuwafikia wwnanchi ipasavyo na kutafuta kuungwa mkono.

CCM wanataka kuilimit Chadema isikue
Baada ya cdm kuwa chama pendwa kwa wananchi, mara moja CCM ilijibanza kwenye vyombo vya dola. Kwasasa ccm imejisahau kabisa, maamuzi ya rais ndio yamegeuka sheria. Ni wakati sasa cdm kwenda mahakamani kupata tafsiri ya kisheria kuhusu mikutano na ufanyaji siasa ndani ya hii nchi.

Sioni CCM ikikubali tena cdm kufikia wananchi, hasa ukizingatia kwa sasa wako madarakani bila ridhaa ya umma. Wakati utaratibu wa kisheria ukiendelea, lazima watu wafanye mikutano ya ndani ama nje kwa lazima kama sheria itakavyo. Kwenye maamuzi haya namuona Mbowe kuwa tayari amefika mwisho, uenyeji apewe John Heche kwani ana maamuzi magumu.
 
Mh Mbowe chukua ushauri huu, Kama mbwai mbwai
Kama kweli ni vidume, waanze ktk viwanja vya biafra, wajitokeze mbele Mbowe, Kigaia, Mnyika, Lwaitama na Mwalimu, msigwa, wote hao wanao uhakika wa familia zao kula bila shida yoyote, tabu ni wafuata upepo tutaabisha familia zetu bure.
 
Back
Top Bottom