munisijo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 1,113
- 927
Ndugu yangu George J Minja,
Awali ya yote nikupe pole kwani ingawa umejaribu kumpaka matope kishkaji Shonza na kuanza kumtuhumu Heche (ambaye hahusiki kabisa na theme ya mada yako); na kutokana na tarehe uliyojiunga hapa JF, inathibitisha kuwa uko kazini kutumika. Bahati mbaya kwako ni kwamba, uwezo na upeo wako kukufanya uwe hapa katika JF, haukidhi matakwa na dhima - yaani kuwa Great Thinker.
1. Barua hiyo haina mapungufu yeyote kama ulivyotaka kupotosha. Shonza amefukuzwa uanachama wa BAVICHA. Tuhuma zilizokuwa zinamkabili zimewekwa wazi katika barua hiyo na hata mtiririko mzima wa mashtaka umewekwa. Maamuzi ya kikao kwa lugha ya kawaida kuitwa 'Maazimio' na katika uandishi tunasema Kikao Kiliazimia (kiliamua) yafuatayo. Kingereza chake ni resolution. Na kwa wale walioko kwenye Taasisi za kufanya kazi, watakumbuka kitu kinachoitwa BOARD RESOLUTION. Hivyo uache kupotosha watu kwa makusudi.
2. Mamlaka halali imekaa na ikafikia maamuzi; na imefanya kulingana na Katiba yake, je kwa nini itafute second opinion? Kama Kamati ingekaa na kuandika 'mapendekezo', then muktasari wa kikao ndiyo ungepelewa ukiwa na mapendekezo kwa authority ya juu ambayo wajibu wake ni aidha kukubaki au kukataa hayo mapendekezo. For this case, kikao hichi halali, kimefanya maamuzi. Wakubwa wamepewa tu taarifa (Rejea Barua, Katibu Mkuu wa CHADEMA anapewa tu taarifa)
3. Ulitaka John Heche aje ajadili kuhusu jina? Katika taarifa ya Shonza alikuwa anatumia majina yote mawili kumwita Heche; hakuna popote alipotoa tuhuma zozote kuhusu hilo jina la pili. Hivyo, kama ni tuhuma ziwekwe wazi, na ushahidi uwekwe then John Heche atakuja kujibu.
Uandishi wa namna hii kama ulivyoufanya wewe na Juliana Shonza, si tu unapoteza hadhi ya JF, bali pia unafanya hapa paonekane kijiwe na majungu, sehemu ya watu ambao hawajasoma, lakini pia tunajenga picha mbaya ya elimu mliyoisoma na vyuo vyenu(tunavionea kutokana na madhambi yenu)
MWISHO
Leo mchana Shonza alilalamika kutokupata barua; wewe umeipata wapi? Umeipataje? Maana kama anajificha haonekani na anafanya vurumai, then haitamsaidia kitu. Halafu hata makazini, kama mwajiri hakutaki na amekufukuza kazi, hauwezi ukang'ang'ania ofisi, badala yake unakimbilia CMA ili haki yako ipatikane. Lakini kama hakutaki, no matter what, atakulipa visenti vyako vya miezi 12, unampisha, anaendelea na maisha yake na wafanyakazi wake wengine ambao ni loyal
Cc Molemo Crashwise Ben Saanane Juliana Shonza Mtela Mwampamba, Mchange & Mwita Maranya
Dah, sasa mbona umemaliza point zote za maana...s wengine tuchangie nini hpgasa??!!
Anyway, asante sana 'kamanda'!
Last edited by a moderator: