Barua ya Kumfukuza Juliana Shonza na aibu kwa BAVICHA

George J Minja

JF-Expert Member
Jan 8, 2013
289
202
Mimi sio masalia lakini lazima nisema ukweli:

Hii barua ina mapungufu mengi sana na inatia mashaka juu ya uongozi wa BAVICHA.

Kichwa cha habari cha barua hii kinasema KUFUKUZWA UANACHAMA WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA lakini para ya pili kutoka mwisho inasema BARAZA LIMEAZIMIA KUKUFUKUZA.

Tafsiri yake ni kuwa Baraza halijamfukuza Shonza bali limedhamiria kumfukuza baadae basi muweke hapa barua ya kumfukuza, huu ni UPUUZI, kama hamuwezi kuandika hata barua kwa umakini ni dalili mbaya.

Pili Kikao kimekaa tarehe 5 barua ikatoka tarehe 6 yaani hata hamkuwa na muda wa kuwashirikisha viongozi wenu wa juu kwa maana ya viongozi wakuu wa Chama kuhusu hili ikizingatiwa Shoza ambaye mimi namuona kama kilaza sana na mjinga wa kwanza alikuwa kiongozi mwenzenu wa ngazi ya juu

Jirekebisheni, hii inanipa shaka kubwa na viongozi wa BAVICHA.

Kwanza uwezo wa Juliana Shonza kama Makamu Mwenyekiti ni mdogo sana hakustahili hiyo nafasi na pili Uandishi huu wa Katibu mkuu wa baraza unanipa mashaka na uwezo wake pia

Lakini Tatu na kubwa shutuma za jina halisi la John Heche hazijajibiwa mpaka sasa iku inakaribia kuisha je tumuingize kwenye kundi la kina Mulugo Amim na Mwigulu Nchemba??

attachment.php

attachment.php

Majibu ya BAVICHA
By SEBM

Ndugu yangu George Minja,

Awali ya yote nikupe pole kwani ingawa umejaribu kumpaka matope kishkaji Shonzana kuanza kumtuhumu Heche (ambaye hahusiki kabisa na theme ya mada yako); nakutokana na tarehe uliyojiunga hapa JF, inathibitisha kuwa uko kazini kutumika.Bahati mbaya kwako ni kwamba, uwezo na upeo wako kukufanya uwe hapa katika JF,haukidhi matakwa na dhima - yaani kuwa Great Thinker.

1. Barua hiyo haina mapungufu yeyote kama ulivyotaka kupotosha. Shonzaamefukuzwa uanachama wa BAVICHA. Tuhuma zilizokuwa zinamkabili zimewekwa wazikatika barua hiyo na hata mtiririko mzima wa mashtaka umewekwa. Maamuzi ya kikaokwa lugha ya kawaida kuitwa 'Maazimio' na katika uandishi tunasema KikaoKiliazimia (kiliamua) yafuatayo. Kingereza chake ni resolution. Na kwa walewalioko kwenye Taasisi za kufanya kazi, watakumbuka kitu kinachoitwa BOARDRESOLUTION. Hivyo uache kupotosha watu kwa makusudi.

2. Mamlaka halali imekaa na ikafikia maamuzi; na imefanya kulingana na Katibayake, je kwa nini itafute second opinion? Kama Kamati ingekaa na kuandika'mapendekezo', then muktasari wa kikao ndiyo ungepelewa ukiwa na mapendekezo kwaauthority ya juu ambayo wajibu wake ni aidha kukubaki au kukataa hayomapendekezo. For this case, kikao hichi halali, kimefanya maamuzi. Wakubwawamepewa tu taarifa (Rejea Barua, Katibu Mkuu wa CHADEMA anapewa tu taarifa)

3. Ulitaka John Heche aje ajadili kuhusu jina? Katika taarifa ya Shonza alikuwaanatumia majina yote mawili kumwita Heche; hakuna popote alipotoa tuhuma zozotekuhusu hilo jina la pili. Hivyo, kama ni tuhuma ziwekwe wazi, na ushahidiuwekwe then John Heche atakuja kujibu.

Uandishi wa namna hii kama ulivyoufanya wewe na Juliana Shonza, si tu unapotezahadhi ya JF, bali pia unafanya hapa paonekane kijiwe na majungu, sehemu ya watuambao hawajasoma, lakini pia tunajenga picha mbaya ya elimu mliyoisoma na vyuovyenu(tunavionea kutokana na madhambi yenu)

MWISHO
Leo mchana Shonza alilalamika kutokupata barua; wewe umeipata wapi? Umeipataje?Maana kama anajificha haonekani na anafanya vurumai, then haitamsaidia kitu.Halafu hata makazini, kama mwajiri hakutaki na amekufukuza kazi, hauwezi ukang'ang'aniaofisi, badala yake unakimbilia CMA ili haki yako ipatikane. Lakini kamahakutaki, no matter what, atakulipa visenti vyako vya miezi 12, unampisha,anaendelea na maisha yake na wafanyakazi wake wengine ambao ni loyal

Cc
MolemoCrashwiseBen SaananeJulianaShonza Mtema Mwampamba MchangeMwita Maranya




Majibu yangu
George J Minja
Nakushukuru sana kwa majibu mazuri yanayoridhisha ila wachana mimi niseme mawili matatu yaliyonigusa kutokana na majibu yako

1.Kutumika
Hii ni dharau na ni tusi,kujiunga kwangu JF tarehe za karibuni hakunifanye niweMtumikaji hasa wa Masalia kama unavyosema,wako watu wengi wanaojiunga na JFhata leo kwa nia njema na wala sio wapinzani wa BAVICHA na CHADEMA.Nakuombaufute kauli yako ya kusema mimi natumika hasa kwa kigezo cha kujiunga JF hivikaribuni kwani hii inawadhalilisha wote wanaojiunga JF baada ya mgogoro wenundani ya BAVICHA.

2.Usomi na Kijiwe cha majungu

Ukisoma kanuni za JF vizuri hakuna mahali popote imeandikwa kuwa hili ni jukwaala wasomi na kwa taarifa yako Great Thinkers wengi wa leo sio wasomi baliwasomi wengi ndio wapuuzi wanaoharibu mustakabali wa nchi yetu rejea maneno yaMzee Butiku siku ya kuazimisha miaka 51 ya uhuru pale Nkhrumah Hall.

3.Utaratibu wa kumfukuza Juliana Shoza

Nakubaliana na wewe bila shaka kuwa mamlaka iliyokaa na kumfukuza Shoza inabaraka za katiba lakini upo utaratibu wa ndani ambao mara zote Utawala Boraunahitaji ufuatwe na hili halikufanyika pamoja na kwamba Shoza alikuwa hanamamlaka juu ya Kamati Tendaji lakini alikuwa Kiongozi wa juu wa Chama,akitumika katika BAVICHA.hauhitaji katiba kukuueleza jinsi ya kupata ushaurikabla ya maamuzi makubwa.

4.Lugha iliyotumiwa kwenye barua

Hii ni aibu kubwa kuwa unatetea UJINGA na UPUUZI ule ule ulioufanya kwenyebarua ,Kiingereza ni Lugha na ina misamiati yake na wakati mwingine ukiitafsirikwa kiswahili utapata maana nyingine kabisa,kulikuwa hakuna haja ya kulichukuaneno RESOLUTION in Mutatis Mutandis way na kulifanay KUAZIMIA??hivi kweliKUAZIMIA na KUKUFUKUZA n i sawa,kuna shida kubwa hapo lazima ukiri,ilikuwarahisi na ya kueleweka tuu kama mngeandika TUMEKUFUKUZA na mbona kwenye kichacha habari hukuandika TUNAAZIMIA??kama ni neno sahihi ungeanza nalo basi kwenyekicha cha habari ungesema TUMEAZIMIA ,hakika isingeleta maana kama isivyoletamaana kwenye para ya nne.


5-Kupata Barua

Huu ni upuuzi mwingine na kutojitambua wewe umepost hapa kwenye thread ya Shozana mimi nimeipata hapo,sasa unaniuliza nimeipata wapi,mimi ningekuwa nayoningeiweka hapa siku nyingi lakini nimeipata hapa nikaisoma na kuamua kuikosoasasa unaanza kuhoji nilipoipata wakati wewe umeweka hapa mwenyewe


6-Masalia

Mimi sio masalia na narudia tena sio MASALIA wala PM7.Ila masaliamnaowazungumzia ni wapi??ni hao mliowafukuza BAVICHA au ni pamoja namnaowaogopa??wakati wa tuhuma zile alitajwa Zitto Kabwe kama kiongozi wa Masaliana PM7

lakini hamjamchukulia hatua zozote na hata uongozi wa juu wa chama haujamuhojiwala kumfukuza mnamuogopa kwa kuwa mnafikiri ana mtaji mkubwa wa watu,mmebakiakusema kila anayejiunga hapa na kuwapinga ni masalia je hao mliowafukuza kwatuhuma ambazo Zitto ametajwa kama kiongozi wenu mmewatendea haki??Kwa ninihamumfukuzi Zitto?

7-John Heche

Narudia tena namheshimu sana Heche na ninamuamini kuliko nyie wanafkimnaomzunguka kwa sababu anao uwezo wa kuongoza ,anayo nia ya kuwakomboawatanzania na ukimwangalia usoni unaliona hilo lakini jina lake limetajwa hapakwa namna tofauti SUGUTI mimi nahoji ni nani huyu??ni jna la wapi hilisilijui,sasa ukinishambulia mimi unapigana na kivuli chako mimi sina shida naHeche nataka ufafanuzi na hii sio lazima iletwe kama shutuma kiongozi bora naanayejali hujibu mambo kama haya,sasa nyie walamba miguu bootleakeres mmekaanaye hapo hammshauri ajibu mnaanza kupambana na mimi sio sawa.
 

Attachments

  • shonza1.png
    shonza1.png
    19.8 KB · Views: 7,478
  • shonza2.png
    shonza2.png
    14.7 KB · Views: 6,693
Ndugu yangu George J Minja,

Awali ya yote nikupe pole kwani ingawa umejaribu kumpaka matope kishkaji Shonza na kuanza kumtuhumu Heche (ambaye hahusiki kabisa na theme ya mada yako); na kutokana na tarehe uliyojiunga hapa JF, inathibitisha kuwa uko kazini kutumika. Bahati mbaya kwako ni kwamba, uwezo na upeo wako kukufanya uwe hapa katika JF, haukidhi matakwa na dhima - yaani kuwa Great Thinker.

1. Barua hiyo haina mapungufu yeyote kama ulivyotaka kupotosha. Shonza amefukuzwa uanachama wa BAVICHA. Tuhuma zilizokuwa zinamkabili zimewekwa wazi katika barua hiyo na hata mtiririko mzima wa mashtaka umewekwa. Maamuzi ya kikao kwa lugha ya kawaida kuitwa 'Maazimio' na katika uandishi tunasema Kikao Kiliazimia (kiliamua) yafuatayo. Kingereza chake ni resolution. Na kwa wale walioko kwenye Taasisi za kufanya kazi, watakumbuka kitu kinachoitwa BOARD RESOLUTION. Hivyo uache kupotosha watu kwa makusudi.

2. Mamlaka halali imekaa na ikafikia maamuzi; na imefanya kulingana na Katiba yake, je kwa nini itafute second opinion? Kama Kamati ingekaa na kuandika 'mapendekezo', then muktasari wa kikao ndiyo ungepelewa ukiwa na mapendekezo kwa authority ya juu ambayo wajibu wake ni aidha kukubaki au kukataa hayo mapendekezo. For this case, kikao hichi halali, kimefanya maamuzi. Wakubwa wamepewa tu taarifa (Rejea Barua, Katibu Mkuu wa CHADEMA anapewa tu taarifa)

3. Ulitaka John Heche aje ajadili kuhusu jina? Katika taarifa ya Shonza alikuwa anatumia majina yote mawili kumwita Heche; hakuna popote alipotoa tuhuma zozote kuhusu hilo jina la pili. Hivyo, kama ni tuhuma ziwekwe wazi, na ushahidi uwekwe then John Heche atakuja kujibu.

Uandishi wa namna hii kama ulivyoufanya wewe na Juliana Shonza, si tu unapoteza hadhi ya JF, bali pia unafanya hapa paonekane kijiwe na majungu, sehemu ya watu ambao hawajasoma, lakini pia tunajenga picha mbaya ya elimu mliyoisoma na vyuo vyenu(tunavionea kutokana na madhambi yenu)

MWISHO
Leo mchana Shonza alilalamika kutokupata barua; wewe umeipata wapi? Umeipataje? Maana kama anajificha haonekani na anafanya vurumai, then haitamsaidia kitu. Halafu hata makazini, kama mwajiri hakutaki na amekufukuza kazi, hauwezi ukang'ang'ania ofisi, badala yake unakimbilia CMA ili haki yako ipatikane. Lakini kama hakutaki, no matter what, atakulipa visenti vyako vya miezi 12, unampisha, anaendelea na maisha yake na wafanyakazi wake wengine ambao ni loyal

Cc Molemo Crashwise Ben Saanane Juliana Shonza Mtela Mwampamba, Mchange & Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Nilishaga sema BAVICHA ni mbulula mimi niliona siku nyingi sana na ndio maana nilipokuwa nawakosoa walikuwa wakali sana. tatizo wakiambiwa ukweli wanakuandama mpaka basi. Haya mtafika.
 
hadith haziishi, Mbowe uko wapi? It is time to show your Uenyekiti wako
 
Hahaha kumbe upo bhana weye? Habari za Ofisi Mpya? CCM wanatafuta mtu kwajaili ya kuwa Kampeni Manager
Nilishaga sema BAVICHA ni mbulula mimi niliona siku nyingi sana na ndio maana nilipokuwa nawakosoa walikuwa wakali sana. tatizo wakiambiwa ukweli wanakuandama mpaka basi. Haya mtafika.
 
Nilishaga sema BAVICHA ni mbulula mimi niliona siku nyingi sana na ndio maana nilipokuwa nawakosoa walikuwa wakali sana. tatizo wakiambiwa ukweli wanakuandama mpaka basi. Haya mtafika.
Bado unatamani BAVICHA? NCCR ndiyo penyewe unawataki nini mambulula au na wewe barua yako ina mapungufu? Hambadilishi kitu mmefukuzwa nendeni huko mnakokumbatiwa
 
Nilishaga sema BAVICHA ni mbulula mimi niliona siku nyingi sana na ndio maana nilipokuwa nawakosoa walikuwa wakali sana. tatizo wakiambiwa ukweli wanakuandama mpaka basi. Haya mtafika.
tulia huko nccr manunuzi ya bavicha hayakuhusu...yani we jamaa kwenye siasa huna mvuto kabisa,.
 
Nilishaga sema BAVICHA ni mbulula mimi niliona siku nyingi sana na ndio maana nilipokuwa nawakosoa walikuwa wakali sana. tatizo wakiambiwa ukweli wanakuandama mpaka basi. Haya mtafika.

Mkuu moja ya sababu ya wewe kutoka CHADEMA ni kwa sababu wageni kama wakina Millya na Mawazo wanapewa kazi ya M4C huku wenyeji wakiachwa, so vipi huko NCCR mbona umepigwa cheo fasta? Je ilipinga wasikupe hicho cheo kwa sababu wkuna wenyeji?
 
Mimi sio mwanasiasa na wala sipendi siasa, na dawa ya tatizo sio kuropoka na kujilinda ni kuuangalia ukweli na kujibu hoja,kama wewe una akili timamu na unatetea huo uozo basi sote tuendelee kuamini kuwa hiyo ndiyo BAVICHA

Binafsi namuamini sana Heche ila utata kwenye jina lake unaweza nifanya nibadili msimamo wangu hata kwa chama kwa ujumla kwani inasadikiwa aua imesemwa sana hata nafasi aliyonayo alibebwa sina hakika ,ila chama chenye mategemeo ya watanzania wengi kwa sasa ni CHADEMA na hili halina ubishi lakini CHADEMA imara bila vijana makini ni hatari kwa mustabali sio wa CHADEMA tuu bali hata wa Taifa kwa ujumla.

Ni mawazo yangu tuu sio lazima ujibu
 
Watanzania na ukosefu wa umakini

Unaazimia kumfukuza au umemfukuza?

Mbona mada tajwa na hitimisho halifanan?

Kwa barua hiyo, Shonza hajafukuzwa uanachama
 
Mimi nafikiri inabidi tupate wanaojua kiswahili wasitusaidie kutwambia kama neno kuazimia na neno kudhamiria yana maana sawa.

Nikipata ufafanuzi, then nitarudi kuchangia hoja.

Tiba
 
Nilishaga sema BAVICHA ni mbulula mimi niliona siku nyingi sana na ndio maana nilipokuwa nawakosoa walikuwa wakali sana. tatizo wakiambiwa ukweli wanakuandama mpaka basi. Haya mtafika.

acha kutafuta umaarufu, eti na wewe ulikuwa unataka kugombea urais! Bora kusiwe na rais kuliko wewe uwe rais.
 
Mimi sio mwanasiasa na wala sipendi siasa,na dawa ya tatizo sio kuropoka na kujilinda ni kuuangalia ukweli na kujibu hoja,kama wewe una akili timamu na unatetea huo uozo basi sote tuendelee kuamini kuwa hiyo ndiyo BAVICHA

Binafsi namuamini sana Heche ila utata kwenye jina lake unaweza nifanya nibadili msimamo wangu hata kwa chama kwa ujumla kwani inasadikiwa aua imesemwa sana hata nafasi aliyonayo alibebwa sina hakika ,ila chama chenye mategemeo ya watanzania wengi kwa sasa ni CHADEMA na hili halina ubishi lakini CHADEMA imara bila vijana makini ni hatari kwa mustabali sio wa CHADEMA tuu bali hata wa Taifa kwa ujumla.

Ni mawazo yangu tuu sio lazima ujibu

Mbona unachanganya madawa wewe? Tatizo la John Heche ni hilo jina lake au utendaji wake? Ni kipi kinakufanya utake kupoteza imani naye? Nina wasiwasi na wewe ni mmoja wao!!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom