Barua Kwa Rais Kikwete Toka Tarime

umesahau na kule kwetu sisi wamachinga,tunampenda sana.watu wanasema eti hatujafumbua macho, hivi kweli kufumbua macho ni kule kupotoshwa na wale wajinga wa kuandamana? Kikwete analipa,anakubalika ndani na nje,mtu wa watu.watachonga sana fainali ni 2015. Wasubiri zamu yao.miaka 100 si mingi

Mhhhh! hivi huyu mtanzania unayemuita mjinga ni yupi?, watu wanapigwa risasi lakini bado hawaachi kuandamana kwa ajili ya haki zao, hupati somo bado!!! naomba niishie hapo maana chochote nitakachoandika zaidi ya hapa nitafungiwa tena....kha!!!
 
Kikwete hawezi kukusaidia au kuwasaidia wana Nyamongo. He is part of the problem.
 
umesahau na kule kwetu sisi wamachinga,tunampenda sana.watu wanasema eti hatujafumbua macho, hivi kweli kufumbua macho ni kule kupotoshwa na wale wajinga wa kuandamana? Kikwete analipa,anakubalika ndani na nje,mtu wa watu.watachonga sana fainali ni 2015. Wasubiri zamu yao.miaka 100 si mingi
Huwa najiuliza hivi CCM ikisimamisha mgombea urais mkatoliki 2015 watabaki waislam wangapi wanaokitetea chama cha magamba? Mimi nadhani hata ukiwa na akili za konokono unaweza kuona udhalimu wa serikali ya CCM ikiongozwa na JK! Ndugu zetu hawa hawaoni , wana matatizo gani ya akili? Serikali inayozuia bungeni hoja ya kujadili mauaji yaliyofanywa na polisi wake kwa raia unaiita ni serikali gani ndugu yangu? no wonder mnaishia kufanya kazi za ndani(house girls ) na umachinga! akili zenu ni nyepesi sana kuzi manipulate!!
 
nahisi huyu Malaria sugu ni kati ya nyumba ndogo za jk ndo maana anatetea upuuzi
 
Poleni ndugu zangu wa Mara, tupo pamoja kwani hata sie tulio mbali roho zetu zimesononeka sana kwa yaliyowatokea!

Na ahidi kuendelea kuwa pamoja nanyi huko mbeleni...
 
Mmh! Sidhani, kwa kiasi fulani nilifanya utafiti wangu ktk mikoa kadhaa japo c wakitaalam hasa nikilenga wamama, wengi niliongea nao hawana imani na ccm ila wanaogopa mabadiliko kuhofia vurugu nchin

sugu ni fisadi anayefaidika damu ikimwagika. Wasubiri siku yao watakapokimbia nchi
 
nahisi huyu Malaria sugu ni kati ya nyumba ndogo za jk ndo maana anatetea upuuzi

Hapa ndipo huwa namsifia MS!! Yaani anaweza kuwayumbisha kutoka kwenye maada na kuanza kumjadili yeye na mkaacha maada!! Mtoa maada ametoa maada nzuri tu ya kujadili lakini MS amekuja na utafiti pori na watu mmeanza ku concentrate kwenye kioja chake badala ya hoja. Huyo ndiye MS.
 
Peeeepooooo kabisa! wanamuunga mkono hao majini na mapepo wanaotangaza atakayegombea atakufa halafu wanakufa wenyewe...Chama Cha Mapepo CCM na JK wao. Joka limetupwa duniani na sasa limejivua gamba( sio maneno yangu, CCM wenyewe wamesema wao ni nyoka yaani shetani, ibilisi, lucifer). Someni misahafu halafu mniambie mnasubiri nini CCM!!!!

Limejivua gamba lakini halijajivua sumu...

Nime kukumbuka sana ndugu yangu enzi zile ulikuwa na hasira sana wakati tukifanya harakati za kimapinduzi pale kwenye kilima.......ukombozi hauji kirahisi kinachotakiwa wote wanaojifanya wameenda bungeni kutetea matumbo yao tukianzia na Makinda ni bakora na mawe tu pindi wakipita majimboni kama vile Nyambare Nyan'gwini......Mpaka watakapo ona kazi hii ya ubunge ni zaidi ya kutetea matumbo yao
 
Kazi bado nzito.... (red)
Lengo la MS limetimia (kuwatoa nje ya topic, ili muanze kumshambulia yeye) Msiwe traped kwenye mtego wake; kumbuka kuna wito wa kuput stop to ukandamizaji wa serikali ya magamba by all cost, l agree kufa kwa a better cause is better than kufa kwa njaa!
 


WATZ WENGI BADO WANAMUAMINI JK KAMA NDIO KIMBILIO LAO.
Nimejaribu kufanya uatfiti wa kina . nilipita karibu Mikoa 18 kujua hali ya kisiasa nchini.
Mikoa hiyo ni wazi inamuunga mkono jk kwa kiasi kikubwa.
mikoa michache ambayo imeingia kasumba ya CDM lkn bado mikoa mingi inaimani ya jk kama ndio mkombozi wao
Mikoa inayomuunga mkono kwa asilimia kubwa ni
1)Dar = 90%
2)pwani=99%
3)Morogoro=89%
4)Dodoma=99%
4)Rukwa=90%
5)Tabora=89%
4)iringa=89%
nitawasisha rasmi kwa waandishi wabari kuhusu Utafiti huo hivi karibuni

Acha kudanganya watu na utafiti uchwara, angalia watanzania wenzako wanavyoteseka hapa, bure kabisa wewe huna hata huruma
 
Last edited by a moderator:
WATZ WENGI BADO WANAMUAMINI JK KAMA NDIO KIMBILIO LAO.Nimejaribu kufanya uatfiti wa kina . nilipita karibu Mikoa 18 kujua hali ya kisiasa nchini. Mikoa hiyo ni wazi inamuunga mkono jk kwa kiasi kikubwa. mikoa michache ambayo imeingia kasumba ya CDM lkn bado mikoa mingi inaimani ya jk kama ndio mkombozi waoMikoa inayomuunga mkono kwa asilimia kubwa ni1)Dar = 90%2)pwani=99%3)Morogoro=89%4)Dodoma=99%4)Rukwa=90%5)Tabora=89%4)iringa=89%nitawasisha rasmi kwa waandishi wabari kuhusu Utafiti huo hivi karibuni
we fara, ndio mikoa aliyopata kura nyingi.
 
Habari ya tarime ni kama ujinga ndio unao sumbua....
wana tarime -nyamongo- walijengewa hospitali.!!!..wali iba kila kitu...magodoro mpaka milango...
walichoma moto magari ya kutengeneza barabara...lakini wala hawasemi...
hawa ni walalamikaji...kwa ardhi walio uza wao wenyewe..tena walitapeliana wakati wana uza kwa muwekezaji...madiwani waliwatapeli...
fedha zinazo tolewa na mgodi kila mwaka hutafunwa na viongozi kila mwaka...
Tatizo kubwa la Nyamongo ni elimu..na ukabila...wizi wamifugo... wamepewa nafasi za masomo huwa hawaendi kusoma!!
nikifikiria huwa na kerereka ....
msitumie vifo kutafuta haki...
 
Mh. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete
Nakuandikia nikiamini kwamba umzima wa afya huko Magogogoni st. ukilitumikia Taifa letu kwa Udanganyifu. nimeamua kutumia mtandao kwa maana barua nyingi nilizokutumia hazikufikii kwa maana sijawahi kupata jibu lako, wal sijaona hatua yoyote ikichukuliwa kusuluhisha matatizo yanayotukaili. Kwanza Kabisa napenda kujitambulisha kama Chacha N. Bwire, mkazi wa Nyamongo wilayani Tarime.Mheshimiwa Rais, nikiwa kijana mdogo katika miaka ya 90, familia yangu na nyingine huko nyamongo ilitegemea kilimo, ufugaji pamoja na uchimbaji wa dhaabu ili kujikimu. Tumekuwa kwa furaha hasa kwa kile kidogo tulichokuwa nacho. Tumewasaidia wazazi wetu kazi nyingi za shamba na pia kuchimba dhaabu. Tumesomeshwa na hizi shughuli ndogondogo, na kwa hakika, maisha ya mbeleni yalikuwa na matumaini makubwa

Nikiwa mzalendo na kijana anayeamini ustaarabu katika kutatua matatizo yetu, nimeamua kukuandikia ili kutoa dukuduku langu na pia kutafuta suluhisho la kudumu kuhusiana na matatizo makubwa tunayokabiliana nayo. Takribani miaka sita iliyopita, nyumba yetu, pamoja na mashamba tuliyokuwa nayo yalichukuliwa na serikali. Tulilipwa kiasi cha shilingi million 6. Tukaanza maisha mapya ambayo hatukuyajua. Miaka sita baadae, hali yetu imedorora na kuwa mbaya zaidi. Tumeingia katika bahari ya ufukara na ukiwa. Ng’ombe, wetu wote wamefariki baada ya kunywa maji machafu kutoka katika mto tulioutegemea maisha yetu yote. Shamba tulilolitegemea kwa uchimbaji na kilimo wamepewa BARRICK Gold. Baba yangu, mdogo wangu wa Kike, waliugua ghafla magonjwa ya ajabu iliyofanya ngozi zao kukatika vipande vikubwa vikubwa na kutapika damu kwa wingi na hatimaye kufariki dunia. Mwanangu wa miaka 4, pia tunawasiwasi atakufa hivi karibuni.

Mheshimiwa Rais, wiki chache zilizopita, kaka yangu, ambaye alibaki nguzo ya familia, kutokana na ukiwa na umasikini, aliamua kwenda kuokota mawe kutoka katika shamba letu waliopewa Barrick, akiwa na vijana wenzake wanaokota mawe, walikuja polisi, na kuwaambia waondoke. Kukumbuka ardhi waliyokulia, amepewa mtu mwekezaji, waligoma kuondoka. Hapo ndipo Polisi, ambao inabidi watulinde waliwapiga risasi migongoni na kuwauwa. Matokeo yake wakaitwa majambazi na wahuni. Hapana, kaka yangu hakuwa jambawazi wala muhuni. Alienda kuokota mawe ambayo yalitupwa ili angalau apate chochote

Mh. Rais, sisi siyo ombaomba. Wakurya ni wachapakazi na wakulima hodari. Hatutaki Misaada kutoka kwa mtu. Tatizo letu ni unanyasaji ambao unafanywa na serikali ya Tanzania(yako) kwa niaba ya Barrick Gold. Mh. Rais, nina maswali machache ambayo kama mzalendo, nadhani utaweza kuyashugulikia ikiwa wewe ni mtu mpenda amani
  1. Kwa nini serikali yetu(yako) ituue na kutuita sisi wahuni wakati tunachokitafuta ni kuishi na kulisha watoto wetu? Ndugu zetu hawakuenda kuiba, bali kuokota mawe iliyotupwa na Barrick Gold
  2. Kwa nini tuingie kwenye umasikini zaidi, wakati hapo hawali tulitegemea hii migodi kujikimu?
  3. Wewe kama mzazi, unaweza kukubali wanao kama Khalfani na Ridhiwani kuuwawa wakiokota maembe kwenye shamba lako huko chalinze?
  4. Kwa nini Chama Cha Mapinduzi inazuia Mjadala wa Migodi ya North Mara Bungeni?
  5. Je ni halali huyu mwekezaji kutuachia mashimo ilhali keshachukua mali zetu zote? Haya mashimo tutayafukia vipi?
  6. Utajisikiaje baba yako, kaka yako, na mdogo wako kuuwawa kinyama kwa sababu ya mwekezaji?
  7. Kwa nini mashamba yetu, na dhaabu zetu zitoe ajira kwa wageni (makaburu, wakenya na mataifa mengine) wakati sis wazawa hatukubaliki kwenye hii migodi. Mkenya kachangia nini kwenye mgodi wa North Mara, au mkaburu kwa nini aendeshe trekta?
Mh. Rais, nadhani majibu yako ya haya maswali hayatakuwa mazuri. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu ambao hatuwezi kuukubali. Nakuandikia kwa uchungu mkubwa, na hapa nilipo tayari nimepoteza matumaini. Ya kuishi, kwani kila kitu nilichokitegemea nimenyang’anywa na kukabidhiwa mgeni. Haki yangu ya msingi imeuzwa kwa Barrick gold. Mh. Rais, Ukikumbuka vyema, hakuna binadamu yeyote anayeogopa kufa pale anapokuwa amepoteza matumaini.Wana Tarime hatuogopi kufa, tupo tayari kwa lolote lile. Tunisia, Misri, Libya, Syria, Bharain, na Yemeni ni mifano hai ya watu walipoteza matumaini na kuchoka na uonevu.

Majeshi makubwa yenye nguvu hayawezi kuzuia nguvu ya umma. Ikiwa wewe ni mtu anayeweza kuona mbali, kwa heshima na taadhima, tunakuomba na kukusihi kwa dhati uliokoe taifa la Tanzania pamoja na utawala wako. Tunakuomba ulifunge mgodi wa North Mara na Kusitisha mkataba wa Barrick Gold Tanzania. Hili ni shirika lenye historia mbaya ya unyanyasaji kote duniani. Wanatuibia na mnaona, hawalipi kodi wala kuchangi chochote hapa nchini. kila siku wanasafirisha michanga na ndege na serikali yetu iko kimya, na hata kufikia hatua ya kubisha kwamba muwekezaji hawasafirishi mchanga

Nashukuru kwa kunisikiliza, na pia kuweza kuchukua maamuzi ya haraka kuhusu Barrick Gold, vinginevyo barua yangu uitunze kama kumbukumbu kuashiria mchakato mpya wa kimapinduzi ya aina yake Barani Afrika. Hatutanyamazishwa na bunduki wala mzinga. Tutakufa wote hadi hapo Barrick Watakapooondoka nchini kwetu. Ukizima, maoni yangu, basi utambue kwamba watu million 40 wapo tayari kuchukua hatua ili kuondokana na unyanyasaji. Mapinduzi yanyoendele katika nchi za kiarabu ilianzishwa na kijana mmoja nchini tunisia aliyejitoa mhanga kwa kijiwasha moto akipinga unyanyasaji... Tanzania hali mbaya ya sasa ikiendelea, basi mwisho utakuwa mbaya kwako na serikali yako
Mtiifu,

Chacha N. Bwire
Nyamongo, Tarime
[video=youtube_share;9tSDVM327uo]http://youtu.be/9tSDVM327uo[/video]
Akisoma atacheka cheka tu Pole Chacha Mwita Marwa
 
Nimeumia sana .Poleni sana Nyamongo . Hivi Nyangwine ndiye Mbunge wenu hadi huko au yeye anaishia wapi ? Maana sijasikia anaongelea hili kwani wakati anaomba kula kwenu maana siyo kura alikuwa ana waambia nini kuhusiana na shida zenu ? Au huna mbunge hapo? Poleni sana lakini mambo haya yana madhara mbeleni .
 
Nimeumia sana .Poleni sana Nyamongo . Hivi Nyangwine ndiye Mbunge wenu hadi huko au yeye anaishia wapi ? Maana sijasikia anaongelea hili kwani wakati anaomba kula kwenu maana siyo kura alikuwa ana waambia nini kuhusiana na shida zenu ? Au huna mbunge hapo? Poleni sana lakini mambo haya yana madhara mbeleni .

Nimetokwa na machozi..
 
WATZ WENGI BADO WANAMUAMINI JK KAMA NDIO KIMBILIO LAO.
Nimejaribu kufanya uatfiti wa kina . nilipita karibu Mikoa 18 kujua hali ya kisiasa nchini.
Mikoa hiyo ni wazi inamuunga mkono jk kwa kiasi kikubwa.
mikoa michache ambayo imeingia kasumba ya CDM lkn bado mikoa mingi inaimani ya jk kama ndio mkombozi wao
Mikoa inayomuunga mkono kwa asilimia kubwa ni
1)Dar = 90%
2)pwani=99%
3)Morogoro=89%
4)Dodoma=99%
4)Rukwa=90%
5)Tabora=89%
4)iringa=89%
nitawasisha rasmi kwa waandishi wabari kuhusu Utafiti huo hivi karibuni

Unaweza kuwa shaihi kwakutegemea umemhoji nani. Unafanya utafiti kwa wagogo ambao waliambiwa wakati wa kampeni wasiposhindisha ccm, ccm itaondoka na hela zake na kuwa vyama vingine havitawapa msaada wa chakula na kwa mantiki hiyo njaa ya kila mwaka itawaua! Unatania labda siamini hiyo Dar yenyewe labda kwakuwa uislamu umezagaa sana maeneo hayo na hamasa zao inawezekana kuungwa mkono
 
We unapigia Mbuzi gittar!?

Nakushauri fanya tukio la kujilipua ufe naye huyo unayemwandikia barua maana najua hata isoma wala hata fanya lolote la kukupa matumaini hana uwezo huo na pia hana wakumsaidia kufanya hayo hata kama angekuwa na nia.
 
Back
Top Bottom