Barua Kwa Rais Kikwete Toka Tarime

WATZ WENGI BADO WANAMUAMINI JK KAMA NDIO KIMBILIO LAO.
Nimejaribu kufanya uatfiti wa kina . nilipita karibu Mikoa 18 kujua hali ya kisiasa nchini.
Mikoa hiyo ni wazi inamuunga mkono jk kwa kiasi kikubwa.
mikoa michache ambayo imeingia kasumba ya CDM lkn bado mikoa mingi inaimani ya jk kama ndio mkombozi wao
Mikoa inayomuunga mkono kwa asilimia kubwa ni
1)Dar = 90%
2)pwani=99%
3)Morogoro=89%
4)Dodoma=99%
4)Rukwa=90%
5)Tabora=89%
4)iringa=89%
nitawasisha rasmi kwa waandishi wabari kuhusu Utafiti huo hivi karibuni

Malaria Sugu;
huwa sipendi kumdhihaki mtu wala kumtukana ila ulicho kiongelea hapa ndani si sahihi and I think you were trying to divert the attention ya wachangiaji...sina, uhakika na uhalali wa tafiti zako..ila kama Rais aliweza kupata 82% mwaka 2005 na akaja kupata 62% uchaguzi ulipofuatia huu ni ushahidi wa wazi anakubalka kwa kiasi gani.....Futa tu hizo takwimu zako zisizo na kichwa wala miguu.
 
jaman mwenye contacts za yule makamu wa Osama -somebody -- zawahir anipe, nataka kujitoa muhanga maeneo fulani
 
Tunashukuru sana kwa kututumia hyo documents Bwana Chacha, ni ukweli usiofichika kwamba serikali ya CCm ilipotufikisha ni pabaya mpaka haifai kueleza wala kuangalia. Mi ushauri wangu ningependa kama ingewezekana barua hii pamoja na Video hii itumwe bungeni afu isomwe na mmbunge. Ni vzr pia Video hii iboreshwe na kuuzwa madukani ili kila mwananchi mwenye uwezo wa kuangalia aitazame kisha aamue mwenyewe ni hatua gani achukue. Hatutegemei kwamba Bwana Nyambari kwamba atawewza kuwasaidia raia wa kule Nyamongo kwani hata ukisikia hoja zake ni pumba tupu, yaani sijuui kaingiaje bungeni, CCM imebaki kutetea maslahi ya chama na si kwa ajili ya wananchi. Haiwezekani Tanzania tuishi maisha kama haya, Migodi ni yetu na si ya Mmarekani, na Kikwete. Tumechoka!
 
Kiburi cha ccm mwisho 2015, hao wazee watapukutika karibu wote kwa BP, maana ma retire officers toka wizara na jeshini ndiyo wakuu wa wilaya na mikoa. Wamechoka sana, hawasikilizi shida za watu, wanajali matumbo yao tu! Vijana wanasoma kazi hakuna! Zote zimeshikwa na vibabu vya ccm.
 
We unapigia Mbuzi gittar!?

Nakushauri fanya tukio la kujilipua ufe naye huyo unayemwandikia barua maana najua hata isoma wala hata fanya lolote la kukupa matumaini hana uwezo huo na pia hana wakumsaidia kufanya hayo hata kama angekuwa na nia.

Ngoja tupige gitaa, lakini kila chenche mwanzo kina mwisho. lazima JK asimame mbele ya haki
 
Mbona tabia yenu ya kuvuta bangi Tarime huja mwambia Mheshimiwa Rais ili atatue na tatizo hili linalowasumbua mkivuta bangi basi bangi inawatuma muende kwenye Mgodi! Mwambie Rais na hili la kuvuta Bangi wana Tarime!
 
Kuna mtu amesema we miss mkapa,na kweli we miss him amesain mikataba inayoendelea kuitesa TANZANIA,mkwereee hana cha kufanya hapo,,,,akibadil sheria OBAMA NA WANAMAGHARIB WATAM'BANA
 
Buriani Ndugu yetu Bhoke!!!

Mh. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete
Nakuandikia nikiamini kwamba umzima wa afya huko Magogogoni st. ukilitumikia Taifa letu kwa uadilifu. nimeamua kutumia mtandao kwa maana barua nyingi nilizokutumia hazikufikii kwa maana sijawahi kupata jibu lako, wal sijaona hatua yoyote ikichukuliwa kusuluhisha matatizo yanayotukaili. Kwanza Kabisa napenda kujitambulisha kama Chacha N. Bwire, mkazi wa Nyamongo wilayani Tarime.Mheshimiwa Rais, nikiwa kijana mdogo katika miaka ya 90, familia yangu na nyingine huko nyamongo ilitegemea kilimo, ufugaji pamoja na uchimbaji wa dhaabu ili kujikimu. Tumekuwa kwa furaha hasa kwa kile kidogo tulichokuwa nacho. Tumewasaidia wazazi wetu kazi nyingi za shamba na pia kuchimba dhaabu. Tumesomeshwa na hizi shughuli ndogondogo, na kwa hakika, maisha ya mbeleni yalikuwa na matumaini makubwa

Nikiwa mzalendo na kijana anayeamini ustaarabu katika kutatua matatizo yetu, nimeamua kukuandikia ili kutoa dukuduku langu na pia kutafuta suluhisho la kudumu kuhusiana na matatizo makubwa tunayokabiliana nayo. Takribani miaka sita iliyopita, nyumba yetu, pamoja na mashamba tuliyokuwa nayo yalichukuliwa na serikali. Tulilipwa kiasi cha shilingi million 6. Tukaanza maisha mapya ambayo hatukuyajua. Miaka sita baadae, hali yetu imedorora na kuwa mbaya zaidi. Tumeingia katika bahari ya ufukara na ukiwa. Ng’ombe, wetu wote wamefariki baada ya kunywa maji machafu kutoka katika mto tulioutegemea maisha yetu yote. Shamba tulilolitegemea kwa uchimbaji na kilimo wamepewa BARRICK Gold. Baba yangu, mdogo wangu wa Kike, waliugua ghafla magonjwa ya ajabu iliyofanya ngozi zao kukatika vipande vikubwa vikubwa na kutapika damu kwa wingi na hatimaye kufariki dunia. Mwanangu wa miaka 4, pia tunawasiwasi atakufa hivi karibuni.

Mheshimiwa Rais, wiki chache zilizopita, kaka yangu, ambaye alibaki nguzo ya familia, kutokana na ukiwa na umasikini, aliamua kwenda kuokota mawe kutoka katika shamba letu waliopewa Barrick, akiwa na vijana wenzake wanaokota mawe, walikuja polisi, na kuwaambia waondoke. Kukumbuka ardhi waliyokulia, amepewa mtu mwekezaji, waligoma kuondoka. Hapo ndipo Polisi, ambao inabidi watulinde waliwapiga risasi migongoni na kuwauwa. Matokeo yake wakaitwa majambazi na wahuni. Hapana, kaka yangu hakuwa jambawazi wala muhuni. Alienda kuokota mawe ambayo yalitupwa ili angalau apate chochote

Mh. Rais, sisi siyo ombaomba. Wakurya ni wachapakazi na wakulima hodari. Hatutaki Misaadi kutoka kwa mtu. Tatizo letu ni unanyasaji ambao unafanywa na serikali ya Tanzania kwa niaba ya Barrick Gold. Mh. Rais, nina maswali machache ambayo kama mzalendo, nadhani utaweza kuyashugulikia ikiwa wewe ni mtu mpenda amani

  1. Kwa nini serikali yetu ituue na kutuita sisi wahuni wakati tunachokitafuta ni kuishi na kulisha watoto wetu? Ndugu zetu hawakuenda kuiba, bali kuokota mawe iliyotupwa na Barrick Gold
  2. Kwa nini tuingie kwenye umasikini zaidi, wakati hapo hawali tulitegemea hii migodi kujikimu?
  3. Wewe kama mzazi, unaweza kukubali wanao kama Khalfani na Ridhiwani kuuwawa wakiokota maembe kwenye shamba lako huko chalinze?
  4. Kwa nini Chama Cha Mapinduzi inazuia Mjadala wa Migodi ya Nroth Mara Bungeni?
  5. Je ni halali huyu mwekezaji kutuachia mashimo ilhali keshachukua mali zetu zote? Haya mashimo tutayafukia vipi?
  6. Utajisikiaje baba yako, kaka yako, na mdogo wako kuuwawa kinyama kwa sababu ya mwekezaji?
  7. Kwa nini mashamba yetu, na dhaabu zetu zitoe ajira kwa wageni (makaburu, wakenya na mataifa mengine) wakati sis wazawa hatukubaliki kwenye hii migodi. Mkenya kachangia nini kwenye mgodi wa North Mara, au mkaburu kwa nini aendeshe trekta?
Mh. Rais, nadhani majibu yako ya haya maswali hayatakuwa mazuri. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu ambao hatuwezi kuukubali. Nakuandikia kwa uchungu mkubwa, na hapa nilipo tayari nimepoteza matumaini. Ya kuishi, kwani kila kitu nilichokitegemea nimenyang’anywa na kukabidhiwa mgeni. Haki yangu ya msingi imeuzwa kwa Barrick gold. Mh. Rais, Ukikumbuka vyema, hakuna binadamu yeyote anayeogopa kufa pale anapokuwa amepoteza matumaini.Wana Tarime hatuogopi kufa, tupo tayari kwa lolote lile. Tunisia, Misri, Libya, Syria, Bharain, na Yemeni ni mifano hai ya watu walipoteza matumaini na kuchoka na uonevu.

Majeshi makubwa yenye nguvu hayawezi kuzuia nguvu ya umma. Ikiwa wewe ni mtu anayeweza kuona mbali, kwa heshima na taadhima, tunakuomba na kukusihi kwa dhati uliokoe taifa la Tanzania pamoja na utawala wako. Tunakuomba ulifunge mgodi wa North Mara na Kusitisha mkataba wa Barrick Gold Tanzania. Hili ni shirika lenye historia mbaya ya unyanyasaji kote duniani. Wanatuibia na mnaona, hawalipi kodi wala kuchangi chochote hapa nchini. kila siku wanasafirisha michanga na ndege na serikali yetu iko kimya, na hata kufikia hatua ya kubisha kwamba muwekezaji hawasafirishi mchanga

Nashukuru kwa kunisikiliza, na pia kuweza kuchukua maamuzi ya haraka kuhusu Barrick Gold, vinginevyo barua yangu uitunze kama kumbukumbu kuashiria mchakato mpya wa kimapinduzi ya aina yake Barani Afrika. Hatutanyamazishwa na bunduki wala mzinga. Tutakufa wote hadi hapo Barrick Watakapooondoka nchini kwetu. Ukizima, maoni yangu, basi utambue kwamba watu million 40 wapo tayari kuchukua hatua ili kuondokana na unyanyasaji. Mapinduzi yanyoendele katika nchi za kiarabu ilianzishwa na kijana mmoja nchini tunisia aliyejitoa mhanga kwa kijiwasha moto akipinga unyanyasaji... Tanzania hali mbaya ya sasa ikiendelea, basi mwisho utakuwa mbaya kwako na serikali yako
Mtiifu,

Chacha N. Bwire
Nyamongo, Tarime
[video=youtube_share;9tSDVM327uo]http://youtu.be/9tSDVM327uo[/video]
 
Pole sana!hii ndo Tanzania bana!

Utapewa majibu yafuatayo:

1.unafanya uchochezi na umetumwa na viongozi wa chadema.

2.hilo suala la nyamongo limeundiwa tume na tunasubiri matokeo ya tume.

3.kwa ari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi nitahakikisha wananchi wanafaidika na rasilimali zilizopo nchini.

4.nawashauri wananchi wa tarime muwe wavumilivu na mpunguze jazba na viburi kwa askari kwani wao wanatekeleza maagizo ya serikali.hvyo mkiwafanyia kiburi mtakufa sana.ukiambiwa acha au ondoka eneo fulani uondoke.

5.nina mpango wa kutoa mabilioni mengine(mabilioni ya kikwete)vijana mkopeshwe na muwe wajasiliamali.

6.mwisho kabisa nasisitiza serikali ya ccm ni sikivu na ipn kwa ajili ya kuboresha maisha ya kila mtanzania.!
Ccm oyee!
 
Poleni wana tarime, ikibidi tunawaunga mkono kwa madai yenu.
Hivi hii nchi ni ya kidemokrasia kweli?
Kama ni huvyo mbona ni hatari jamani. Yaani tunashindwa kujaliana watanzania wenyewe na kuwajali wageni?

 
Kuna mtu amesema we miss mkapa,na kweli we miss him amesain mikataba inayoendelea kuitesa TANZANIA,mkwereee hana cha kufanya hapo,,,,akibadil sheria OBAMA NA WANAMAGHARIB WATAM'BANA
angekua soni japo kidogo jk asinge ruhusu mikataba mingine ya kinyonyaji kusainiwa
 
@mmingereza

taarifa za ndani ya ikulu zinaonyesha baada ya unyanyasaji huo walikupa nafasi ya upendeleo kwenda Marekani, kama sehemu ya fidia na kujikimu. tunaomba mwongozo wako
 
mbeya, mwanza, arusha wameweza kwanini tushindwe

raha moja wote hawa wanafanya vurugu kudai maslahi yao..na kama umewasikia wote wanaomba serikali yetu iwasaidie.
Nakubaliana sana na MS, raisi JK amekuwa tumain kubwa sana kwa wananchi hasa waliokataa tamaa na maisha. Nimekuwa nikitembea na mh kwenye mikoa mbali mbali na hili nimelishuhudia.
 
guys... Hevbu tumuweke ms kwenye ignore list ili tujadili barua ya tarime
 
WATZ WENGI BADO WANAMUAMINI JK KAMA NDIO KIMBILIO LAO.
Nimejaribu kufanya uatfiti wa kina . nilipita karibu Mikoa 18 kujua hali ya kisiasa nchini.
Mikoa hiyo ni wazi inamuunga mkono jk kwa kiasi kikubwa.
mikoa michache ambayo imeingia kasumba ya CDM lkn bado mikoa mingi inaimani ya jk kama ndio mkombozi wao
Mikoa inayomuunga mkono kwa asilimia kubwa ni
1)Dar = 90%
2)pwani=99%
3)Morogoro=89%
4)Dodoma=99%
4)Rukwa=90%
5)Tabora=89%
4)iringa=89%
nitawasisha rasmi kwa waandishi wabari kuhusu Utafiti huo hivi karibuni


Huo utakuwa mfumuko wa bei na kupanda kwa bidhaa hebu kaangalie upya tena. Kama bidhaa zimeweza kupanda kwa asilimia 99 basi baada ya miezi mitatu ita kuwa zaidi ya 100%
 
Back
Top Bottom