Barua kwa Dr. W. Slaa

luten ni ushauri mzuri sana.Naamini CDM kuna wasomi wengi wa watu wenye mapenzi na chama pia na wazee wenye busara.maamuzi yoyote watakayo fanya naamini yatakuwa sahii.Hata kama Lewa akiwekewa pingamizi la kutogombea anaweza gombea Slaa.naanini SLaa na Lema wanavaliana viatu,Lema anaweza fanya kazi anayofanya Dr sasaivi ya kujenga chama, natumaini ni wakati mzuri sasa kwa vijana kuanza kujitetgemea na kujifunza.ndani ya chaaaadema kila mtu ni jembe.chadema ilinza na Mungu na tutakuwa na Mungu siku zote.KUMPIGA CHURA TEKE NI KUMUONGNEZEA SPEED.PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS.......................
 
Nakubaliana na maneno yako, kwani kuweka vifungu viwili kwenye hukumu moja ni mtego kwa CDM. Please CDM tuweni makini
 
Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.

Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.

Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?

Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?

Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.

CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.

Mkuu naona unijibu endapo CDM itakata rufaa Lema ataendelea kuwa mbunge au jimbo litakuwa halina mbunge mpaka hukumu iamuliwe?
 
Najua shukrani zako zimejikita katika kulikomboa jimbo. Mnadhani Lema peke yake ndiyo tishio Arusha.
Kwa taarifa yako hata Mbwa akipewa bendera ya CDM akasimama na Jk mbwa anashinda.
Arusha wanaiona ccm kama Shetani
Tunashukuru luteni kwa barua yako yenye maneno murua...
 
kama hata kata rufaa?je kifungu hicho kilichotumika kinamzui kugombea ubunge tu au ni pamoja na mambo ya kisiasa?jamani ile hukumu ni balaa kwa Lema kwa kweli.
 
Nasema tena na tena ,giza huwa nene zaidi kabla ya mapambazuko.Saa hii tutazungumza sana kwa sababu tunamhemko na hukumu ya kipuuzi iliyotolewa dhidi ya kamanda lema ,Lakini ni tumaini langu na makamanda wenzangu kwamba kutapambazuka .Hatuna budi kuamini kwamba njia ya kutupatia haki itapatikana tena sio mbali ni hapo jumamosi,Amri jeshi mkuu mbowe atasema ,jipeni moyo konde ndg zangu .
 
Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.

Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.

Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?

Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?

Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.

CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.

Spanner kwa Luteni hiyo haiwezekani..... nadhani hujui track record yake, anaweza kuwa katoa ushauri ambao wewe hukubaliani nao , lakini hili la kutumwa NO!
 
Ndugu Slaa,
Kwanza niruhusu nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwako binafsi na kwa chama chako cha CHADEMA kwa mafanikio mliyoyapata kwa kipindi kifupi. Natambua kazi mnayoifanya ni nzito na ya hatari maana wengi wanatamani kuwa kama ninyi lakini wanaogopa kutangulia ila nyie mmesema mnatangulia wengine watawakuta mbele ya safari. Kwa hilo hongera sana.

Bila kupoteza muda kutaja mafanikio mliyoyapata naomba nijikite moja kwa moja kwenye kiini cha barua hii.

Kabla sijasahau naomba chama kisikate rufaa kwa kesi ya Lema.

Naomba nikukumbushe tu kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 CCM hawakutaka si tu nyie mshinde bali msiongeze wabunge wa kuchaguliwa. Utakumbuka matamshi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba alipowaambia wanachama wa CCM kwenda kutafuta sababu yeyote ile wafungue kesi kupinga ushindi wa wabunge wa Chadema na chama kitagharamia kesi? Yanayotokea sasa ni utekelezaji tumjiandae kwa makubwa.

Utekelezaji wa hukumu ya Lema ni mwanzo tu ya mipango mingi ya CCM kuihujumu Chadema. Mpango ulikuwa trh 1-4 washinde Arumeru Mashariki halafu trh 5-4 ushindi wa Lema utenguliwe na sherehe kubwa yakupongezana ilikuwa ifanyike weekend hii mjini Arusha. Najua hilo limeshindikana.

Hukumu ya kupinga ushindi wa Lema si kwamba Jaji kajichanganya ni mtego wa makusudi ili nyie mjichanganye waendelee na plan B,C. Lengo lao ni kuikamata Arusha kwa hali yeyote kwa vile wanajua fika hawawezi kuikamata kwa kutumia sanduku la kura, kwa hiyo njia iliyobaki ni kutumia mahakama na pingamizi. Narudia tena msikate rufaa.

Lema amehukumiwa kwa kifungu 108 ‘Illegal Campaign’ kinachomruhusu kugombea lakini kwenye majumuisho ya hukumu imeandikwa kahukumiwa kwa kifungu 114 “Illegal Practice” kinachomuzuia kugombea kwa miaka 5. Wanataka mkate rufaa au muombe ku review case na hapo itacheleweshwa mwisho mtaambiwa muda ni mfupi wa kuitisha uchaguzi.

CCM imeanza kuhaha baada ya kuona hamna mpango wa kukata rufaa, wanachosubiri ni Lema ateuliwe kugombea wamuwekee pingamizi, believe me or not lazima ataondolewa hata kama mtakuwa na hukumu mkononi.

Ndugu Slaa, CCM wameshafanya kosa wanajishauri endapo waingie kwenye uchaguzi ama la. Ushauri wangu ni kuwa, whatever the case, nendeni kwenye uchaguzi hata kama Lema hatogombea najua mtapata mgombea mwingine makini. Kama chama kitaona Lema asigombee, apewe kazi makao makuu ya kukiimarisha chama, akusaidie kuzunguka nchi nzima hasa katika kuimarisha matawi tayari kwa uchaguzi wa ndani na wa serikali za mitaa.

Nawatakia mafanikio mema katika ukombozi, najua kadritaabu zinavyozidi ndivyo ukombozi unavyokaribia.

Luteni.

Big up man, This is a greater thinking, CDM watch out. Kwahaya unabashiri kwamba hata Meatu na singida ndo hayo hayo?
 
Luten Mungu akubariki na bila shaka Dr Slaa atapita hapa.
Lakini suala hili kunatakiwa kufanyike kitu ili serkali ijifunze, tunasubiri busara za viongozi wa cdm
Ili serikali ijifunze CDM inatakiwa ishinde uchaguzi wa marudio kwa kishindo, itatoa funzo kuwa mbunge ni chaguo la wananchi si la mahakama.
 
Mimi sio mwanasheria ila ni gwiji wa mchezo wa CHESS! Luteni ana-predict two moves za mpinzani wake (wetu)! LAKINI counter attack yake inampa adui muda mrefu wa kufikiri...LUTENI NA PASCO peanieni contacts za kweli then do something!
 
Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.

Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.

Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?

Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?

Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.

CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.
SPANNER

Si wote tuko hivyo wengine ni ma-independent thinkers.
 
Kushindwa huanza na hofu, haraka ya nini? Rufaa ikatwe, mahakama iamue upya, c majaji wote ni wahuni, pili c lema, ni Zaidi ya lema, kesi mahakamani ni mapambano mengine muhimu dhidi ya mhimili huu wa dola, mandela alikaa gerezani Zaidi ya 20yrs na akaingia ikulu, marando, safari, na lisu simamieni rufaa ikatwe. Tuache hisia, Kama jaji. Kajichanganya ni jukumu la cdm kuweka sawa.
 
Mkuu Luteni naunga mkono ushauri wako wa CDM kisikate rufaa na kita liretain jimbo la Arusha kwa kishindo kikubwa kuliko 2010.

Lakini kwa vile Chadema ni chama cha kutetea haki, na ile hukumu sio hukumu ya haki kisheria, nashauri Chadema wafanye yafuatayo.

1. Kwanza Chadema iombe expert legal opinion toka kwa wanasheria nguli na mahiri.
2.Kuangalia uwezekano wa kuomba "Stay Off Excecution Order" toka mahakama ya juu wakionyesha intention ya kukata rufaa hivyo mahakama ya juu itatoa "stay order" kwa Lema kuendelea kuwa mbunge mpaka baada ya rufaa yake kusikilizwa!.
3. Kinachotakiwa ni kutumia nguvu za hoja kupata hiyo "Stay Order" na sio hoja za nguvu!.
4. Wakijiridhisha kuwa hili la stay order haliwezekani ndipo waamue wasikate rufaa na wasimsimamishe Lema!. Nimemsikia mkazi wa Arusha akisema hata CCM ingemsimamisha JK mwenyewe na Chadema wakasimamisha jiwe, jiwe litashinda!.

Pasco
Mkuu Pasco hizo zote ni court proceedings ambazo ndio mtego wenyewe, kama CDM wanauhakika wa kushinda kwanini wampe mpinzani wao muda wa kujipanga? Halafu using common sense kama unajua hii njia ni hatari kwanini uitumie?
 
Kaka mimi nimekukubali kwa analysis yako, najua una uelewa wa sheria kwa kiasi fulani ambao mimi sina, lakini nakubaliana na wewe kwamba lema akionekana kuna vifungu vya sheria vinavyombana basi afanye kazi za chama kitaifa zaidi na aendelee kuhamasisha na kutia moyo wananchi kuwa ukombozi wao upo karibu, na kwa wakati huohuo, chama kiteue mtu mwingine ambaye kwa namna yoyote ile atashinda hapo ccm watakuwa wameaibika zaidi na lema ataendelea kuwa mwiba kwao kwa kufungua matawi kila kona ya nchi.
 
Back
Top Bottom