Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Na Salim Said Salim
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, anasema baraza lina wajumbe wengi kupindukia.
Anaona haiwezekani libaki hivyo; akiwa na maana kwamba inafaa wapungue.
Kupunguza ukubwa wa baraza ni wazo la zamani ambalo halikupata kusikilizwa kwa uzito uliostahili. Labda kwa sababu halikutolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kauli ya Spika inaonyesha ameanza kufikiri kwa maslahi ya nchi si itikadi za chama cha siasa. Kwa hatua hii mpya, anastahili pongezi.
Nionavyo, ukubwa wa Baraza unatokana zaidi na mfumo wa uteuzi. Kumpa rais madaraka ya kuteua wajumbe kunatumika vibaya.
Fursa hiyo ya kikatiba, imempa mwanya kuteua bila ya kuzingatia vigezo muhimu. Badala yake, huteua kwa hisani.
Rais wa Zanzibar aweza kuteua watu 10 kuwa wajumbe wa baraza la wawakilishi. Hao ni mbali na wakuu wa mikoa mitatu Unguja na miwili ya Pemba ambao huingia moja kwa moja barazani, utaratibu ambao umefutwa bungeni.
Baadhi ya wakuu wa mikoa waliomo bungeni waliteuliwa baada ya kuwa ni wabunge tayari waliochaguliwa na wananchi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayeteuliwa na Rais, naye ni mjumbe kwa wadhifa. Ukijumlisha wajumbe wanawake wanaoingia kwa utaratibu wa Viti Maalum, unakuta zaidi ya asilimia 40 ya wajumbe hawakuchaguliwa na wananchi.
Kumekuwa na minong'ono kuwa zile nafasi 10 anazopewa Rais kuteua, zinatumika kuzawadia watu ambao ana mahusiano ya damu nao au kisiasa.
Wenzetu kama Sweden na Denmark, nafasi kama hizo huwekewa masharti ili kuzuia kutumika vibaya.
Kwa kuwa Baraza linahitaji watu werevu na weledi wa mambo, si vibaya, kwa mfano, rais akateua mtu kutoka chama cha upinzani.
Au akaangalia makundi maalum katika jamii. Akipata mtu anayeheshimika na kuaminika, anaweza kumteua japo hatoki chama chake.
Wakati Benjamin Mkapa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, alimteua Hamad Rashid Mohamed wa Chama cha Wananchi (CUF) kama mmoja wa wabunge 10 wa uteuzi.
Hamad alikosoa serikali ya Mkapa na alishauri pale alipoamini ni muhimu. Mchango wake unajulikana nchi nzima hata sasa akiwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
Ni vizuri katiba ikabainisha vigezo vya kielimu au jinsia. Kwanza nafasi za uteuzi zingekatwa na kubaki sita kutoka kumi. Ni vuziri azuiwe kuteua ndugu au rafiki na azingatie jinsia.
Rais anaporuhusiwa kuteua atakavyo, si ajabu kuteua hawara, ndugu na rafiki aliyesoma naye au kucheza naye utotoni. Hataweza kumdhibiti au mteuliwa mwenyewe hatamkosoa rais.
Katiba inaweza kusema kutokana na wale anaoteua, labda mawili tu ndio wawe mawaziri na ikiwa hivyo, basi wasishike wizara fulani, kwa mfano ya fedha, mambo ya ndani na biashara.
Inafaa pia wale wanaoteuliwa, wathibitishwe na baraza ili kuepuka baraza kuwa na watu wachafu kimaadili. Wakati wa uongozi wa Dk. Salmin Amour Juma, asilimia 60 ya mawaziri walikuwa wateule wa rais. Sura halisi barazani, ilikuwa "Baraza la Rais" badala ya Baraza la Wawakilishi.
Ni vyema pia wakuu wa mikoa wakabaki watendaji wakuu mikoani badala ya kuingizwa barazani.
Muda wanaokaa barazani ungeleta tija iwapo ungetumika kwa kutatua matatizo ya wananchi na kuhamasisha shughuli za maendeleo vijijini.
Kupunguza ukubwa wa baraza lazima kwende na kupunguza viongozi katika serikali.
Serikali iliyopo chini ya Rais Amani Abeid Karume, ni kubwa mno kiasi cha kuwa mzigo kwa walipa kodi na haileti ufanisi.
Rais ameteua mawaziri wengi; bado ana washauri katika masuala mbalimbali. Ajabu ni kuteua waziri wa kilimo na naibu wake, huku akiwa na mshauri wa masuala hayohayo.
Utafiti uliofanywa mwaka juzi na wataalamu wa Uingereza ulionyesha utendaji SMZ hautaathirika hata kama mawaziri na watendaji wakuu watapunguzwa kwa thuluthi moja. Spika Kificho amefichulia umma fikra pevu. Muhimu zijadiliwe kwa nia nzuri siyo kunufaisha watu wachache au chama cha siasa.
SOURCE: MWANAHALISI