Baraza La Wawakilishi Lipunguzwe: Spika Kificho

Mzalendohalisi,Mwanafalsafa1,

..ninavyoelewa ktk majimbo kuna serikali na bunge la kila jimbo. ndiyo mfumo wanaofuata Nigeria, USA etc ambako kuna majimbo.

..halafu tena kuna bunge la nchi nzima, nalo hujumuisha wabunge toka constituencies zilezile zilizoko ktk mabunge ya majimbo. sidhani kama wabunge wa majimbo huwa ndiyo hao hao wanakwenda kuingia ktk bunge kuu.

..pia unakuta kuna mawaziri wa majimbo, na tena kunakuwa na majeshi,polisi,mahakama za majimbo, na makorokoro mengine, na juu ya hao wote kuna federal government and its agencies.

..sasa nadhani hizo ni gharama kubwa sana.


Mkuu Jokakuu, gharama haitaongezeka significantly...

Kwa kuangalia mfano wa USA, tunaweza kwanza kuangalia idadi ya wabunge wetu in proportion to the population. Kwa TZ katika miaka 20 iliyopita idadi ya wabunge imeongezeka sana, na hii imeongeza gharama, hivyo idadi yao inatakiwa ipunguzwe ili kupunguza gharama. Jumla wabaki kati ya 100 hadi 150.

Kuhusu Polisi, kunaweza kuwa na Polisi wa majimbo na mkuu wao (mfano kama RPC) anayewajibika kwa mkuu wa jimbo(mfano Governor in US).
Mahakama zinakuwepo za majimbo (mfano zile za Resident Magistrates au hata High Courts) na pia kunakuwa na Court of Appeal ya nchi nzima.

Hiyo ya majimbo itafuta Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, hivyo gharama zitahamishwa tu. Watendaji mfano District Executive Directors watabaki tu, hao wana kazi muhimu za kufanya.

Kunaweza kuwa na mabaraza ya wawakilishi ndani ya majimbo, wawakilishi kama 20 hivi (mabunge madogo ya majimbo. Hayaongezi gharama kwani yatachukua nafasi ya madiwani)

Muhimu:
Wakuu wa majimbo wachaguliwe kwa kura na wakazi wa majimbo husika. Na hata wasio wanachama wa vyama vya siasa pia waruhusiwe kugombea, vinginevyo vyama vinaweza kuwabania wale wanaopendwa na wananchi wa kawaida.
Hii itafanya wakichaguliwa wawajibike kwa wananchi wao, tofauti na sasa ambapo wakuu wa mikoa na wilaya wanawajibika kwa anayewateua, yaani Rais.

Kuhusu Zanzibar, kunaweza kuwa na jimbo la Unguja na jimbo la Pemba. Muhimu ni Pemba kuwa na maamuzi yake kama jimbo kamili.
 
Back
Top Bottom