Baraza La Wawakilishi Lipunguzwe: Spika Kificho

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Na Salim Said Salim

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, anasema baraza lina wajumbe wengi kupindukia.

Anaona haiwezekani libaki hivyo; akiwa na maana kwamba inafaa wapungue.

Kupunguza ukubwa wa baraza ni wazo la zamani ambalo halikupata kusikilizwa kwa uzito uliostahili. Labda kwa sababu halikutolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kauli ya Spika inaonyesha ameanza kufikiri kwa maslahi ya nchi si itikadi za chama cha siasa. Kwa hatua hii mpya, anastahili pongezi.

Nionavyo, ukubwa wa Baraza unatokana zaidi na mfumo wa uteuzi. Kumpa rais madaraka ya kuteua wajumbe kunatumika vibaya.

Fursa hiyo ya kikatiba, imempa mwanya kuteua bila ya kuzingatia vigezo muhimu. Badala yake, huteua kwa hisani.

Rais wa Zanzibar aweza kuteua watu 10 kuwa wajumbe wa baraza la wawakilishi. Hao ni mbali na wakuu wa mikoa – mitatu Unguja na miwili ya Pemba – ambao huingia moja kwa moja barazani, utaratibu ambao umefutwa bungeni.

Baadhi ya wakuu wa mikoa waliomo bungeni waliteuliwa baada ya kuwa ni wabunge tayari waliochaguliwa na wananchi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayeteuliwa na Rais, naye ni mjumbe kwa wadhifa. Ukijumlisha wajumbe wanawake wanaoingia kwa utaratibu wa Viti Maalum, unakuta zaidi ya asilimia 40 ya wajumbe hawakuchaguliwa na wananchi.

Kumekuwa na minong'ono kuwa zile nafasi 10 anazopewa Rais kuteua, zinatumika kuzawadia watu ambao ana mahusiano ya damu nao au kisiasa.
Wenzetu kama Sweden na Denmark, nafasi kama hizo huwekewa masharti ili kuzuia kutumika vibaya.

Kwa kuwa Baraza linahitaji watu werevu na weledi wa mambo, si vibaya, kwa mfano, rais akateua mtu kutoka chama cha upinzani.

Au akaangalia makundi maalum katika jamii. Akipata mtu anayeheshimika na kuaminika, anaweza kumteua japo hatoki chama chake.

Wakati Benjamin Mkapa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, alimteua Hamad Rashid Mohamed wa Chama cha Wananchi (CUF) kama mmoja wa wabunge 10 wa uteuzi.

Hamad alikosoa serikali ya Mkapa na alishauri pale alipoamini ni muhimu. Mchango wake unajulikana nchi nzima hata sasa akiwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

Ni vizuri katiba ikabainisha vigezo vya kielimu au jinsia. Kwanza nafasi za uteuzi zingekatwa na kubaki sita kutoka kumi. Ni vuziri azuiwe kuteua ndugu au rafiki na azingatie jinsia.

Rais anaporuhusiwa kuteua atakavyo, si ajabu kuteua hawara, ndugu na rafiki aliyesoma naye au kucheza naye utotoni. Hataweza kumdhibiti au mteuliwa mwenyewe hatamkosoa rais.

Katiba inaweza kusema kutokana na wale anaoteua, labda mawili tu ndio wawe mawaziri na ikiwa hivyo, basi wasishike wizara fulani, kwa mfano ya fedha, mambo ya ndani na biashara.

Inafaa pia wale wanaoteuliwa, wathibitishwe na baraza ili kuepuka baraza kuwa na watu wachafu kimaadili. Wakati wa uongozi wa Dk. Salmin Amour Juma, asilimia 60 ya mawaziri walikuwa wateule wa rais. Sura halisi barazani, ilikuwa "Baraza la Rais" badala ya Baraza la Wawakilishi.

Ni vyema pia wakuu wa mikoa wakabaki watendaji wakuu mikoani badala ya kuingizwa barazani.

Muda wanaokaa barazani ungeleta tija iwapo ungetumika kwa kutatua matatizo ya wananchi na kuhamasisha shughuli za maendeleo vijijini.
Kupunguza ukubwa wa baraza lazima kwende na kupunguza viongozi katika serikali.

Serikali iliyopo chini ya Rais Amani Abeid Karume, ni kubwa mno kiasi cha kuwa mzigo kwa walipa kodi na haileti ufanisi.

Rais ameteua mawaziri wengi; bado ana washauri katika masuala mbalimbali. Ajabu ni kuteua waziri wa kilimo na naibu wake, huku akiwa na mshauri wa masuala hayohayo.

Utafiti uliofanywa mwaka juzi na wataalamu wa Uingereza ulionyesha utendaji SMZ hautaathirika hata kama mawaziri na watendaji wakuu watapunguzwa kwa thuluthi moja. Spika Kificho amefichulia umma fikra pevu. Muhimu zijadiliwe kwa nia nzuri siyo kunufaisha watu wachache au chama cha siasa.

SOURCE: MWANAHALISI
 
Nimtazamo chanya na fikra nzuri. Sasa tusikie vyama vitasemaje? SMZ itajibu vipi? kwani hapo ni lazima BLW lipitishe sheria na BMZ wapitishe.
 
..hata mimi hili nimeliona.

..nadhani idadi ya wawakilishi sasa hivi ni almost three times ya waliokuwepo kabla ya Mapinduzi.

..hapo bado hujaongeza wabunge wanaowakilisha ktk bunge la muungano.

..sijui sababu yake ni nini haswa. Zanzibar haijaongezeka eneo, na mawasiliano naamini yamekuwa bora na ya kisasa kuliko kabla ya mapinduzi.

..huu ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi wa Zanzibar.
 
Visiwani karibu kila mtu ni mwanasiasi au mtawala

Watu ni 1 milioni- angalia Raisi, Mawaziri-SMZ na SMT, Wabunge Muungano, wawakilishi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Masheha, Makatibu wakuu wa Wizara, Wakurugenzi!!! n.k

Sasa hapo niambie nani aliyebaki wa kumfanyia kazi mwingine ktk nchi ndogo hivi?
 
Simple solution but which is complicated by some........wekeni serikali moja tu. Mkisha amua kua na serikali moja then iangaliwe upya allocation za uongozi kama vile idadi ya wabunge nk.Mtazamo wangu tu....mnaotaka serikali mbili au tatu msikasirike.
 
MwanaFalsafa1,

..ni rahisi sana kutamka tuwe na serikali moja.

..tatizo ni kwamba hiyo serikali moja tunayotaka kuiunda ni muunganiko wa serikali mbili toka maeneo ambayo ni extremely dispropotional in terms of area and population.

..nafasi ya Zanzibar ktk muundo wa serikali moja itakuwa ni nini? je, itakuwa wilaya au mkoa, au jimbo[ this is a different discussion].

..binafsi nadhani tuachane na muungano wa kisiasa badala yake tuwe na bilateral agreements kwenye masuala kama biashara, ulinzi, uvuvi etc.
 
MwanaFalsafa1 na Jokakuu!

1. May be wazo la majimbo Tz..na Visiwani wakawa na serikali yao ya Jimbo..na kuwe na Fed. Government kama Afrika Kusini! Je Visiwani watakubali? Pia siyo fair kwa bara watu 40m kuwa na usawa na Visiwani ambao ni milioni 1. Angalia tu Bunge..tuna wabunge 320 hati ya hawa 50 wanatoka Visiwani na wanawakilisha tu watu 1m!

2.Hivi lile wazo la Majimbo limeishia wapi?? Maana hii habari ya Raisi kuteua Wakuu wa Mikoa/Wilaya kiswahiba je ni tija kwa nchi?? Niambieni mtu toka Mtwara akateuliwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ataona uchungu gani kwa Wanarukwa wakati anaweza kuhamishwa wakati wowote?? Au basi Mkuu wa Mkoa/Wilaya atoke shemu hiyo hiyo na achaguliwe na watu kama madiwani!
 
Mzalendohalisi,

..wengi wanaopinga Majimbo wanadai yatarudisha ukabila.

..pia sijui gharama za kuendesha serikali za majimbo zitakuwa kiasi gani. nina wasiwasi zitaongeza mzigo kwa walipa kodi wa Tanganyika.
 
MwanaFalsafa1,

..ni rahisi sana kutamka tuwe na serikali moja.

..tatizo ni kwamba hiyo serikali moja tunayotaka kuiunda ni muunganiko wa serikali mbili toka maeneo ambayo ni extremely dispropotional in terms of area and population.

..nafasi ya Zanzibar ktk muundo wa serikali moja itakuwa ni nini? je, itakuwa wilaya au mkoa, au jimbo[ this is a different discussion].

..binafsi nadhani tuachane na muungano wa kisiasa badala yake tuwe na bilateral agreements kwenye masuala kama biashara, ulinzi, uvuvi etc.

Nadhani tatizo linakuja kwenye compromising. No one wants to compromise.
 
Mzalendohalisi,

..wengi wanaopinga Majimbo wanadai yatarudisha ukabila.

..pia sijui gharama za kuendesha serikali za majimbo zitakuwa kiasi gani. nina wasiwasi zitaongeza mzigo kwa walipa kodi wa Tanganyika.

Majimbo siyo lazima yarudishe ukabila kwa maana majimbo siyo lazima yakae kimkoa. Majimbo yanaweza kuwa divided into political, administrative regions. Hata mikoa mitatu inaweza ikawa administered kama jimbo moja...politically.

Mkuu gharama ya kuendesha serikali ya majimbo sioni kama itakua gharama kubwa uki zingatia sasa hivi wananchi wana lipia serikali mbili, bunge mbili, viongozi wa pande mbili etc. Anyway I think this issue it requires more debate.
 
Mzalendohalisi,

..wengi wanaopinga Majimbo wanadai yatarudisha ukabila.

..pia sijui gharama za kuendesha serikali za majimbo zitakuwa kiasi gani. nina wasiwasi zitaongeza mzigo kwa walipa kodi wa Tanganyika.

JokaKuu,

1. Ukabila..nadhani kama nchi tumeshavuka..tuko ktk level ingine! Mbona SA hawana ukabila na wana Majimbo system? Naona Majimbo itachochea zaidi maendeleo!

2. Gharama..hizi pesa za kuwalipa Wakuu wa Mikoa/Wilaya zinatosha..zitaongezwa kidogo.. Pia hizi pesa za Mfuko wa Jimbo za wabunge sii zingetumika huko ktk Majimbo?? Sizungumzii majimbo mengi..kama majimbo 6 au 7 tu. Na kunakuwa na kazi za federal gov. kama polisi, Elimu, Afya.

tukiwa na majimbo Visiwani wanashauriwa wawe na jimbo..swala je watakubali??
 
JokaKuu,

1. Ukabila..nadhani kama nchi tumeshavuka..tuko ktk level ingine! Mbona SA hawana ukabila na wana Majimbo system? Naona Majimbo itachochea zaidi maendeleo!

2. Gharama..hizi pesa za kuwalipa Wakuu wa Mikoa/Wilaya zinatosha..zitaongezwa kidogo.. Pia hizi pesa za Mfuko wa Jimbo za wabunge sii zingetumika huko ktk Majimbo?? Sizungumzii majimbo mengi..kama majimbo 6 au 7 tu. Na kunakuwa na kazi za federal gov. kama polisi, Elimu, Afya.

tukiwa na majimbo Visiwani wanashauriwa wawe na jimbo..swala je watakubali?

I doubt it.
 
serikali moja
pemba mkoa na unguja mkoa
kwa hiyo TZ kuwe na mikoa 23
na kila mkoa uwe na mayor na mayor awe anapigiwa kura na wananchi
cheo cha wakuu wa mikoa kifutwe
 
Mzalendohalisi,Mwanafalsafa1,

..ninavyoelewa ktk majimbo kuna serikali na bunge la kila jimbo. ndiyo mfumo wanaofuata Nigeria, USA etc ambako kuna majimbo.

..halafu tena kuna bunge la nchi nzima, nalo hujumuisha wabunge toka constituencies zilezile zilizoko ktk mabunge ya majimbo. sidhani kama wabunge wa majimbo huwa ndiyo hao hao wanakwenda kuingia ktk bunge kuu.

..pia unakuta kuna mawaziri wa majimbo, na tena kunakuwa na majeshi,polisi,mahakama za majimbo, na makorokoro mengine, na juu ya hao wote kuna federal government and its agencies.

..sasa nadhani hizo ni gharama kubwa sana.
 
Last edited:
Visiwani karibu kila mtu ni mwanasiasi au mtawala

Watu ni 1 milioni- angalia Raisi, Mawaziri-SMZ na SMT, Wabunge Muungano, wawakilishi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Masheha, Makatibu wakuu wa Wizara, Wakurugenzi!!! n.k

Sasa hapo niambie nani aliyebaki wa kumfanyia kazi mwingine ktk nchi ndogo hivi?

hapo kificho kaongea...Tatizo kubwa linaloleta machafuko zanzibar ...ni kuwa kila mtu ni mwanasiasa..especially unguja....wana kazi moja tu ya kutafuta nafasi za uteuzi au kuchaguliwa ...zikijaa za unguja wanaaza kuangalia za muungano .....hata pale inapolazimu baadhi ya nafasi kushikwa na PHD holders ..inabidi utaratibu usifuatwe ili ku accomodate qualifications ndogo za wenzetu kwenye baadhi ya fani.....
siku huu muungano ukivunjika kama wanavyotaka ....tutawapokonya wote wanaoshikilia nafasi za muungano na taasisi zake [unless wanaamua kuukana uzanzibar]..si mnajuwa hakuna mbara anayeshika nafasi yeyote kwenye SMZ....
SMZ ina mlongo mkubwa wa vyeo visivyokuwa na tija na idara zisizokua na tija.....zanzibar inaweza kuendeshwa na robo ya taasisi na viongozi waliopo sasa,wengine watafute kazi zingine wakafanye!!!
 
..hata mimi hili nimeliona.

..nadhani idadi ya wawakilishi sasa hivi ni almost three times ya waliokuwepo kabla ya Mapinduzi.

..hapo bado hujaongeza wabunge wanaowakilisha ktk bunge la muungano.

..sijui sababu yake ni nini haswa. Zanzibar haijaongezeka eneo, na mawasiliano naamini yamekuwa bora na ya kisasa kuliko kabla ya mapinduzi.

..huu ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi wa Zanzibar.

Juu ya kukubaliana nawe kimawazo hili la kuongezeka kwa eneo hakuwezi kuwa kigezo kwani nchi huwa na eneo hilo hilo na kinachofanyika ni kuangalia kiasi cha uwakilishi kwa eneo.
 
Visiwani karibu kila mtu ni mwanasiasi au mtawala

Watu ni 1 milioni- angalia Raisi, Mawaziri-SMZ na SMT, Wabunge Muungano, wawakilishi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Masheha, Makatibu wakuu wa Wizara, Wakurugenzi!!! n.k

Sasa hapo niambie nani aliyebaki wa kumfanyia kazi mwingine ktk nchi ndogo hivi?

Angalia usije ukaleta kebehi kwa kudharau unachokiona wewe ni kidogo.
Kama ni nchi juu ya udogo wake na uchache wa watu Zanzibar ni nchi na inahitaji safu ya uongozi kama nchi nyengine yoyote.
Kwani Zanzibar ina Marais wangapi? Jee hao mawaziri wa Zanzibar hawana nafasi za kuhudumia hizo wizara walizopangwa? Juu ya uchache wake kule kuna binaadamu ambao wanataka mahitaji yaliyo sawa kama mnayoyapata nyie Bara na kwa maana hiyo ndio huwekwa Mawaziri kuongoza nyanja hizo. Kwa vile wananchi hao millioni moja hawawezi kukaa pamoja na kutunga sheria wanahitaji wawakilishi na ndio maana ya kuwepo wawakilishi. Wabunge? Wao ni wawakilishi wa Wazanzibari kwenye hiyo Serikali ya upande wa pili. Wao wapo pale ili tu ionekane kuwa eti Zanzibar inashirikishwa katika maamuzi ya inatoitwa Tanzania.
Suala hapa lingekuwa ni kuangalia iwapo kama namba ya uwakilishi inaenda sambamba na haja ya kuwakilishwa na sio kuona safu ya uongozi haihitajiki eti kwa kuwa Zanzibar ni ndogo na ina watu wachache. Kama ukubwa na wingi wa watu kunapunguza mahitaji muhimu ya kibinaadamu yanayopelekea kuwekwa viongozi basi sijui tungesema nini Kuhusu Tanzania Bara kuilinganisha na nchi kama India naChina?
 
serikali moja
pemba mkoa na unguja mkoa
kwa hiyo TZ kuwe na mikoa 23
na kila mkoa uwe na mayor na mayor awe anapigiwa kura na wananchi
cheo cha wakuu wa mikoa kifutwe

Pogosha shuka ukiitegemea kutoka kwa jirani au vipi!
 
hapo kificho kaongea...Tatizo kubwa linaloleta machafuko zanzibar ...ni kuwa kila mtu ni mwanasiasa..especially unguja....wana kazi moja tu ya kutafuta nafasi za uteuzi au kuchaguliwa ...zikijaa za unguja wanaaza kuangalia za muungano .....hata pale inapolazimu baadhi ya nafasi kushikwa na PHD holders ..inabidi utaratibu usifuatwe ili ku accomodate qualifications ndogo za wenzetu kwenye baadhi ya fani.....
siku huu muungano ukivunjika kama wanavyotaka ....tutawapokonya wote wanaoshikilia nafasi za muungano na taasisi zake [unless wanaamua kuukana uzanzibar]..si mnajuwa hakuna mbara anayeshika nafasi yeyote kwenye SMZ....
SMZ ina mlongo mkubwa wa vyeo visivyokuwa na tija na idara zisizokua na tija.....zanzibar inaweza kuendeshwa na robo ya taasisi na viongozi waliopo sasa,wengine watafute kazi zingine wakafanye!!!

Jambo usilolijuwa ni usiku wa kiza! Kama unamaana ya wazawa kutoka pahala umekosea sana. Mbona Wabara wana nafasi nyeti huko Zanzibar, tuulize tukwambie usifikie conclussion bila kufanya utafiti.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom