Baraza la Madiwani lasimamisha Watumishi watatu Geita

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Snapinsta.app_426627153_18316325203193701_2125555842774966569_n_1080.jpg
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mkoani Geita, limewafuta kazi watumishi 3 wa Halmashauri hiyo kwa mujibu wa Kanuni za Kiutumishi .

Akitoa Taarifa hiyo katika kikao Maalumu kilichoketi mara baada ya kukamilika kwa Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Butobela, Charles Kazungu amesema watumishi hao wamefutwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya Utoro kazini.
Snapinsta.app_426600919_18316325224193701_2893918701056049341_n_1080.jpg

Snapinsta.app_426606636_18316325245193701_3963327129049595512_n_1080.jpg
“Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kauli moja limekwenda kuwafuta kazi watumishi watatu kwasababu ya kanuni zetu za kiutumishi ,” Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Kazungu.

Kazungu amewataja watumishi hao kuwa ni Aden Benard ambaye ni Afisa Mtendaji katika Kijiji cha Nzera, John Misango Afisa Mtendaji Kijiji na Walter Innocent ambaye pia alikuwa ni Mteknolojia Maabara, pia Baraza linaendelea kuwachungunza watumishi wawili akiwemo Mussa Alfredy ambaye ni Afisa Tabibu Msaidizi pamoja na Elisha Makaja ambaye pia ni Mteknolojia wa Dawa.
 
Manesi, watendaji na maafisa walioajiriwa na halmshauri hunyooooshwa hatari na vidiwani vilivyopita bila kupingwa.

Walimu walibahatika, hata ukinya kwenye Baraza la madiwani hawana Cha kufanya isipokuwa wakushiraki TSC

Katika hili walimu walijikomboa,vidiwani ni vipuuzi sana,ukiingia nacho ugomvi kinaenda kukuazimia.
 
Kazungu amewataja watumishi hao kuwa ni Aden Benard ambaye ni Afisa Mtendaji katika Kijiji cha Nzera, John Misango Afisa Mtendaji Kijiji na Walter Innocent ambaye pia alikuwa ni Mteknolojia Maabara, pia Baraza linaendelea kuwachungunza watumishi wawili akiwemo Mussa Alfredy ambaye ni Afisa Tabibu Msaidizi pamoja na Elisha Makaja ambaye pia ni Mteknolojia wa Dawa.
Semi gods at work🛑
 
Back
Top Bottom