Baraza la Maaskofu wa Pentekoste lakutana ghafla kuhoji kwanini halina mwakilishi Bunge la Katiba

Status
Not open for further replies.
ukienda hospital unakuta kuna wagonjwa jiulize hayo magonjwa wanayatoa wap? ukitumia akil kidogo hapo utapata jib. watu wanapata mapepo toka kwa ambao wanayafuga na kuamini ni maumini menzao....yaan kuna iman zinaabudu na majin.majin ni part and parcel ya iman na uumin wao.sasa yanapowatesa watu ndo wanaenda kanisan kutibiwa kama mtu anavyopata cholera huko then anaenda hospital. haimaanish anapoenda hosp ndo kilipo kipindupindu. shekhe kipozeo....kipozeo ni kama kitu kinachopoza kitu kingine.sasa hapo unapozewa kivip?
 
Hebu jihesabuni kwanza mpo wangapi?

Ungesoma vizuri mada ungeona kuwa kuna ma ASKOFU binafsi 2. Sasa unashindwa kuona umuhimu wa uwakilishi i wa kundi la watu milioni 10 unateua private bishops ambao hawawakilishi taasisi yeyote, wastaafu wa CCT. WEWE NA YULE ALIYETEUA MNA AKILI SAWA
 
Kuna watu waafikiri wao Tanzania ni mali yao hasa walio upanda wa magamba, kwa hiyo wapentecoste siyo watanzania?????????????????
 
Umeshawahi kusikia ibada ya krismasi imefanyika kitaifa katika kanisa fulani la Pentekoste. Au ibada ya pasaka itafanyika kitaifa katika kanisa fulani la pentekoste. Jibu ni hapana, mara zote hufanyika kwenye makanisa ya CCT (Anglikana na KKKT) au TEC (Catholic) Mahali zinapofanyika sherehe hizi, vyombo vya habari vya kitaifa hurusha hewani ibada husika.

Lakini umeshawahi kuona hiyo TBC (ambayo inayoendeshwa kwa kodi za watu wa dini zote wakiwemo wapentekoste na wale wasio na dini) ikionyesha kipindi cha jumapili ibadani kutoka katika kanisa la kipentekoste? jibu ni hapana.

Swali la kujiuliza: Kwanini wapenteKotse wanadharauliwa na serikali ya CCM?

Hapa kuna nadharia kama tatu ambazo makala hii itazijadili: Nadharia ya kwanza inaweza kujengwa kwenye uchache. Mtu ataweza kujipa ujasiri feki na kusema "hawadharauliwi ila ni wachache sana, yaani wapo kiduchu kama wafuasi wa ile dini ya marastafarian" au ile dini ya Bhai, au hadhi na idadi yao ni sawa tu na kundi la Bongo movies ambao idadi yao haijai kwenye kiganja cha mkono"

Hata hivyo hoja hiyo hapo juu ni hoja dhaifu kwani makanisa yaliyochini ya PCT(Pentecostal Coiuncil of Tanzania) yapo 10,000 nchi nzima na wanachama 10,000,000 TZ.

Nadharia nyingine ya Wapentekoste kutengwa tunaweza kusema labda ni ile tabia yao ya kutokunywa pombe na kuhubiri na kushawishi mno watu waache pombe na hatimaye wanasababisha serikali ya CCM kukosa mapato yatokanayo na kodi ya vileo. Nadharia hii inaweza kuwa na ka- ukweli fulani ingawa si ya msingi sana.


Nadhari nyingine inaweza kuwa mtazamo wa serikali kuwa Wapentekoste ni watu wapole, wanafuata misingi ya kibiblia bila uchakachuaji wowote, hivyo hata wakipunjwa au kuonewa hawana noma yaani kwa lugha ya kibiblia " akupigaye shavu la kulia mgeuzie na la kushoto amalize hamu ya kukupiga" serikali ya CCM inawatambua kuwa ni washamba na ni mamburura tu wasio na madhara yoyote. Hii inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya CCM kutowajali na kuwapuuza Wapentyekoste.

Kilele cha yote ni uteuzi wa Rais katika Bunge la katiba, amewadharau.

WITO: HIMAHIMA WAPENTEKOSTE TUUNGANE TULIANGUSHE HILI ZIMWI LINALOITWA CCM MWAKA 2015, KURA 10,000,000 ZINATOSHA KUCHAGUA RAIS ASIYE NA UBAGUZI.

GREAT THINKER TU WANARUHUSIWA KUJADILI
Tujikumbushe Uteuzi - TAASISI ZA DINI
1.Waislamu-kuna wajumbe-10
2.TEC kuna wajumbe-4
3.CCT kuna wajumbe-5
4.Maaskofu binafsi-2
5.PCT- Hakuna mjumbe hata mmoja.

Jadili vitu vya mana wewe!huu ni Ujinga....katiba ni ya Watanzania, sio Dini..mbona Waislamu awajalalamika kuwa wameunganishwa Pamoja bila kujali madhehebu,wakati kuna washia,suni,answal,nk mengine
 
Kwa kitendo chake cha kutubagua watu wa bwana ktk kujadili hatima ya tz yetu natangaza masaa 24 kwake otherwise nitamlaani mpaka atakapoenda kaburini

WAPENTEKOSTE TUUNGANE KUMLAANI JK,TUKO MIL 10 HIVYO 2015 TUTAIONDOA CCM RASMI KWA KUMDHIHAKI BWANA
 
Jadili vitu vya mana wewe!huu ni Ujinga....katiba ni ya Watanzania, sio Dini..mbona Waislamu awajalalamika kuwa wameunganishwa Pamoja bila kujali madhehebu,wakati kuna washia,suni,answal,nk mengine

Mkuu with all due respect.
Waislam tunaunganishwa na BAKWATA.
Hutaki unaacha.
Ila na sisi tupunguze uswahilu na ulalamishi.
Tukapiganie Ile Mahama yetu ilee
 
walokole in principle ni protestants mm cwatofautishi sana na lile jeshi lililopigana na malaika mbinguni na hatimaye likatupwa motoni kwa ghadhabu ya Mungu. wakiwepo utaskia viwanda vya pombe na sigara viondolewe, kuwe na std ya sadaka, na na vtu km hvo
 
Jadili vitu vya mana wewe!huu ni Ujinga....katiba ni ya Watanzania, sio Dini..mbona Waislamu awajalalamika kuwa wameunganishwa Pamoja bila kujali madhehebu,wakati kuna washia,suni,answal,nk mengine
Tutajuaje kuwa hoja yako sio ujinga jitazame kwanza ndipo ujibu na sio kuita dini za watu ujinga!!
 
Wadau tuacheni utani, PENTEKOSTE ina waumini kila kona, ni wengi hata kuliko Waislam hapa nchini. Hawa jamaa wameenea hadi vijiji uwezi kuamini

Mkuu utani wako mbaya sana kusema Walokole wengi zaidi ya Waislamu ktk nchi hii ya Tanganyika. Kijana tembea ujionee ukubwa wa nchi na watu wake,achana na stori za watu wanaojipachika Uaskofu,Utume,Unabii na Uchungaji bila hata Elimu ya Dini!
 
Mkuu with all due respect.
Waislam tunaunganishwa na BAKWATA.
Hutaki unaacha.
Ajabu ni kuwa Mufti wa BAKWATA amewafanyia takfir (kuwatoa katika Uislamu) Waislamu wote waliokataa kumtambua Kadhi aliyechaguliwa na yeye.

Sasa sijui ni Waislamu wangapi au wa namna gani wanaowakilishwa na BAKWATA! sijui.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom