Baraza la Maaskofu wa Pentekoste lakutana ghafla kuhoji kwanini halina mwakilishi Bunge la Katiba

Status
Not open for further replies.

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
1,231
Baraza la maaskofu la makanisa la PENTECOSTE Tanzania limekutana ghafla kujadili kwanini katika Bunge la katiba hakuna mwakilishi wao aliechaguliwa na Rais, wanasema walipeleka orodha ya majina lakini hawana muwakilishi.

Maaskofu hao wanasema wao ni taasisi kubwa na wana wafuasi wengi sana hapa tanzania. Wamesema iwapo hawatajibiwa hoja yao wataitisha kongamano la kitaifa kuamua hatua ya kuchukua.

Source: Channel Ten

NB: Pentecoste ni jamii ya Makanisa ya kilokole


Zacharia%20Kakobe.jpg

Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Askofu David Butenzi, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani), wakati Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo lilipotoa tamko lao kuhusu kutopata mwakilishi wao katika Bunge la Katiba pamoja na kupeleka orodha ya majina katika Ofisi ya Rais. Wengine kutoka kushoto ni Askofu Zakaria Kakobe, Katibu Mkuu wa makanisa hayo, Askofu David Mwasota na Askofu Sebastian Mcheri.


Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT), limesema limefedheheshwa na kusikitishwa kwa kunyimwa uwakilishi wa kushiriki katika Bunge maalum la Katiba licha ya kuwasilisha majina ya wajumbe wake.

Limesema kitendo cha kushindwa kupewa fursa ya kushiriki katika Bunge hilo, ni kuwanyima haki za msingi Watanzania wengi wanaowakilishwa na Baraza hilo, kama ilivyo kwa Watanzania wengine.

Akisoma tamko la baraza hilo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kufikiwa katika mkutano ulioshirikisha Maaskofu wakuu wa Madhehebu ya Kipentekoste jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa PCT, David Mwasota, alisema wameamua kutoa tamko hilo ili kuonyesha namna ambavyo wamesikitishwa na kitendo hicho.

"Tumewaita leo (jana) ili mtusaidie kufikisha masikitiko yetu kwa viongozi, Watanzania na waamini wa Kipentekoste kutokana na kitendo cha serikali yetu tunayoiheshimu, kuipenda na kuiombea, kwa kutubagua na kututenga katika bunge maalum la Katiba, huku tukiwa ni miongoni mwa taasisi kubwa za kidini na makundi mengine ya kijamii," alisema na kuongeza:

"Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais aliagiza makundi mbalimbali ya kijamii na taasisi za kidini kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kuchaguliwa kushiriki katika bunge maalum la Katiba na kwa kuzingatia wingi wa wanachama wetu tulipendekeza majina tisa ya watu tulioona wanafaa kutuwakilisha, lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyeteuliwa."

Aidha, aliongeza kuwa ikiwa serikali itaendelea kunga`ng`ania msimamo wake wa kutaka wajumbe wa baraza la PCT wasihusike katika Bunge hilo, Baraza litaitisha mkutano mkuu wa dharura wa kitaifa utakaojumuisha maaskofu wote wa kitaifa, Kanda na jimbo, mitume na manabii na wachungaji zaidi ya 30,000 ili kutafakari kwa pamoja na kuamua hatua za kuchukua.

Mjumbe wa TCP ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe, alisema Katiba ni haki ya Watanzania wote hivyo haoni sababu ya wengine kubaguliwa.



CHANZO: NIPASHE
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Tamrina Manzi2. Olive Damian Luwena
3. Shamim Khan4. Mchg. Ernest Kadiva
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo6. Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
7. Magdalena Songora8. Hamisi Ally Togwa
9. Askofu Amos J. Muhagachi10. Easter Msambazi
11. Mussa Yusuf Kundecha12. Respa Adam Miguma
13. Prof. Costa Ricky Mahalu
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo2. Suzana Peter Kunambi
3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu4. Fatma Mohammed Hassan
5. Louis Majaliwa6. Yasmin Yusufali E. H alloo
7. Thuwein Issa Thuwein




PENTEKOSTE WALIA KUBAGULIWA
BAADHI ya taasisi za kidini, wanaharakati na watu binafsi, wamepinga vikali uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, huku Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT) likidai kubaguliwa na serikali kwa miongo miwili.Kwamba badala ya uteuzi huo kuzingatia uwakilishi wa makundi stahiki, umefanyika ujanja wa baadhi ya wanasiasa kujipenyeza katika makundi wasiyostahili pamoja na ndugu zao kisha wakateuliwa kuwa wajumbe.Kwa mtazamo huo, Bunge Maalumu la Katiba linatazamwa kuwa limetawaliwa na undugu wa kisiasa badala ya kuzingatia utaratibu na sheria zilizowekwa katika utezi wa wajumbe kupitia makundi.
Kwa mujibu wa taarifa yao kwa vyombo vya habari jana, PCT imedai kuwa majina waliyopeleka hayakuchaguliwa kuingia Bunge Maalumu la Katiba.Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa PCT, David Batenzi, alisema ni kwa miongo miwili sasa wamekuwa wakibaguliwa na kutengwa.Alisema kuwa wanaishangaa Serikali ya CCM kuendeleza mfumo dini ambao imekuwa ikifanya ubaguzi wa makusudi kwa baadhi ya makundi ya dini.
Batenzi alisema mfumo huo umekuwa ukikumbatia makundi mengine ya kidini hali ambayo imesababisha wengine kupokwa haki zao za msingi wanazostahili kupewa na serikali.Alisema utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonyesha hali ya udini, usiasa na ukabila imeendelea kujitokeza katika nchi, hususani unapofika wakati wa kuamua masuala yenye manufaa ya taifa katika vizazi vijavyo."PCT inaundwa na maaskofu wakuu wa madhehebu ya Kipentekoste yapatayo 75, ili waongoze na kusimamia misingi ya imani ya Kipentekoste kwa waumini wake wapatao milioni 10 Tanzania bara na Visiwani," alisema.Alisema hii si mara ya kwanza kwa serikali kupuuza mapendekezo yao, kwani imekuwa ikiwabagua na kuwatenga kila yanapojitokeza masuala yanayohusu uwakilishi wa kidini katika taifa."Leo hii tunajitokeza hadharani ili kutetea haki yetu ya kikatiba kwani tunaamini haki huinua taifa na dhambi ni aibu ya watu wote, ubaguzi umeendelea kwa miongo miwili sasa, tumekuwa hatuhusishwi.
"Katika sherehe za kitaifa, katika maombi na dua wakati rais mteule anapoapishwa, kunyimwa fursa ya kushiriki kutoa mahubiri na mafundisho katika runinga na radio za kitaifa kama taasisi nyingine," alisema.Aliongeza kuwa wameshangazwa na serikali kuwaona hawafai, hawana sifa za kuweza kuchaguliwa katika Bunge Maalumu la Katiba na kuteua taasisi nyingine za kidini zenye hadhi kama yao."Ikiwa serikali itang'ang'ania msimamo wake wa kutaka wajumbe wa PCT wasihusike katika Bunge hilo tutaitisha mkutano mkuu wa dharura ili kutafakari hatma ya kutengwa kwetu na kuchukua hatua," alisema Batenzi.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Penuel Hill Ministry, Alphonce Temba, alisema kuwa kilichofanyika katika uteuzi huo kinaweza kutafsiriwa kwamba ilikuwa ni wanasiasa kujazana ili kuteka mchakato."Hivi hili litakuwa Bunge la namna gani ambalo unakuta mtoto na mama au baba yake, mtu na kaka au dada yake wote wamekuwa wajumbe wa Bunge maalumu. Wananchi wengine wameachwa wapi?
Mchungaji Temba alisema kuwa ushauri wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesigwa Baregu unapaswa kufanyiwa kazi kwa kuyarudisha majina kwa wananchi ili wachague.Alisema uwakilishi wa viongozi wa dini haujatendewa haki na wengine wameachwa ambao wangesaidia katika uchambuzi wa rasimu hiyo ya katiba.
Wakati huo huo, wanaharakati wa masuala ya kijinsia, haki za binadamu, demokrasia na utawala bora, wamedai kuwa mchakato wa uteuzi umekuwa na upungufu na sura tofauti kama ilivyokuwa katika kipindi cha kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013.Taaarifa ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGP), Lilian Liundi kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa wamefuatilia kwa makini mchakato huu wakiwa pamoja na wenzao wa mashirika mengine ya kiraia.
Alisema kuwa walipendekeza majina ya wataalamu wa masuala ya kijinsia na haki za binadamu ambao wangeweza kutoa uchambuzi wa kina na kushiriki kutetea baadhi ya vifungu vya rasimu ambavyo vinabeba sauti za wananchi kwa mustakabali wa taifa letu, lakini hawakuteuliwa.Alisema kuwa kukosekana kwa ushiriki mpana wa uwakilishi wa makundi halisi yaliyoko pembezoni na kuchomeka majina ya watu wasiostahili kwenye nafasi za makundi mengine kutasababisha upungufu mkubwa wa uwakilishi katika mchakato huu.
"Tumesikitishwa na kuingizwa kwa majina ya wanasiasa kwenye kundi la NGO na kuwaacha wawakilishi wa asasi za kiraia wakati wanasiasa walikuwa na uwakilishi mkubwa kwenye kundi lao la watu 40."Aidha kundi la watu wenye mlengo unaofanana nalo hatukupewea tafsiri halisi kuwa ni watu kutoka kundi gani au ni kina nani, badala yake wameingia wanasiasa na kulifanya Bunge hili la katiba kuwa na wanasiasa wengi zaidi ya makundi mengine," alisema.
Alisisitiza kuwa wanaendelea kudai usawa wa kijinsia katika mchakato huu kwani msingi wa kijinsia haujazingatiwa kama vile Itifaki ya Maputo, AU Constituent Act, AU Shared Values na CEDAW na Mkataba wa Watoto (CRC) inavyotamka.





 
mimi ni miongoni mwa walokole halafu nimechaguliwa wakae watulie nitawawakilisha vema.
 
Na sisi mashahidi wa jehova tutakutana kesho.

Nasikia Wabahai, wahindu, wasabato, zion church na jeshi la wokovu nao wanakutana

Bila kusahau chama cha maseremala, mafundi bomba, umoja wa wakwezi, umoja wa wauza ulanzi nk... mwisho wake kila mtu atataka awemo
 
Mmoja wa hao wanaojiita maaskofu alisema umeme unaopitishwa mbele ya kanisa "lake" hautawaka. Ulipowashwa tu ukaanza kuwaka. Na watu bado wanamfata mtu huyo. AMA KWELI. Watu wa aina hiyo wanatafuta sana kuonekana tu cheap popularity lakini la maana hatuoni zaidi y kulamba sadaka n michango y wafuasi wao
 
Walokole wamedharaulika katika jamii ya watanzania kwa sababu ya mienendo na tabia za kujipendekeza za viongozi wao mfano wa kina mzee wa upako, mwingira, Temba na wengine kama hao. Kwa kifupi ni kwamba hawajiamini na hawana pa kuwajibika hivyo katika maisha ya kila siku ya jamii inayowazunguka hayawahusu.
.
 
Na sisi mashahidi wa jehova tutakutana kesho.

Nasikia Wabahai, wahindu, wasabato, zion church na jeshi la wokovu nao wanakutana

Bila kusahau chama cha maseremala, mafundi bomba, umoja wa wakwezi, umoja wa wauza ulanzi nk... mwisho wake kila mtu atataka awemo

Bila kusaha umoja wa wala rambirambi, umoja wa wabeba mabox na umoja wa makaka wanaolala sebureni kwa dada zao, nao wanataka wapewe nafasi katika bunge la katiba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom