Baraka za kichaa.....nimebarikiwa sana leo

Tutafika

JF-Expert Member
Nov 4, 2009
1,443
631
Basi leo ndani ya A - town, nimetoka katika hotel moja kupata lunch nikiwa nimeshika chupa ya maji mkononi. Baada ya kutembea kama hatua 100, nikakuta mama mmoja aneonekana kuwa kichaa wa siku nyingi amekaa pembeni ya barabara na furushi la vitu. Mara nikasikia yule mama ananiita ''..mwanangu, we mwanangu naomba hayo maji ninywe. kweli kabisa mi sijawahi kuiba kitu cha mtu...na maneno mengine kibao''

Nikamuangalia kidogo nikakumbuka jana pale mjini Moshi nilikutana na kichaa mwanaume ana bonge la fimbo na akaja kwangu akiwa anafoka eti ''nikupige, nikupige..?'' nikajisemea ngoja niangalie kama na huyu ni wa aina ile ya jana!, Basi nikaona ni mpole nikamfuata kule alikokaa nikampa yale maji. Mama yule aliyapokea na kuanza kunimwagia baraka nyingi sana huku akichomoa Rozali yake shingoni. Yaani nimejisikia vizuri sana kupewa baraka na kichaa kwani nimehisi zimeandikwa mbinguni moja kwa moja!!


Blessed is the hand that give.....Lucky Dube
 
Lakini baraka kwa kuombwa maji? Unapaswa kuona mahitaji ya watu na kusukumwa kusaidia kabla hujaombwa. Anyway, chunga hiyo baraka uliyopata. Isitokee upande wa pili kwa kiburi na majivuno.
 
hao vichaa mbona wamekuhusudu hivyo....?au wamedhani wewe mwenzao nini?....

Labda, wakitokea wengine wakafika 10 nitauliza wataalam wa saikolojia ya vichaa waniambie sababu inaweza kuwa ni nini.
 
Lakini baraka kwa kuombwa maji? Unapaswa kuona mahitaji ya watu na kusukumwa kusaidia kabla hujaombwa. Anyway, chunga hiyo baraka uliyopata. Isitokee upande wa pili kwa kiburi na majivuno.

Kweli, lakini si uliona yule wa kwanza kule moshi alivyotaka kunitandika mikwaju?, Sikua na lengo la majivuno ndugu yangu, nilitaka tu tujifunze wote (mimi na wewe) kwa hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom