Barabara yaweka rehani ubunge wa Dr. Mwakyembe 2015...

Kyela waliyataka wenyewe kwa kuacha kumchagua Mtu ambaye ameleta misaada na mwamko kibao hapo Kyela.

Ni mtu mwenye muono wa mbaali sana wa kimaendeleo na uchungu sana na jimbo lake.

Shida yake kubwani kung'ang'ania kugombea kupitia CCM. Sijui mwaka 2015 kwa hali inavyokuwa mbaya kwa CCM, watu kama yeye wanaoamini CCM ya Nyerere bado ipo hai, watagombea bado kwa kupitia CCM.

Pamoja na uwezo wake mdogo, amekuwa MENEJA mzuri kwa kuwaanzishia vitu vingi tu wana Kyela.

Pichani, jengo JEUPE lililo na paa jekundu kushoto, ni sehemu lilipo Duka, likifuatiwa na jengo ilipo Kyela FM (Radio) na kwa nyuma upo ukumbi wa mkutano na vyote hivyo vikiwa sehemu ya Kyela Business Centre (KBC). Miradi hii imetoa AJIRA kwa vijana wengi sana na Radio imechangamsha mji na kutoa ELIMU kwa watu wa Kyela hadi nje ya Mpaka wa Tanzania.
Watu kama Dunga Dunga, wamekuwa maarufu sana na kujipatia mialiko sehemu nyingi kama wageni wa heshima.

100_0486.JPG

Kama nilivyosema hapo juu, ukumbi wa Mkutano ambao unatumia KIYOYOZI kuweka hali ya heya nzuri humo ndani kama unavyoonekana NYUMA ya jengo ilipo Kyela FM. Hata wageni hawa kutoka German, waliona ndiyo SEHEMU pekee wanayoweza kupiga picha na kuonyesha kwenye Blog zao. HONGERA MTANZANIA aka George Mwakalinga.

P1030551.JPG

NB: Na wewe Mwakalinga basi, hebu jipigepige umalizie hizo kuta za jengo na madirisha....... Najua uchaguzi ulikula hela Mtani wangu ila muda umewadia sasa hilo jengo liishe ili kubadilisha kabisa sehemu ya kupigia picha iwe kwa mbele ya jengo na si NYUMA.
 
Sikonge;

Mwakalinga George njoo upinzani tuanze kufanya mikakati ya kui-revival Kyela yetu inayodidimia;lkn Mwakalinga asipo tusikiliza na akigombea kupitia CCM ya JK iliyochuja kiasi hiki nakuhakikishia nitamgaragaza vibaya hata kata anayotoka ya Katumba-Songwe;naweka ahadi yeye akipata hata kura 5 kwenye kata yangu ya Ngonga nitamtangaza kashinda!

Mwakalinga au yeyote yule akigombea kupitia CCM sidhani kama kuna kata watashinda Kyela kwa jinsi walivyotutenda!
 
MMHHH haya bwana siasa wote mnaziendesha kwa kulalamika, but I can assure u matatizo hayo yaliyopo hayahitaji mtu mjanja mjanja katika kuyashughulikia msije mkazaa mtu anayepinga ufisadi mwingine, Haitoshi kuhitaji A level school wakati O level hawafaulu nani atakuja kusoma hizo shle. Mimi msimamo wangu ni kuwa wana kyl wote tuungane kuzikabili hizi changamoto hata ukiwa nje ya uwanja, Baadhi tunafanya baadh ya research huko tukiwa likizo na kuja na vijisuluhisho kwa pale tunapoweza, huyo africa anasubili ubunge ndo ajue kwanini watoto wanafel??? si atajipanga mwaka mzima. Unajua kwanini kuna failure rate kubwwaa?? sasa watu tumepiga tempo huko na kukaa na madent na kujua ubovu ni nini . Kama mnataka kuikomboa kyl sio kila kitu kukimbila siasa we can even discus those issues hata kama sio wabunge na tukafanya yaliyo ndani ya uwezo na yaliyo nje tusubili hizo siasa za JOPE AKAGELEPOOOO,, njoo kyela member fb u welcome au mnaweza kuwa mpo but mnaogopa chngamoto kule msipinge ufisadi tutawarushia mawe we need kaziiii

Wanafunzi watafaulu vipi wakati;
1. Hakuna vifaa vya kufundishia mashuleni
2. Walimu wanafundisha katika mazingira magumu
3. Wanafunzi wanakosa motisha wa kusoma kwavile hata wakifaulu wote watakwenda kusoma kwenye shule ya nani wakati kila Wilaya hapa nchini inahangaika na watoto wao?

Moja ya motisha ya mwanafunzi kufaulu ni lazima ajue hata akifaulu atakwenda kusoma wapi? Bila kuwekewa mazingira hayo atakata tamaa mapema na sisi tutaishia kumlaumu tu.

Hivyo mtoto wa CHEKECHEA atafaulu kama atatambua kuwa kuna shule za MSINGI, na wa msingi atafaulu kama atatambua kuna shule za SEKONDARI, na wa Sekondari hivyo hivyo kama atatambua kuna A-LEVEL na wa A- Level kama atatambua kuna CHUO chochote katika maeneo husika bila hivyo watateuliwa au watafaulu tuwale waliobarikiwa.

Mwananchi mzuri ni yule anayetambua mazuri na mabaya yaliyofanywa na mwenziye na si yule anayeona mabaya tu kwani hata Wabunge waliotangulia Kyl wamefanya mazuri na mabaya kulingana na uwezo wao kwa vile hata wao sio malaika wafanye mazuri tu. Mfano; Mhe.Mwakipesile (1975 – 1985) alifanya mazuri mengi tu, Mhe. Alipipi L. Kasyupa(1985 – 1995) alifanya mazuri mengi tu, Mhe. John L. Mwakipesile (1995 – 2005)naye pia alijitahidi, Mhe. Harrison G. Mwakyembe (2005 – Sasa) naye pia amejitahidi.

Lakini tujiulize kwanini Kyl haijapiga hatua kubwa kimaendeleo wakati ina rasilimali nyingi? Kyl yenye mabonde, ziwa, bandari,mito, boda (Malawi), fukwe na makaa ya mawe.

Jiulize kwanini bus la Mohammed Trans linawatoa wafanyabiashara Lilongwe (Malawi) hadi DSM zaidi ya km 1500 kununua bidhaa wakati tungeweza kujenga soko la Kimataifa pale Boda (Kasumulu) wakaishia pale kama Tunduma?
Kyl ni yetu hivyo hakuna haja ya kulumbana kwani fito tulizonazo zitumike kuijenga Kyl yetu.
 
Katika analysis yangu katika jimbo la kyela wananchi wanasema huenda ukawadia mwisho wa ccm katika jimbo la kyela mara itapofika mwaka 2015 huku barabara ya kyela-ipinda-matema haitakuwa imejengwa kwa kiwango cha lami...tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi na uchaguzi wa kwanza mwaka 95 wabunge wa CCM wamekuwa wakiahidi kuijenga barabara hiyo lakini hakuna kilichofanyika.
Mbunge wa kwanza alikuwa Kasyupa, akaja akaja mwakipesile na sasa Mwakyembe wote wametoa ahadi hizohizo...
Katika kampeni zake Mwakyembe aliwaambia wananchi wa kyela kuwa wampigie kura Kikwete kwa sababu amemwahidi kuijenga barabara hiyo.
Katika maelezo yake bungeni Mwakyembe alisema hawezi kudai ujenzi wa barabara ya wilaya wakati barabara za mikoa katika mikoa mingine bado hazijajengwa kauli ambayo ilileta minong'ono mingi miongoni mwa wananchi wa kyela...
Katika kata za Talatala, Ipinda, Lusungo, Makwale na Matema wamesema watalazimika kufanya mabadiliko iwapo barabara hiyo haitajengwa.
Hata baada ya kupewa unaibu waziri wa ujenzi wananchi wengi wa kyela wamekuwa wakiweka matumaini mengi kwa Mwakyembe lakini hadi hivi sasa ikiwa imebakia takribani miaka mitatu ya ubunge wake hakuna kilichofanyika.
CCM haina ushawishi wa kichama katika jimbo lolote lile bali kimebaki na ushawashi wa mtu binafsi tu,hivyo iwapo wananchi wa kyela wataamua kuachana na mwakyembe jimbo hilo litakwenda kwa upinzani maramoja...mathalani katika kata ya ipinda tayari chadema kilishapata diwani katika uchaguzi wa 2010 na katika kata nyingi kama ile ya makwale ccm ilipata upinzani mkubwa...vijiji vingi vya talatala, tenende, ipinda, kafundo, ikulu, bwato, lupaso, lukama, mpanda lusungo, kisale, mpunguti, makwale na matema vinapata usumbufu mkubwa wa usafiri ikiwemo gharama kubwa za usafiri kutokana na ubovu wa barabara....Mwakyembe itambidi afanye jithada kubwa kuweza kujenga barabara ile ili kuongeza ushawishi..HAKUNA MAENDELEO KATIKA JIMBO LA KYELA NA MWAKYEMBE AMEKUWA MTU WA KYENYE MAGAZETI TU NA SIO MAENDELEO YA JIMBO LA KYELA...HAELEWANI NA WATENDAJI WENGI WA JIMBO HILO.

Mkuu Mwakiluma,
Sahihisho kidogo katika ujumbe wako, CHADEMA hawana diwani kata ya Ipinda, diwani wa kata hiyo ni Dr. Hunter wa CCM.
Kyela ina kata 21 na kati ya hizo madiwani wa CCM ni 19 na CHADEMA ina wawili kutoka kata za Usale na Itope. Diwani wa kata ya Itope ni mwanamama.

Mkuu Wwww,
Kyela tayari ina shule mbili za serikali za A-level ambazo ni Kyela Day pamoja na Matema. Hivyo rekebisha kidogo records zako.

Ni kweli kwa watu wengi Kyela, hiyo barabara ya Nkuyu mpaka Ipinda na Matema ni muhimu mno, na kwa vipindi mbalimbali serikali pamoja na wabunge wetu wamekuwa wakiahidi kuijenga lakini mpaka sasa ahadi hizo hazijatekelezwa. Kwa nilivyoona mimi hata hiyo barabara iwekwe lami bado Kyela tutaendelea kuwa nyuma kama hatutafanya juhudi kubadili fikra zetu ili ziwe chanya na zilenge kwenye kujiaminisha wenyewe kwamba tunaweza kujiletea maendeleo yetu wenyewe kama watu binafsi, famili na wilaya.

Kyela tunaweza kulaumu watu wengine lakini huenda tatizo liko kwetu sote maana tumekuwa tukiongea mno na kusahau kwamba maendeleo ya wilaya yetu hata siku moja hayawezi kuletwa na mtu mmoja. Kwamba sisi wenyewe lazima tujiletee maendeleo yetu kupitia mipango mbalimbali. Kiongozi atakayefaa ni yule ambaye atasaidia kuvunja makundi ambayo Kyela yamejazana na kikubwa atakuwa na ubunifu juu ya miradi mbalimbali yenye tija ambayo itatumia resources zilizopo ili kuisukuma wilaya mbele. Wilaya ikiamua na kwa resources zilizopo, inaweza kabisa hata kuanza kujenga kwa kiwango cha lami baadhi ya barabara zetu hata kama ni km tano tu kwa mwaka kuliko kusubiri mpaka serikali itimize ahadi zake.

Mambo kama shule, afya na vitu vingine tunaweza kusaidiana kuviboresha bila hata juhudi ya mbunge. Wale wenye ubunifu na ambao wanafanya mambo ya maana tuwaunge mkono na sio kuwapiga vijembe na kuongelea siasa tu miaka mitano. Sasa Mango Tree wanaanzisha chuo, kama tuko serious na Kyela basi tuwaunge mkono ikiwezekana hata kuwaelemisha ndugu zetu ili wafaidike na kuwepo kwa chuo hicho. Lakini cha kushangaza utakuta badala ya kuwaunga mkono watu kama hao sisi tunaanza kuwaundia majungu na mizengwe kibao.

Kyela ina bahati ya kuwa na zao la kokoa ambalo lina soko na halina kazi kubwa kulilima, lakini inakuwaje tunashindwa kutumia sehemu ya pato hilo kujijengea nyumba za maana kama wenzetu wa wilaya ya Rungwe? Tuko active sana kwenye kusema na kuandika lakini kule chini tunahitaji zaidi watu ambao ni active kwenye kutenda. Kuzisaidia hizo shule zetu ziwe imara na kusaidia afya ili watoto na akina mama wasife hata kwa magonjwa ambayo yanatibika kirahisi.

2015 imebaki kama miaka mitatu, lakini watu tayari tumejikita kwenye majina ya watu. Tutumie huu muda kuwabana viongozi wetu wote ili wafanya yale waliyoahidi na pia tuandae sifa za watu ambao tutataka wawe viongozi 2015. Kutumia mijadala yote kuongelea majina ya watu naona ni kupoteza muda maana tuna uhakika gani hata hao watu watakuwepo 2015.

Sisi wote tunaolaani maendeleo duni ya Kyela basi tusaidie hata kukuza japo kilimo kupitia familia? Unapita Rungwe wana migomba ina afaya, unaingia Kyela ni balaa tupu. Unaenda vijijini, unakutana na nyumba zinatisha huku nje wahusika wamezungukwa na utajiri mkubwa wa kilimo. Kwanini tusiwashauri hawa wazee wetu wabadilike na kuweka maendeleo ya familia mbele? Kwanini tunashindwa kuwashauri wazee na ndugu zetu waachane na ushirikina na kuamini kila jambo kuna mkono wa mtu?

Kyela wote tuna matatizo makubwa na tuanze kujirekebisha kuanzia kwenye familia zetu. Ifike mahali tujikite kwenye kutenda hata kama ni jambo dogo. katu maendeleo hayataletwa na Magamba au Magwanda bali wana Kyela wenyewe.
 
Sikonge;

Mwakalinga George njoo upinzani tuanze kufanya mikakati ya kui-revival Kyela yetu inayodidimia;lkn Mwakalinga asipo tusikiliza na akigombea kupitia CCM ya JK iliyochuja kiasi hiki nakuhakikishia nitamgaragaza vibaya hata kata anayotoka ya Katumba-Songwe;naweka ahadi yeye akipata hata kura 5 kwenye kata yangu ya Ngonga nitamtangaza kashinda!
Mwakalinga au yeyote yule akigombea kupitia CCM sidhani kama kuna kata watashinda Kyela kwa jinsi walivyotutenda!

Inaonekana wanamageuzi mmeng'ang'ana sana kuzungumzia vyama. Chama cha Siasa hakitaleta mageuzi Kyl isipokuwa Umoja, Ushirikishaji wananchi katika kufanya maamuzi, Upendo, Uzalendo, Fikra hai, Kuweka pembeni itikadi zetu za vyama, Kujitambua na Kuziendeleza na Kuzisimamia vizuri rasilimali zilizopo ndiyo mambo ya Msingi.
 
Sikonge,
Itabidi ushitakiwe kwa kuvunja sheria za copyright. Wewe toka umesema utakuja Kyela mpaka leo miaka. Njoo, utuletee hizo pesa tumazie kazi.
 
Mkuu Mwakiluma,
Sahihisho kidogo katika ujumbe wako, CHADEMA hawana diwani kata ya Ipinda, diwani wa kata hiyo ni Dr. Hunter wa CCM.
Kyela ina kata 21 na kati ya hizo madiwani wa CCM ni 19 na CHADEMA ina wawili kutoka kata za Usale na Itope. Diwani wa kata ya Itope ni mwanamama.

Mkuu Wwww,
Kyela tayari ina shule mbili za serikali za A-level ambazo ni Kyela Day pamoja na Matema. Hivyo rekebisha kidogo records zako.

Ni kweli kwa watu wengi Kyela, hiyo barabara ya Nkuyu mpaka Ipinda na Matema ni muhimu mno, na kwa vipindi mbalimbali serikali pamoja na wabunge wetu wamekuwa wakiahidi kuijenga lakini mpaka sasa ahadi hizo hazijatekelezwa. Kwa nilivyoona mimi hata hiyo barabara iwekwe lami bado Kyela tutaendelea kuwa nyuma kama hatutafanya juhudi kubadili fikra zetu ili ziwe chanya na zilenge kwenye kujiaminisha wenyewe kwamba tunaweza kujiletea maendeleo yetu wenyewe kama watu binafsi, famili na wilaya.

Kyela tunaweza kulaumu watu wengine lakini huenda tatizo liko kwetu sote maana tumekuwa tukiongea mno na kusahau kwamba maendeleo ya wilaya yetu hata siku moja hayawezi kuletwa na mtu mmoja. Kwamba sisi wenyewe lazima tujiletee maendeleo yetu kupitia mipango mbalimbali. Kiongozi atakayefaa ni yule ambaye atasaidia kuvunja makundi ambayo Kyela yamejazana na kikubwa atakuwa na ubunifu juu ya miradi mbalimbali yenye tija ambayo itatumia resources zilizopo ili kuisukuma wilaya mbele. Wilaya ikiamua na kwa resources zilizopo, inaweza kabisa hata kuanza kujenga kwa kiwango cha lami baadhi ya barabara zetu hata kama ni km tano tu kwa mwaka kuliko kusubiri mpaka serikali itimize ahadi zake.

Mambo kama shule, afya na vitu vingine tunaweza kusaidiana kuviboresha bila hata juhudi ya mbunge. Wale wenye ubunifu na ambao wanafanya mambo ya maana tuwaunge mkono na sio kuwapiga vijembe na kuongelea siasa tu miaka mitano. Sasa Mango Tree wanaanzisha chuo, kama tuko serious na Kyela basi tuwaunge mkono ikiwezekana hata kuwaelemisha ndugu zetu ili wafaidike na kuwepo kwa chuo hicho. Lakini cha kushangaza utakuta badala ya kuwaunga mkono watu kama hao sisi tunaanza kuwaundia majungu na mizengwe kibao.

Kyela ina bahati ya kuwa na zao la kokoa ambalo lina soko na halina kazi kubwa kulilima, lakini inakuwaje tunashindwa kutumia sehemu ya pato hilo kujijengea nyumba za maana kama wenzetu wa wilaya ya Rungwe? Tuko active sana kwenye kusema na kuandika lakini kule chini tunahitaji zaidi watu ambao ni active kwenye kutenda. Kuzisaidia hizo shule zetu ziwe imara na kusaidia afya ili watoto na akina mama wasife hata kwa magonjwa ambayo yanatibika kirahisi.

2015 imebaki kama miaka mitatu, lakini watu tayari tumejikita kwenye majina ya watu. Tutumie huu muda kuwabana viongozi wetu wote ili wafanya yale waliyoahidi na pia tuandae sifa za watu ambao tutataka wawe viongozi 2015. Kutumia mijadala yote kuongelea majina ya watu naona ni kupoteza muda maana tuna uhakika gani hata hao watu watakuwepo 2015.

Sisi wote tunaolaani maendeleo duni ya Kyela basi tusaidie hata kukuza japo kilimo kupitia familia? Unapita Rungwe wana migomba ina afaya, unaingia Kyela ni balaa tupu. Unaenda vijijini, unakutana na nyumba zinatisha huku nje wahusika wamezungukwa na utajiri mkubwa wa kilimo. Kwanini tusiwashauri hawa wazee wetu wabadilike na kuweka maendeleo ya familia mbele? Kwanini tunashindwa kuwashauri wazee na ndugu zetu waachane na ushirikina na kuamini kila jambo kuna mkono wa mtu?

Kyela wote tuna matatizo makubwa na tuanze kujirekebisha kuanzia kwenye familia zetu. Ifike mahali tujikite kwenye kutenda hata kama ni jambo dogo. katu maendeleo hayataletwa na Magamba au Magwanda bali wana Kyela wenyewe.

Mtanzania
Nimerekebisha records zangu nashukuru sana kwa taarifa, hivyo kwa sasa tuna shule za A- Level tatu sio? Dennob, Kyela Day na Matema sio?

Hata hivyo kama Mango Tree wataanzisha Chuo japo sijui ni chuo gani lakini binafsi nitawaunga mkono na nitawatangaza popote pale TZ na Nje ya Nchi. Muungwana ni yule anayetambua michango ya wengine mfano George Mwakalinga binafsi nitamuunga mkono sana kwa kuanzisha KYELA FM, anayebeza kwa itikadi za siasa huyo sio mwanamageuzi.

Vile napenda kukuambia kuwa umenifurahisha sana kwa mchango wako, kweli wewe ni mwanamageuzi. Kyl haitajengwa na mtu mmoja ila sisi sote. Hata hizo nyumba za nyasi unazosema zimetoa watoto ambao wana maisha mazuri lakini hawataki kubadilisha maisha ya wazazi wao waliowasomesha.

Kwavile tumekosa upendo kwa wazazi wetu ndio maana unaziona hizo nyumba la sivyo usingeweza kuona nyumba ya nyasi hata moja Kyl.

Lakini ndugu yangu Mtanzania tambua kuwa maendeleo ya Tukuyu ni nguvu za Wanakyela pia, unakumbuka kuwa kabla ya Kyela kuwa Wilaya miaka ya 1970 Kyela na Ireje tulikuwa chini ya Rungwe, hivyo maendeleo yote tuliyaelekeza kule.

Hata hivyo kunahijika fikra mpya katika kuleta maendeleo kuanzia kwenye familia zetu kama ulivyosema.
 
Wwww,

Chuo cha Mango Tree kitaitwa Kyela Polytechnic College na kozi zao ni kama wanavyoeleza wenyewe hapa chini (nimeitoa hii Facebook ya Kyela).

65758_10150564115026637_591406636_9512027_90928150_n.jpg

Tutaanza kutoa Kozi tano kama ifuatavyoi:

(a). Agriculture and food processing-walengwa ni wakulima wadogo, wazazi, walezi wa watoto yatima na watu wengine. Lengo la kozi ni kukifanya kilimo kuwa kama biashara, na watu watafundisha njia za kisasa za ufugaji samaki, kuku, nyuki. Kozi hii itakuwa ya wiki 5.

(b). Hospitality and Tourism -
(1).Certificate in Hotel Management -Walengwa form IV POINT 28 kuendelea, muda ni miaka miwili 2.
(2).Foundatio course for Hotel Management-walengwa ni darasa la 7 na form four failures , hawa watasoma kwa miezi 9 kisha watajiunga mwaka 1 wa speciization.

(c).Business Administration -
Certificate in Business Adminstration , form four point 28 kuendelea

(d).ICT
Basic Comp Application- 6 weeks, 2 hours contact per day, walengwa ni watu wote

Certificate in Computer repair and maintainance, 2 years, walengwa form IV point 28 kuendelea

(e). Construction Engineering
Certificate in masonry- 2 years , walengwa darasa la 7 na kidato cha nne

Mwisho kutakuwa na masomo ya jumla kwa wanafunzi wote , kama computer application skills, entrepreneurship, Communicatio skills, professional ethics , life skills etc.

Ada haitazidi 550, 000 kwa kozi za miaka 2. Msihofu kuhusu ada kwani bado utaratibu unaandaliwa ni kiasi gani cha ada itozwe
 
Ukweli ni kwamba huwezi kuongelea maendeleo sehemu yoyote ile bila kutaja siasa.Nchi yoyote iliyoendelea duniani ina siasa safi, hivyo maendeleo ya kyela yatategemea sana chama kilichomadhubuti kufanya mabadiliko ya kweli. Ccm imedhihirisha kwamba haiwezi kuwaletea maendeleo watu wa kyela.Watu wa kyela tunajuhudi sana na ndio maana kila mwaka tunalima lakini kikwazo kikubwa ni watendaji.
 
....wana-Kyela tujilaumu sisi wenyewe,hatuna wa kumlaumu hapa. Tuliacha kuchagua mbunge ambaye angefanya kazi za ubunge wa Kyela,sisi tukamchagua muuza sura na siasa za kitaifa badala ya za kijimbo. Mwache apambane na kina Lowasa huko. Twasobile,kangi atungisa kwandisya ukusoba. Mgonile lelo bhakukaja!!?
 
Uvivu, ubishi na kupenda vya bure ndo tatizo lenu ninyi watu wa kyela hata akija malaika Gabreil kuwa mbunge wenu bado hataweza kuwafaa.Hadi sasa nadhani ni moja ya wilaya inayoongoza kwa kubadili wabunge mara nyingi kuliko wilaya nyingi nchini lakini bado mnalalamika. Hiyo barabara ijengwe kiwango cha lami ikiwa na manufaa gani kiuchumi au mnataka iwe barabara nzuri muendeshee vibaskeli vyenu vya mitumba? Ni kweli mnahitaji mabadiliko lakini anzeni kubadilika tabia zenu wenyewe mnaongoza kwa majungu Tanzania wanawake wenu kila siku ni sikukuu kutwa wameulamba watafanya kazi saa ngapi za kuwaletea maendeleo? Mnaomboleza msiba mwezi mzima sasa ikitokea misiba mitatu kijijini ina maana mwaka huo hamtavuna vimpunga vyenu maana mtalala msibani miezi yote.

Hamtaki mabadiliko pamoja na kuwa na mpunga mzuri kuliko mwingine nchini lakini mnaendeleza kilimo cha kumwaga mbegu kilichoandikwa katika biblia enzi za Yesu kristo. Anzeni kubadilika wenyewe na muombeeni mbunge wenu apone maana amepigana sana kwaniaba ya watanzania, mshaulini atoke huko kwa magamba aende kwenye upande wanaoelewa athali za ufisadi.

Ninamashaka kama wewe umeishi kyela muda mrefu na ninawasiwasi kama wewe unaijua vizuri barabara hiyo ambayo unasema haina manufaa.
Kwa ufupi mimi ni mwandisi kwa elimu katika mambo ya ujenzi wa barabara...moja ya kazi kubwa ya barabara ni usafirishaji wa mazao na watu. Kyela kuna kilimo kikubwa cha mpunga bei ya zao hilo ni chini na haliwakomboi wananchi kutokana na ubovu wa barabara hiyo inayoongeza gharama kubwa za usafirishaji, Matema beach ni eneo zuri sana la utalii lakini kutokana na ubovu ya barabara hiyo utalii umedorola kwa kiasi kikubwa. Huduma za umeme zinadolora kutokana na ubovu wa barabara hiyo, maendeleo sehemu yoyote ile duniani hutegemea sana ubora mzuri wa barabara...kipimo kimojawapo cha maendeleo sehemu yoyote ile hupimwa kwa barabara....tungekuwa na barabara nzuri kungekuwa na maendeleo na tungevutia sana walimu kwenda kufundisha katika shule zetu na kuongeza ufaulu katika shule zetu.mimi nadhani kwa jimbo la kyela "BARABARA KWANZA"

Ninyi ombeni kutengenezewa barabara ya kiwango cha kawaida tu siyo lazima lami maana matema beach ni watalii wangapi wanaoenda kwa mwaka? Hujui wewe hata maeneo yanayolima mpunga matema tujenge lami msafilishie vyungu na usipa?

Huna hoja mkuu zipo wilaya ma mikoa inazalisha na haina barabara ninyi mnataka upendeleo kwasababu naibu waziri anatoka kwenu hoja gani hiyo.

Nipe takwimu za uzalishaji na mchango wenu kimapato kwa mchi hii, maana rutile wakati vipaumbele viendane na uzalishaji na mchango katika pato la taifa. Kuna jamaa alijenga lami kwenda migombani akaacha mikoa na wilaya. Mnapenda majungu Kila uchaguzi mnabadili wabunge kuanzia Kasyupa,mwakipesile sasa nahuyu mwakyembe hamtaki aje nani inamaana ninyi miaka yote mnakosea?
 
Afrika namfahamu sana ni mpenda madaraka mno yaani ana uleunyakyusa hasa ni mtu ambaye huwa ashauriki hata kidogo.analololíamini yeye ndilo anataka liwe.na kama suala ni kuandika kitabu hyo itakuwa kwa manufaa yake na familia yake na wala si kwa wanakyela.kama unampigia debe tambua kuwa hapo hakuna mtu kaka jaribu mwingine.
 
mimi nilidhani baada ya kunikosoa basi wewe utaandika cha maana umeacha reality umeandika hisisa.Tembea nchi nzima uulize mchele wa kyela kama hutaambiwa kuwa huo ndio mchele bora. Mara ngapi serikali imeagiza mchele kutoka nje? Hivi wewe unadhani kama miundombinu ya kyela ingekarabatiwa tusingeweza kuzalisha mchele wa kulisha nchi nzima hivyo tungeondoa tatizo la chakula nchini.Tunahitaji barabara kuliko hayo maneno yako ya unafiki maana hayatatusaidia watu wa kyela.
 
Afrika namfahamu sana ni mpenda madaraka mno yaani ana uleunyakyusa hasa ni mtu ambaye huwa ashauriki hata kidogo.analololíamini yeye ndilo anataka liwe.na kama suala ni kuandika kitabu hyo itakuwa kwa manufaa yake na familia yake na wala si kwa wanakyela.kama unampigia debe tambua kuwa hapo hakuna mtu kaka jaribu mwingine.

Nilidhani unahoja za maendeleo ya Kyl kumbe wewe unamjadili Africar tu. Badala ya kutoa hojaunazungumzia mipasho kama mcheza taarabu. Inawezekana unakaa Temeke Mikoroshiniwewe.

Mimi nilimtaja huyu bwana kwa vile namfahamu na siongelei unafiki hapa kwaniningeweza hata kujiongelea mimi mwenyewe kama ninafaa kugombea hiyo nafasi.Kwani sina nina haki kikatiba?

Tunahitaji mabadiliko na tunahitaji watu wa kutuletea mabadiliko, hata weweunaweza kumtaja unayemfahamu nasi tumjadili hapa.

Maendeleo ya Kyl yanahitaji fikra hai, mfumo mpya wa kupanga mambo. Ngojanikueleze mambo ya maendeleo yanayotakiwa Kyela, pamoja na barabara ya Njiapanda - Ipinda - Matema Beach tunahitaji haya pia;

  1. Mbunge atakayeweka kipaumbele katika uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo kwa ajili ya usindikaji wa mafuta ya mawese na matunda yake (Enbosa) ili kutoa ajira kwa vijana.
  2. Tutahitaji mtu atakayefikilia kuanzishwa kwa chuo cha Ualimu kwa ajili ya vijana wetu wanaomaliza kidato cha nne na Sita
  3. Tunahitaji mtu atakayefikiria kuanzisha soko la Kimataifa pale Boda (Kasumulu) ili kuwazuia wafanyabiashara kutoka Malawi hadi DSM karibu km 1500 kufuata bidhaa ambazo zingepatikana pale Kasumulu
  4. Tunahitaji Mtu atakayeongoza harakati za kuanzishwa Benki wa Wananchi wa Kyela (Kyela Community Bank) ili kutatua matatizo ya mikopo wanayopata wafanyabiashara wadogowadogo na wakulima.
  5. Tunahitaji mtu atakayehakikisha hakuna kijana anayefaulu masomo anashindwa kusoma kwa kukosa karo ya shule.
  6. Tunahitaji mtu atakayehakikisha dagaa wetu kutoka ziwa Nyasa na mchele wa Kyl vinawekewa Trademark ili viuzwe kwa bei ya faida
  7. Tunahitaji mtu mwenye fikra ya kuanzisha chuo cha VETA
  8. Tunahitaji mtu mwenye fikra chanya kuwa shule Tatu za A-Level hazitoshi, hivyo kuhakikisha kunaongezwa shule zaidi za A-level
  9. Tunahitaji mtu wa kuwaonea huruma Madaktari wa Hospitali ya Kyela kwa kuwaboreshea majengo yale chakavu na kuwaongezea vifaa vya afya.
  10. Tunahitaji mtu atakayetenganisha kati ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya (Bomani) na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuweka mikakati wa kuzijenga upya ikiwa ni pamoja na nyumba zao za kuishi.
Endelea hapa..................................... hivi ndivyo tunavyovitakaKyl sio porojo na mipasho. upo?
 
Watabadilisha sana Wabunge,na wala barabara hiyo haitajengwa!

Mark my words..
MAN EATETH WHERE HE WORKETH! na MWAMBA NGOMA HUVUTIA KWAKE! Mwakyembe atumie tu wizara yake ya Ujenzi kulazimisha kujenga barabara hiyo. Ndivyo mawaziri wa fedha na ujenzi hufanya kujenga barabara za majimboni kwao. Angalia Mramba alipokuwa waziri wa fedha barabara ya rombo - tarakea ikaanza kujengwa, alipokuwa waziri wa miundombinu akaimalizia. Magufuli hadi alipindisha barabara kuu kutoka biharamulo akaipitisha jimboni kwake chato kuelekea bukoba ingawa ilikuwa hiyo ni barabara ya mkoa tu. Kawambwa baada ya kuukwaa uwaziri wa miundombinu, bagamoyo - msata ikaanza kujengwa kwa kasi. Mkullo baada ya kuukwa uwaziri wa fedha kilosa sasa lami zajengwa. Mahanga naye alipokuwa naibu waziri wa ujenzi akaamuru lami nyepesi ya barabara ya tabata - segerea - kinyerezi - majumba sita ing'olewe na iwekwe lami kamili, na kazi hiyo sasa imekamilika. Akaamuru barabara ya banana - kitunda ijengwe na tanroad ingawa ni barabara ya manispaa, akaanza na mradi wa daraja la vingunguti ingawa manispaa haikuwa na hela, akajenga kituo kikubwa cha mabasi segerea mwisho kwa kutumia tanroads. Ndiyo maana wananchi wa segerea wanampenda. NA MWAKYEMBE AFANYE HIVYO KABLA HAJATOLEWA WIZARA HIYO.
 
Back
Top Bottom