Habari wadau,
Mi ni mkazi wa Dar maeneo ya Gongo la Mboto (kipunguni) ambapo kuingia huko lazima ushuke Mombasa na upande vigari vinavyoingia ndani kuelekea moshbar.
Kwa hali ya wakazi wa maeneo hayo ni wengi sana-nafikiri ni moja kati ya maeneo yenye wakazi wengi sana hapa DAR, ikiifuatia Mbagala kwa karibu. Wakazai wa huku ndio waathirika wakubwa wa mabomu ya Gongo la mboto.
Toka nimepahafamu mahali hapo miaka ya 2006, kero kubwa imekuwa imekuwa ni barabara. Barabara ni ya vumbi isiyofanyiwa ukarabati wa aina yoyote ile. Si wakati wa mvua ama jua.
Kwa barabara hii ukiiona hutaamini kuwa uko mjini/jijini Dar, na kwa hapa huwa najiuliza, kama hapa-kilometa 16-18 tu hivi kutoka Ikulu panakuwa hivi, vipi huko majita -makojo Musoma kilometa zaidi ya 1000?
Nimekuwa nikisikitika sana unaposhuka Mombasa makonda wa daladala wanasema haya wale wa visiwani (kwa kuwa inaonekana ni kisiwa kilichojitenga). Magari yenyewe yanayoenda huko ni mabovu-nani atapeleka gari yake nzima huko?
Hata wenye magari binafsi magari hufa kila siku. Barabara hii ni chafu kwelikweli-mabonde, milima, mahandaki humo humo. Huwa najiuliza hivi huku hakuna mwenyekiti wa serikali za mitaa, diwani, mbunge, waziri na hta rais?
Ni barabara hii liliyomfukuza Makongoro Mahanga kugombea tena jimbo la Ukonga (2010) na kuligawa kuwa sehemu mbili. Nakumbuka wananchi wa kule walimwambia hawatampa kura hata moja kwa kuwa pamoja na kuwa alikuwa mbunge wao na waziri wa miundo mbinu hakuitilia maanani barabara ya jimboni kwake.
Sasa hivi kashika mama Eugene Mwaiposa ambaye pamoja na kumtumia rais Kikwete katika kujinadi wakati wa uchaguzi na agenda ya barabara hii kuwekwa mbele hata na rais mwenyewe-bado suala hili limekuwa ni kero-kero.
Mwaiposa mwenyewe kama ameonekana kupwaya katika hili na kujikita katika mabonanza na kutetea mikopo ya wabunge (Maslahi binafsi) badala ya maslahi ya wale waliomchagua.
Barabara inaendelea kuwa kero huku barabara nyingine zikiendelezwa kwa kasi ya ajabu kote jijini Dar, mfano Vingunguti, Tandika, Buza, Kipawa-Machimbo n.k.
Kwa maneno hayo ya machungu kwelikweli, nashawishika kufikiri kuwa hili suala la barabara yenye wakazi wanaokadiriwa kufika 200,000 (sehemu hii imemeza idadi kubwa ya iliyokuwa Kipawa, Majohe, Moshibar Kipunguni, kwa Mkolemba, Moshbar kwa diwani n.k) imekuwa "fupa lililomshinda fisi mbwa ataliweza"?
Lilimshinda mbunge wa kwanza Balozi Paul Rupia (1995-2000), mtu mwenye ushawishi mkubwa sana hapa nchini, Makongoro Mahanga (2000-2010)- waziri na mbunge na ikisemekana kuwa ni mtu wa karibu na mzee; na sasa Mama Mwaiposa ataliweza?
Kwa ujumla wanachi wanateseka-(naombeni tu niseme ukweli), na ni kama vile wametupwa na viongozi wao, hawana mtetezi na hawana pa kusemea. Hawajui nini kinaendelea, ikiwa kuna mtu humu ndani ana tetesi zozote, au habari zozote zenye uhakika atujuze tafadhali, tumo gizani na mateso yanazidi kuwa makali kila kukicha. Ukisomasoma kwenye magazeti hupati habari yoyote kusus hili.
Mwisho niwape pole wakazi wote wanaotegemea barabara hii, yenye umbali wa kilometa kama tatu-nne tu hivi, mwendo wa dk 5-10 tu hivi, lakini habari yake mmmh.
Nawasalisha.