Barabara ya Banana - Kitunda ni kero kubwa kama vile hatuna viongozi wanaotusimamia

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Barabara ya Banana Kitunda (Dar es Salaam) imekuwa ni kero kubwa sana kama vile hatuna viongozi wanaotusimamia.

Barabara ni mbovu na kila kipindi cha mvua usafiri ni shida na magari yanaharibika sana, tunaomba hii taarifa imfikie Mbunge wetu ni Jerry Silaa.
 
imfikie Mbunge wetu ni Jerry Silaa.
Imfikie ndio Ila endeleeni Kula vumbi ana mambo mengi hivi hamna madiwani au hamkuwachagua? Hamjawahi kuwahoji hao madiwani mliowachagua wanafanya kazi gani hapo kwenu? Mmekaa barabara mbovu wao wapo tu wanawaangalia?
 
Huku maeneo ya Ulongoni Gongo la Mboto, miaka michache nyuma ilikuwa kero kubwa sana kuishi, barabara mbovu za vumbi, madaraja yote ya mto msimbazi yalikuwa yamevunjika, hilo lote ni Jimbo lake, sijajua huko tatizo linalokwamisha ni nini?
 
Mbunge,waziri manenoooo mengiiii
Kutwa kutembea na madokomaa tu


Ova
 
Barabara ya Banana Kitunda (Dar es Salaam) imekuwa ni kero kubwa sana kama vile hatuna viongozi wanaotusimamia.

Barabara ni mbovu na kila kipindi cha mvua usafiri ni shida na magari yanaharibika sana, tunaomba hii taarifa imfikie Mbunge wetu ni Jerry Silaa.
Mbunge wenu anakuna pumb.u tu anasema hata akipitidha greda Bado mvua zinanyesha zitaharibu tena
 
Zamani Barabara hiyo ilikuwa na lami kutokea barabara ya Pugu road Banana mpaka Kitunda, baada ya kuharibika sana na kutengeneza mashimo makubwa waliamua kuikwangua sehemu kubwa lakini zipo sehemu chache bado zina lami..
 
Kwanini mmejenga sehemu ambayo haina lami?

Kwani kuna aliyelazimishwa kwenda kujenga huko?

Dar ina maeneo mengi yenye lami. Mngeenda huko!
Umenikumbusha nukuu ya zamani ya yule binti wa Mfalme wa Ufaransa aliyekuwa anashangaa wananchi wanaandamana kwa sababu bei ya Mkate imepanda. Akauliza kwa mshangao "Kwa nini wasile Keki badala ya Mkate kama umepanda bei?" "Let them eat cake" in original French "Qu'ils mangent de la brioche"
 
Mtoa hoja umekuja kulalama humu, why usifanye push back na wenzako, fanyeni service delivery protest, fungeni hiyo barabara kwa saa 1 tu, wote kuanzia RC comedian atakuja kuwasikiliza, hii ndio lugha pekee wanayoweza kusikiliza hawa viongozi wetu, kulalama humu hakutakusaidia chochote
 
Back
Top Bottom