Barabara na madaraja kubomoka, ukaguzi na ukarabati unafanyika kwa wakati?

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Kama wengi tulivyoshuhudia na mitandao mingi inavyoripoti hali ya mafuriko ni mbaya na athari kubwa ni barabara na madaraja kuharibika vibaya kiasi ya njia nyingi kufungwa kwa tahadhari.

Kama tunavyofahamu, tumepata mvua mfululizo na inawezekana matokeo ya leo si sababu ya mvua iliyonyesha leo bali uharibifu kufanyika kidogo kidogo.

Ni vizuri mamlaka zetu ziweke utaratibu wa kukagua barabara na hasa madaraja kuona ustahimivu wake kadri mvua zinaponyesha ili kama kuna athari zilizoanza zirekebishwe kabla ya matokeo makubwa zaidi.

Tanroads na mamlaka zingine ni vizuri wawe wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara utasaidia sana kuimarisha madaraja yetu ambayo wakati mwingine yanaharibika kidogo kidogo kabla ya kushindwa kabisa kuhimili mvua kubwa.

Janga halipigi hodi lakini ukaguzi na ukarabati kila baada ya mvua kubwa ingepunguza athari tunazoona zimetokeo leo maeneo mengi.

Sasa ni wito kwa serikali kufanya ukaguzi mkubwa haraka kabla mvua nyingine kubwa haijasomba barabara na madaraja yaliyosalia tukaingia hasara kubwa.
 
Madaraja mara nyingi hukaguliwa baada ya ujenzi ili kuidhinishwa kwa matumizi, bahati mbaya baada ya hapo hakuna ukaguzi unaofanyika kila mara ili kuangalia uimara wa madaraja husika, wao ni kama vile wakishakagua mara moja huamini madaraja hayo hayawezi kuharibika kamwe mpaka muda uliowekwa ufike.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kuna madaraja ustahimivu wake hauwezi kuhimili mvua nyingine kama ya jana. Focus isiwe kwenye madaraja na barabara zilizobomoka tu!

Ni vizuri ziundwe timu mbili tofauti za kufanyia kazi sehemu zilizokwisha haribika na nyingine wafanye kazi ya kuimarisha maeneo yanayoelekea kukosa ustahimivu.
 
Madaraja mara nyingi hukaguliwa baada ya ujenzi ili kuidhinishwa kwa matumizi, bahati mbaya baada ya hapo hakuna ukaguzi unaofanyika kila mara ili kuangalia uimara wa madaraja husika, wao ni kama vile wakishakagua mara moja huamini madaraja hayo hayawezi kuharibika kamwe mpaka muda uliowekwa ufike.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ni kweli maana kuna daraja limebomoka mbweni jkt lakini kama ukipita pale taratibu siku za karibuni kwa umakini ungegundua linaelekea kuathirika na niliwahi kusimama na kuchungulia hadi chini kuona hali ilivyokuwa! Ningeandika hapa nisingeeleweka ila sasa limesombwa lote.
 
Kwasasa inabidi JWTZ waokoe jahazi ili jumatatu mji usisimame.
 
Wakuu,

Kama wengi tulivyoshuhudia na mitandao mingi inavyoripoti hali ya mafuriko ni mbaya na athari kubwa ni barabara na madaraja kuharibika vibaya kiasi ya njia nyingi kufungwa kwa tahadhari.

Kama tunavyofahamu, tumepata mvua mfululizo na inawezekana matokeo ya leo si sababu ya mvua iliyonyesha leo bali uharibifu kufanyika kidogo kidogo.

Ni vizuri mamlaka zetu ziweke utaratibu wa kukagua barabara na hasa madaraja kuona ustahimivu wake kadri mvua zinaponyesha ili kama kuna athari zilizoanza zirekebishwe kabla ya matokeo makubwa zaidi.

Tanroads na mamlaka zingine ni vizuri wawe wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara utasaidia sana kuimarisha madaraja yetu ambayo wakati mwingine yanaharibika kidogo kidogo kabla ya kushindwa kabisa kuhimili mvua kubwa.

Janga halipigi hodi lakini ukaguzi na ukarabati kila baada ya mvua kubwa ingepunguza athari tunazoona zimetokeo leo maeneo mengi.

Sasa ni wito kwa serikali kufanya ukaguzi mkubwa haraka kabla mvua nyingine kubwa haijasomba barabara na madaraja yaliyosalia tukaingia hasara kubwa.
Chini ya ccm tutaendelea kuumia tu maana yanafika na yatapita kama mengine tu
 
Serikali yetu ikishajenga ndio shughuli imeishia hapo, walau kidogo miundombinu ya reli huwa inafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara...
 
Ni kweli maana kuna daraja limebomoka mbweni jkt lakini kama ukipita pale taratibu siku za karibuni kwa umakini ungegundua linaelekea kuathirika na niliwahi kusimama na kuchungulia hadi chini kuona hali ilivyokuwa! Ningeandika hapa nisingeeleweka ila sasa limesombwa lote.
Baada ya kugundua hilo u likwenda Tan road kutoa taarifa au umekimbilia jf?
 
Tuna Maafisa wa Uhandisi ambao wametanguliza Uboss kufunga Tai, Suti na kukaa Maofisini kulea Vitambi na kufukuzia Madeal ya pesa.
Siku Mainjinia Wetu wakibadilika na Kushinda Site kuona kazi zao zilizofanya wakaajiriwa Nchi itabadilika.
TARURA ovyo kabisa, barabara za Mtaani zenye Uwezo wa kupitisha Tani 10 yanapita Malori makuuuubwa Tani 45+. Mfano pale Mchicha barabara ya kwenda Fire, barabara ya Mnyamani, Vingunguti Baracuda.
Tumeruhusu BANDARI KAVU (ICD) kujengwa mpaka vichochoni malori yanapenya na kuvunja tubarabara twetu ambako huenda wanamtaa tulijichanga, Nchi inajiendea tu kama mgari mbovu usio na breki.
Wenye pesa wanafanya watakalo, wenye malori wanapita Barabara yoyote na hakuna mamlaka inakemea madaraja na barabara vitapona?
Uchimbaji mchanga kwenye mito unafanyika mchana jamii inaona wala haikemei what a shame!
We need a social reform, hatujitambui kama jamii na kama Nchi sio raia wala Viongozi.
 
Kwani kazi ya jwtz ni kujenga madaraja?
Tuna jeshi la Zimamoto na uokoaji lakini hata wananchi wenyewe wanafikiri kazi yao ni moto tu lakini eneo la uokoaji bado wapo nyuma sana.
 
Tuna Maafisa wa Uhandisi ambao wametanguliza Uboss kufunga Tai, Suti na kukaa Maofisini kulea Vitambi na kufukuzia Madeal ya pesa.
Siku Mainjinia Wetu wakibadilika na Kushinda Site kuona kazi zao zilizofanya wakaajiriwa Nchi itabadilika.
TARURA ovyo kabisa, barabara za Mtaani zenye Uwezo wa kupitisha Tani 10 yanapita Malori makuuuubwa Tani 45+. Mfano pale Mchicha barabara ya kwenda Fire, barabara ya Mnyamani, Vingunguti Baracuda.
Tumeruhusu BANDARI KAVU (ICD) kujengwa mpaka vichochoni malori yanapenya na kuvunja tubarabara twetu ambako huenda wanamtaa tulijichanga, Nchi inajiendea tu kama mgari mbovu usio na breki.
Wenye pesa wanafanya watakalo, wenye malori wanapita Barabara yoyote na hakuna mamlaka inakemea madaraja na barabara vitapona?
Uchimbaji mchanga kwenye mito unafanyika mchana jamii inaona wala haikemei what a shame!
We need a social reform, hatujitambui kama jamii na kama Nchi sio raia wala Viongozi.
Hilo la ICD ni jipu ...
 
Ni kweli maana kuna daraja limebomoka mbweni jkt lakini kama ukipita pale taratibu siku za karibuni kwa umakini ungegundua linaelekea kuathirika na niliwahi kusimama na kuchungulia hadi chini kuona hali ilivyokuwa! Ningeandika hapa nisingeeleweka ila sasa limesombwa lote.
Bahati nzuri mvua imenyesha weekend, kama ingenyesha katikati ya wiki ndio hali ingekuwa mbaya zaidi, huo uharibifu ungeleta usumbufu mkubwa kwa wengi.

Inabidi sasa mamlaka husika ziamke, wasisubiri kufanya mambo kwa style ya zimamoto, kama ambavyo wamezoea kusafisha mitaro misimu ya mvua ikikaribia, tofauti na hapo wataiacha ibaki na uchafu siku zote, kama ikija mvua ya ghafla, maji yote yanaishia barabarani.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Serikali yetu ikishajenga ndio shughuli imeishia hapo, walau kidogo miundombinu ya reli huwa inafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara...
Reli ya kati nao kuna kipande cha Kilosa,Morogoro kila mwaka ikinyesha mvua lazima palete shida.Juzi walitangaza kuwa wamesitisha safari za treni kwa Mikoa nane!
Reli ya Tazara ndiyo huwa ipo safe!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Hili Nina uhakika ni pigo Kwa mdomo ulioropoka Jana wakati Makonda anajivuna kutoa matingatinga 20 kuimarisha mabarabara Sasa Mungu kajibu
Na Bado mengi yanakuja

Tuombe rehema na kutubu
 
Duh ..
 
Back
Top Bottom