DOKEZO Bandari ya Ujiji imedumaa tofauti na matarajio yetu wana Kigoma Ujiji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Chiston junior

New Member
May 7, 2021
4
28
Bandari ya Ujiji imedumaa tofauti na matarajio yetu wana Kigoma Ujiji.


Kuna suala la Bandari ya Ujiji Kigoma tunaomba Serikali itusaidie Wananchi wa Kigoma Ujiji ,Bandari ya UJIJI haileta matarajio kama ilivyotarajiwa kutokana na kasoro kadhaa.

Bandari ya Ujiji ni bandari ya tatu kwa ukubwa baada ya bandari ya Kigoma na Kibirizi . Bandari ya Ujiji inajengwa na mkandarasi China Railway 5th Group Cooperation,mradi huu ulianza tangu Machi 2019 kwa gharama za Bil.32. Serikali tayari imeruhusu Maboti kuanza kazi katika bandari hiyo kwenda maeneo ya Sibwesa,Mgambo,kalilani na Kalia ila hadi sasa wamiliki wa Maboti wamekataa kupeleka Maboti yao katika bandari yetu hiyo kutokana na kasoro zilizopo katika Bandari ya UJIJI .Ni boti moja tuu ambalo linafanya kazi kwa wiki mara moja. Kasoro zilizopo ni hizi.

1.Kina cha Bandari ya UJIJI ni kidogo chenye uwezo wa kubeba boti ya chini ya tani 30 tuu na sio zaidi ya hapo , jambo ambalo wamiliki wa Maboti wamedai hiyo ni kasoro ambayo hawawezi peleka Maboti yao hapo sababu Maboti yao yana beba hadi tani 60 na zaidi. Kubeba chini ya tani 30 ni kupata hasara .

2. Gati la Bandari ya Ujiji ni dogo ,haliruhusu boti zaidi ya 3 , mwisho ni boti tatu tuu . Hivyo eneo la Maboti kupaki na kupakia na kushusha mizigo ni dogo sana sio zaidi ya boti 3. Jambo ambalo ni kasoro kubwa.

3.Bandari ya Ujiji haina uzio wa kuzuia upepo , hivyo wamiliki wa Maboti wanaepuka boti zao kupasuka kutokana na upepo,ukizingatia boti zinazotumika ni za Mbao .

4.Bandari ya UJIJI ina tozo nyingi ,kwa mizigo inayo safirishwa jambo linaloongeza gharama za usafiri kwa mizigo inayokwenda Sibwesa, Kalia ,Mgambo , Kalilani ,kaparamsenga hivyo watu wanaamua kukimbilia usafiri wa njia ya Gari (basi) na kuepuka usafiri wa boti kutokana na uwepo wa gharama kubwa.

5.Serikali inalazimisha boti zote zinazotaka kuhudumia bandari ya Ujiji ziende safari za ndani tuu kama Kalia,Mgambo , Kaparamsenga,Kalilani ,Sibwesa ikiwa maeneo hayo sasa hivi yana ushindani mkubwa wa magari na mabasi ambayo yanakwenda huko .

Maboti kutoka Ujiji yapewe pia safari nyingine za nje kwenda Kalemii -Kongo ,sababu ni rahisi sana kwenda Kalemii kutokea Ujiji kuliko kutokea Kibirizi .Maboti ya Kibirizi safari zake za nje ziwe Bujumbura ,Uvira na maeneo mengine.

6.Bandari ya Ujiji haina jengo la Utawala . Yaani kuna Jengo la kuhifadhia mizigo , Jengo la kupumzika abiria ila hakuna Jengo la Utawala ,hivyo hakuna Ofisi za uhamiaji ,askari maji wala Ofisi yeyote. Hata hayo majengi mengine yaliyojengwa yapo chini ya kiwango.

Serikali kupitia wizara ya uchukuzi na mamlaka ya Bandari (TPA)ichukue suala hili la kasoro Bandari ya Ujiji kwa uzito wake na kulifanyia kazi . Bandari ya Ujiji ni muhimu sana kwa Maendeleo ya Mji wa Ujiji na Kigoma kwa ujumla ili kuongeza shughuli za kiuchumi .
IMG-20231008-WA0004.jpg
 
Yaani, boti zenu za mbao zinabeba tani 60? Kweli? Ndo hizo hizo zinazohitaji kina cha mita 60???
 
Back
Top Bottom