Balozi Ombeni Sefue amrithi Luhanjo

Historia ni kitu muhimu na hayo yote yalioandikwa amepitia labda grom primary school to whatever japo kwa upande mwengine si msingi..Kwa mujibu wa jarida la Dagnyheter (Uswidi)jamaa yuko makini kiutendaji Watanzania tuumpe mda si kila samaki alekuwepo kwenye tenga kaoza kama harufu inavyonuka wengine wanafaa kuwa ng onda na wakalisongesha
ALLAH BARIK TANZANIA NA WATU WAKE NA SI MAFISADI

Huyo Bw. is good! Believe me wana JF. Cha msingi tumpe muda atende kazi zake.
 
He is now exposed to the large public. Who is this guy again? What is he going to do for this country?
 
KATIBU Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ni Manataaluma ya Dipromasia ambaye tokea Agosti 31, 2010, amekuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
Kabla ya kuteuliwa kwenda kuwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Balozi Sefue, alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani katika mji wa Washington DC tokea Juni 15, 2007. Na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, nafasi aliyoishikilia tangu Oktoba 2005 hadi Juni 2007.Sefue, pia amewahi kuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden katika Mji wa Stockholm kati ya mwaka 1987 na 1992.

Kati ya mwaka 1993 na 2005, Sefue, alikuwa ni mwandishi wa hotuba na msaidizi binafsi wa Marais wawili, Rais Ali Hassan Mwinyi (1993-1995) na Rais Benjamin Mkapa (1995-2005).


Miongozni mwa mambo mengine, Balozi Sefue alimsaidia Rais Mkapa wakati alipikuwa Kamishna wa Afrika (kwenye Kamisheni ya Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, akiwa ni Tony Blair), ambapo alitoa ripoti iitwayo, ‘Our Common Interest, Ripoti of the Commission for Africa', mwezi Machi mwaka 2005, na pia alishiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za G8, ambao ulijadili ripoti hiyo ambao ulifanyika Gleneagles, Scotland mwezi Julai mkwa 2005.

Aidha Balozi Sefue, alifanya kazi na Rais Mkapa wakati Mheshimiwa Mkapa alipokuwa Mwenyekiti mwenza wa Kamisheni ya Shirika la Kazi Duniani ya ILO World Commission, iliyojadili masuala ya Kijamii ya Utandawazi kati ya mwaka 2002 na 2004, ambapo alishiriki katika maandalizi ya ripoti ya Kamisheni hiyo iitwayo, A Fair Globalisation Creating Opportunities For All, iliyotolewa mwzi Februari mwaka 2004.
Balozi Sefue, alipata Elimu yake ya Juu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe (ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Mzumbe) katika masuala ya Utawala mwaka 1997.Pia alipata Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sera na Utawala kutoka Institute of Social Studies (ISS) mjini The Hague, Uholanzi mwaka 1981.
Alipata Diploma ya Juu katika Chuo cha Diploma cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1986
, na pia Balozi Sefue alimuoa Mama Anita M. Sefue na anawatoto wawili. Mia

Ukinisaidia kuuelewa huo mpango wa elimu hapo ntashukuru
 
Samahani, unaweza kutoa ufafanuzi kidogo juu ya hili maana nilikosa huo mjadala.

Nakumbuka tulijadili nguvu aliyokuja nayo Prof. Tibaijuka wizara ya ardhi kuwa atabomoa structures zote zilizojengwa viwanja vya wazi, kwenye ardhi ya taasisi za serikali zilizovamiwa, rushwa kwenye vizara etc. Tukasema kuwa mama wewe ni msafi lakini as long as umekuja kwenye genge la CCM, mafisadi , you will never go against your boss's instructions. Kuwa vimemo vitakushinda. Kweli na sasa ulibomolewa ukuta mmoja tu, kwisha habari yake!!!! Ni hiyo Mchambuzi. Na Ombeni hatakuwa nje ya ushirika huo wa vimemo!!!
 
Wanaomudu kazi hizi ni walewale. Atatoka Washington atakwenda New York, atatoka New York atakwenda Ikulu. Akitoka Ikulu atagombea Ubunge. Akipata Ubunge atakuwa Waziri wa mambo ya nje! Yaani ni kama vile WATANZANIA wengine hatupo au hatujawahi kuwepo. KUmbe serikali nayo ina wenyewe!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huyu mzee si inabidi awe amestaafu tangu August? Au kaongezewa mkataba wa ulaji? Alizaliwa august 1954!
 
Atleast hapo Jk kateua.

Unaweza kuleta mrejesho sasa baada ya zaidi ya miaka Tatu Ikulu kama Katibu Mkuu Kiongozi au unaweza hata kusema neno mmoja!

Uteuzi huu umenifanya ni waze hali ya sasa -wakati Raisi Magufuli akiumiza kichwa kutafuta Mawaziri wa Baraza lake jipya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom