Balozi Maajar and REX Attorneys

niliwaambia - matawi ya watanzania UK, sijuii Moscow wote ni mafisadi. badala ya kuzichanga za huko wazilete wao wanakaba penalti za nyumbani. na michuzi yuko karibu nao sana inawezekana ni shunter wa pesa. yeye kila siku kitaa!
 
Kwani si kulikuwa na wakati huyu mama aliomba kwa president aachane na ubalozi ili kafanye kazi kwenye hiyo law firm yake na president alikataa resignation yake??
Maybe hataki kuachia position yake sbb anaona inamlipa sana kuliko huo ubalozi.
 
Kwa mujibu wa thread iliyoanzishwa na Vuvuzela hivi leo, kampuni ya mawakili ijulikanayo kwa jina la Rex Attorneys, iliwahi kuwa mwakilishi wa Richmond Development Corporation(RDC) hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, ni dhahiri kampuni hiyo ilikiuka miiko ya taaluma (profession misconduct), kwa kuwakilisha TANESCO katika kesi ambayo ilifunguliwa dhidi yake na kampuni iliyorithi mkataba wa mteja wake wa zamani. Nakaribisha maoni zaidi katika suala hili.
 
Duuu, hii sasa kali.

Itabidi TANESCO WAKATE RUFAA na watu fulani washitakiwe kwa kuipa kazi hii kampuni.

Hapa kama ni kweli itakuwa ni USANII wa hali ya juu.

Tuwakamate hawa jamaa na tuwatandike watuambie DOWANS ni nani na Richmond ni nani.
 
kaka hapo ilikua hakuna kesi,hawa watu wana genge lao la kifisadi!tulipo kataa kununua mtambo kwa 50bn wakaamua kupata watakacho 185bn watu ni walewale!
 
Kama kweli hii ni kali. Wanataaluma kama hawa waliobobea katika mambo ya sheria walitakiwa walifahamu hili.

REX Attorneys
 
How did it end with with Rex Attorneys? Hii ni kampuni ya wakubwa na pengine wengine wana maslahi na Dowans. What suprises me ni kuona kwamba issue ya Dowans wakuu wetu wanaichukua kwa urahisi sana. Ni kweli ni issue rahisi kama wanavyotueleza? Kama ndivyo Tanzania kuna mambo marahisi mangapi?
 
Kwa mujibu wa thread iliyoanzishwa na Vuvuzela hivi leo, kampuni ya mawakili ijulikanayo kwa jina la Rex Attorneys, iliwahi kuwa mwakilishi wa Richmond Development Corporation(RDC) hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, ni dhahiri kampuni hiyo ilikiuka miiko ya taaluma (profession misconduct), kwa kuwakilisha TANESCO katika kesi ambayo ilifunguliwa dhidi yake na kampuni iliyorithi mkataba wa mteja wake wa zamani. Nakaribisha maoni zaidi katika suala hili.

Sasa hapo mkuu umegusa kwenye kisogo manake unamtafuta ubaya yule mama Maajar balozi wetu kule USA!! Manake yeye ni partner wa hiyo REX Attorneys.....who knows may be amepelekwa jikoni kufungisha midomo watu huko USA
 
Sasa masihara! Namhagiza AG mwaka huu nimechangia kodi kubwa hapa nchini. Natoa tamko mkiwalipa hawa wahuni,kodi yangu msiiunganishe,itenge tafadhali,ela iyo nimeilipa kodi badala ya kuvuja jasho. Tafadhali tafadhali. Ukienda kulipa waambie wakurudishie change ambayo ni kodi yangu,irudishe kwenye consolidated fund niendelee kuchangia mshahara wa rais. Sitorudia,nimeeleweka!
 
Nothing is more destructive of respect for the government and the law of the land than passing laws which cannot be enforced. Hawa Rex Attorneys hawakujua hili la profession misconduct?
 
Kwa mujibu wa thread iliyoanzishwa na Vuvuzela hivi leo, kampuni ya mawakili ijulikanayo kwa jina la Rex Attorneys, iliwahi kuwa mwakilishi wa Richmond Development Corporation(RDC) hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, ni dhahiri kampuni hiyo ilikiuka miiko ya taaluma (profession misconduct), kwa kuwakilisha TANESCO katika kesi ambayo ilifunguliwa dhidi yake na kampuni iliyorithi mkataba wa mteja wake wa zamani. Nakaribisha maoni zaidi katika suala hili.

Na baada ya kazi nzuri ya kuiwakilisha vema Kampuni tata ya Richmond Development Corporation ambayo pia inadaiwa kuwa na mkono wa ikulu yetu, Mhe Kikwete aliweza pia kumteua mwanasheria mwandamizi wa Rex Attorneys, Mama Maajar kwenda kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Mpaka leo, inashangaza kwamba hata magazeti ya uchunguzi nchi hayajaweza kusema lolote kuhusu uteuzi huo kama una uhusiano wowote na kutoa asante kwa mama mwanasheria huyo au hapana.

Mama Maajar waliapishwa na Mapuri siku moja ikulu kuanza kazi wakati mwenzie akielekea Uchina.
 
Mbona hakuna majina ya wamiliki kwenye hiyo website yao?!!

hujaangalia vizuri wote wamo humo. Nguluma, Sinare, Majaar Rwechungura. Kuna pia sina hakika mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Makani(labda ni jina tu) ila kama ni yeye anatakiwa atoe maelezo ya kina.
 
Back
Top Bottom