ABEDNEGO CHARLES
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 567
- 104
Balozi Job Lusinde ni ndugu wa mzee John Samuel Malecela, lakini pia ni waziri wa kwanza wa serikali za mitaa nchini, mmoja wa watu wawili tu waliobakia waliokuwepo kwenye baraza la kwanza la mawaziri mara tu baada ya uhuru 1962 na waziri pekee aliye hai aliyeshiriki uwekwaji sahihi wa hati ya Muungano(Article of union) 1964 wakati huo akiwa Waziri wa mambo ya ndani.
Mwaka 1971 alifukuzwa kazi na Rais Nyerere kwa kosa la kuweka lami kipande cha barabara iliyokuwa inaingia ikulu. Balozi Lusinde alikuwa amemweleza mwl kuwa barabara hiyo ni muhimu ikawekwa lami kwakuwa kuna wageni wengi walikuwa wakifika ikulu na tayari wengine walikwisha ilalamikia kwa ubovu wake. Nyerere alikataa kwa maelezo kuwa kodi ya Mtanzania haipo kwa ajili ya kujenga lami ya Rais, kodi ya Mtanzania ipelekwe mashuleni na mahospitalini na sio vinginevyo.
Baada ya mzee Lusinde kushindwa kumshawishi mwl, alisubiri mwl aende ziara nje ya nchi na yeye akaamua kumwaga lami. Kilichompata baada ya mwl kurudi alishangaa kupigiwa simu na secretary wa Rais aliyemtaka afike ikulu anaitwa na Rais, Alikarimiwa kwa chai na biscuit na kisha secretary akam despatch na kumkabidhi barua ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kuwasaliti watanzania. Alirudishwa kazini baadaye alipoomba radhi na kupelekwa China. Kabla ya kumpeleka China mwl alimwambia mzee Lusinde ahamie ikulu maana anapenda sana lami na yeye Mwl akahamia magomeni.
Haya ni masimulizi ya balozi Job Lusinde mwenyewe wakati akihojiwa na ITV. Kosa alilofanya mzee Lusinde, hali ingekuwaje leo km angefanya kosa km hilo?