Balozi Job Lusinde na kibano cha Mwl Nyerere 1971

ABEDNEGO CHARLES

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
567
104
Balozi Job Lusinde ni ndugu wa mzee John Samuel Malecela, lakini pia ni waziri wa kwanza wa serikali za mitaa nchini, mmoja wa watu wawili tu waliobakia waliokuwepo kwenye baraza la kwanza la mawaziri mara tu baada ya uhuru 1962 na waziri pekee aliye hai aliyeshiriki uwekwaji sahihi wa hati ya Muungano(Article of union) 1964 wakati huo akiwa Waziri wa mambo ya ndani.

Mwaka 1971 alifukuzwa kazi na Rais Nyerere kwa kosa la kuweka lami kipande cha barabara iliyokuwa inaingia ikulu. Balozi Lusinde alikuwa amemweleza mwl kuwa barabara hiyo ni muhimu ikawekwa lami kwakuwa kuna wageni wengi walikuwa wakifika ikulu na tayari wengine walikwisha ilalamikia kwa ubovu wake. Nyerere alikataa kwa maelezo kuwa kodi ya Mtanzania haipo kwa ajili ya kujenga lami ya Rais, kodi ya Mtanzania ipelekwe mashuleni na mahospitalini na sio vinginevyo.

Baada ya mzee Lusinde kushindwa kumshawishi mwl, alisubiri mwl aende ziara nje ya nchi na yeye akaamua kumwaga lami. Kilichompata baada ya mwl kurudi alishangaa kupigiwa simu na secretary wa Rais aliyemtaka afike ikulu anaitwa na Rais, Alikarimiwa kwa chai na biscuit na kisha secretary akam despatch na kumkabidhi barua ya kufukuzwa kazi kwa kosa la kuwasaliti watanzania. Alirudishwa kazini baadaye alipoomba radhi na kupelekwa China. Kabla ya kumpeleka China mwl alimwambia mzee Lusinde ahamie ikulu maana anapenda sana lami na yeye Mwl akahamia magomeni.

Haya ni masimulizi ya balozi Job Lusinde mwenyewe wakati akihojiwa na ITV. Kosa alilofanya mzee Lusinde, hali ingekuwaje leo km angefanya kosa km hilo?
 
Katika zote hii nimeipenda mno na nahisi yule mtu ni mtakatifu wa kweli vision ya mwalimu ilikuwa ikifanana na thread yangu niliyoanzisha humu yenye kichwa cha habari hatuna maji watoto wanakaa chini madarasani flyover za nini?
 
UCOMMUNIST UMEISHIA WAPIIII! ILIKUWA SAFI SANAAA! Tatizo vyama vya siku hizi vyote ni CAPITALIST TUUU! Communist aliebaki Babu Kingungee nae naona kaamua kuwa Capitalist tuu.
 
Vijana wa siku hizi kazi yao kucopy na kupaste tu hata makosa ya wazi wazi wanashindwa kuyasahihisha!! NCHI YA TANGANYIKA ILIPATA UHURU WAKE MWAKA 1961!! sio 1962!
 
Tuwanasubiria waje akina nanihii na matusi na kejezi zao dhidi ya Mwalimu...
 
vijana wa siku hizi kazi yao kucopy na kupaste tu hata makosa ya wazi wazi wanashindwa kuyasahihisha!! Nchi ya tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961!! Sio 1962!

Ohoo wewe ndio utapata sifuri.........tulikuwa jamhuri lini?
 
Vijana wa siku hizi kazi yao kucopy na kupaste tu hata makosa ya wazi wazi wanashindwa kuyasahihisha!! NCHI YA TANGANYIKA ILIPATA UHURU WAKE MWAKA 1961!! sio 1962!
Labda ana maanisha Lusinde alikuwa waziri mwaka 1962
 
Ohoo wewe ndio utapata sifuri.........tulikuwa jamhuri lini?

Ile cabinet ya kwanza iliyowajumuisha wakina JAMAL,BRYCESON, TEWA, BOMANI ,LUSINDE NA ERNEST VASSEY haikuwa mwaka 1961? Ebu nipe shule hapo kama nimekosea! Una maana hatukuwa na Cabinet mpaka tulipokuwa Jamhuri?
 
Vijana wa siku hizi kazi yao kucopy na kupaste tu hata makosa ya wazi wazi wanashindwa kuyasahihisha!! NCHI YA TANGANYIKA ILIPATA UHURU WAKE MWAKA 1961!! sio 1962!

Mkuu naona unataka tu kuleta ubishani na ushindani wa kitoto. Mtoa mada kasema "... mara tu baada ya uhuru 1962..."

Hakusema Uhuru ndiyo ulipatikana 1962. Wote tunajua Uhuru ulipatikana 09/12/1961. Kwa akili na mahesabu ya haraka haraka, ukiwa GT, utakubaliana na mimi kwamba, uhuru ulipatikana kuelekea mwishoni mwa mwaka (1961) na hivyo, neno mara baada ya uhuru, lingemaanisha majuma kadhaa baadaye (majuma kama 3) ingeangukia 1962!
 
...........alikuwa ni rafiki wa karibu na Mwl. Nyerere na hakuwa serious kwa kumfukuza na kumrudisha... wapo ambao aliwatimua na hawakurudi tena mpaka leo ......... wengine walichapwa viboko kwa tuhuma za rushwa
 
Back
Top Bottom