BAKWATA, Clouds FM huko mwendako siko!As-Salamu Alaykum

Angekua anatoa salaam ya 'Bwana Yesu Asifiwe" waislam wangetishia kuandamana kupinga hiyo salaam.

wakiristo wamekaa kimya bila ya kuongea neno
kwa clouds fm kueneza udini kwa kuweka vipindi vya kuamasisha udini
sajawai kusikia wanasema Kristu......tumain letu
Je kwa nini serikali iko kimya kwa clouds fm kueneza udini?
 
Clouds na Kibonde kwa ujumla huwa hawavaliagi njuga ishu kama inawahusu waislam kupotoka kwa kuhofia ofisi zao kulipuliwa.
Mfano ishu ya yule mahabusu kuachiliwa baada ya waislam kutoa tamko.

Lakini kwasababu wanajua wakristu ni mafala na ni wa kupelekwa kama makondoo, huwa wanatumia kila lugha ya kuwakashifu,,, na wakristu hawatoi tamko lolote.

Hata ze komedi huwa wanadhihaki nyimbo za waimbaji wa dini, mfano ule wimbo wa Rose Mhando, wa Nibebe,,Joti alionekana kuvaa kama chizi akimwakilisha YESU KRISTu, lakini waumini wa kikristu tumejawa upendo wa uvumilivu.

Haitatokea hata siku moja ze komedi wakaigiza nyimbo ya kaswida, kwasababu wanajua hawa ndugu zetu hawachelewi kujitoa mhanga kwenye ofisi zao.
 
mkuu naomba ufanye kuhusisha hizo sentensi mbili zenye red colour.Nadhani utakua umeshajua ni kwanamna gani unajichanganya katika mada yako na kwamba unatolea hukumu jambo ambalo hujalielewa TAMBUA KWAMBA UISLAMU SI KUJIONYESHA KAMAULIVYO SEMA KWAMBA HIJJAB NI ISHALA TU KATIKA JAMII JAMBO LISILO LA KWELI HATA KIDOGO UISLAM UNAHUKUMU ZAKE AMBAZO MWANADAMU YEYOTE HAWEZI KUZIBADIRISHA NA KUWEKA KTK FIKRA ZAKE NA NAIKAKUBARIWA KATIKA UISLAMU.KITENDO CHAKUSEMA HIJJAB NI ALAMA AU UTAMBULISHO WA UISLAMU SIKWELI BALI HIJJAB NI STARA AMBAYO MWISLAMU KAAMRISHWA AIVAE SO NI NILAZIMA AWE KATIKA MAZINGIRA HAYO MUDA WOTE. Mimi binafsi siungi mkono jambo ambalo KIBONDE amelifany BUT ninacho kupinga ni wewe kuchanganya kauli ya kibonde kanakwamba katumwa na bakwata. Bakwata take yao ilikua ni kwenye hijjab suala ambalo lilitokea

Yule mama anafuga kitimoto kwake na wala hakuvaa hijab alivaa mtandio na wala si muislam anaishi kipagani yule, BAKWATA walidandia tu treni kwa mbele kwa ukosefu wa elimu
 
Hizi hoja wanazozishabikia hii Radio ipo siku wataona madhara yake.Clouds ni chombo cha habari kibaya sana ,nilishawahi kuuliza humu jamvini uwezo wao katika kuendesha mijadala hewani.
Miaka ya 1990 huko Rwanda na Burundi vituo vya Radio ambavyo havikuwa na maadili kama hii Clouds ,vilikuwa vikiendesha/kurusha matangazo yao namna hii.Na kupitia kwa watangazaji kama hawa kina Kibonde walikuwa ni moja ya wahamasishaji/wachochezi wakubwa wa chuki za ukabila hadi kufikia mauaji ya watu takribani 800,000.
Hii ni kutokana na uelewa mdogo wa watangazaji wanaoendesha mijadala kwenye Radio bila kufuata misingi ya taaluma zao.Watu kama Kibonde ni hatari sana kwa jamii yoyote iliyostaarabika.Sizani kama jamii ya kitanzania inahaja ya kusikiliza hizi hoja na matamko yenye lengo la kugawa wananchi.
Pia hawa wanaofanya hivi (Wanaoendesha hii mijadala/kutoa matamko ) hawajuai wanamwelezea nani kwani jamii ya watanzania haiko hivyo wao wanavyofikiri.Muisilamu/Mkristo anayeishi Tanga /Tabora ama Kilimanjaro anaishi peke yake ? ama anaishi na waisilamu tu /wakristo tu katika utekelezaji washughuli zake mbalimbali za kijamii/kiuchumi? .Hichi kikundi cha watu wanaotumiwa vibaya kwa maslahi ya watu binafsi ni mbaya sana kwa mustakabali wa Taifa letu.
Kwenye familia nayotoka mimi tumechanganyika waisilamu na wakristo yupo Dada(Muisilamu) aliyeolewa na Mkristo. Watoto wao watatu, wawili wakristo mmoja Muisilamu.Yupo baba mdogo(Muisilamu) aliyeoa mkristo -mkewe hajabadili dini na wanaishi vyema miaka 18 ya ndoa .Wapo ndugu wengine wa mchanganyiko (waisilamu na wakristo).Sasa tukikaa kama familia tutaanzia wapi kufanya mijadala ya kidini (Kusutana kunyosheana kidole kwa misingi ya kidini)?.Dada aliyeolewa na Mkristo bwana yake (Mkristo) ndio anayenisomesha.Huo hapo ni moja ya mifano ila kwa familia nyingi ndivyo mambo yalivyo kutokana na misingi tulionayo watanzania tokea enzi hizo.
Hawa wanaotaka kutugawa hawataweza kamwe kwa matamko yao yasio na baraka za watanzania, sio Waisilamu /Wakristo.
Anayejifanya anajua dini zaidi ya watu wengine huyo ndio adui wa amani na upendo.Hakuna mafundisho yoyote dunia hii kwenye Quran/Bible unaosema tuishi kwa kushutumiana ama tusipendane kutokana na tofauti zetu za kiimani.
Nimesikitika sana kwa kikundi cha watu kutoa matamko bila kujua undani na uhalali wa kile wanachokikemea.Kuna ushahidi gani kuwa waliomkamata yule mama ni vijana wakikristo na si vijana wa kiisilamu wenzetu?.Familia ya kimariyo ikijitokeza hadharani na kusema kuwa kwenye familia yao hakuna muisilamu,itakuwaje?.Watoto wa Bi fatma waliolelewa kwenye misingi ya kidini tena kikatoliki wanafundishwa nini? na watamchukuliaje mama yao ?

Angalizo;Napinga kitendo cha yule mama kushikwa kikatili namna ile,nikiwa kama mwana harakati.Ila mbaya na ninachopinga ni kitendo cha watu/kikundi kutumiwa sivyo kushabikia ,mpaka kufikia kutoa tamko lenye kuhusisha imani zenye malengo ya chuki za kidini.Historia itawasuta hawa kina Kibonde wanaoshabikia/kuendeleza hili.
 
HISTORIA ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.

Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mama Fatma Kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa CHADEMA. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.

Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya BAKWATA na BASUTA kutaka CHADEMA iombe radhi Waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya Kiislamu yanavyowataka wanawake wa Kiislamu wawe).

Kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamii Forum alivyochangia kuwa “Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa Watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiano”

Ninaamini Clouds FM wanalijua hili, lakini katika moja ya vipindi vyao, mtangazaji wao( Epharim Kibonde) akizunguza kuhusu sakata hili la Mkuu wa Wilaya wa Igunga, amenishtua na kwa hakika nimeogopa. Mtangazaji huyo katika moja ya vipindi anapolivisha suala hili sura ya kidini kwa kiwango kile, huku akijua kuwa wasikilizaji wake wana viwango tofauti sana vya uelewa sijui alikuwa anadhamiria kuiambia nini jamii.

Mtangazji huyu amekwenda mbali (mbali sana) kupandikiza hisia za udini wa hali ya juu kwenye suala hili, anapozungumzia habari za kwamba eti Waislamu nao wakifikia hatua ya kuwavua watawa Wakatoliki vilemba vyao kama alivyofanywa mkuu wa wilaya, kwa hakika hii ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa hili.

Maadili ya taaluma hii yanatutaka tusema ukweli tu na ukweli mtupu kwa manufaa ya ustawi na mshikamano wa jamii tuliyomo.
Tukifika mahali tukaanza kuwianisha hisia zetu au ushabiki wetu katika mambo tete na nyeti kama imani za dini tunakuwa hatuitendei haki nchi yetu wala sisi wenyewe.

Kwa sababu, hebu tufikiri pamoja kwa sauti, hivi katika hili Ukatoliki au watawa Wakatoliki wamehusika vipi, Je, mtangazaji huyu anaweza kusema kwa uhakika aliyosema anawasemea Waislamu, amefanya utafiti kiasi gani au akajiridhisha kwa kiwango gani suala hili linahusu Ukristo na Uislamu?

Hapana, tusilifikishe taifa hili mahali ambapo halitakuwa tena taifa moja tunalojivunia sasa kwa ajili tu ya kuwanufaisha watu wachache au kwa maslahi ya nani sijui. Hatimaye Tanzania kwa Watazania ni juu ya kila kitu, utaifa wetu unakuja kwanza na mengine yatakuja baadae, tutumie nafasi zetu na mamlaka tuliyo nayo katika jamii kuhakikisha tunahamasisha umoja zaidi kuliko kupandikiza mbegu za kutugawa, tunaweza kudhani ni mbegu ndogo sana, lakini madhara yake ni makubwa kuliko tunvyoweza kufikiri.
Wapo miongoni mwetu, wanachukulia kitu wanachosikia redioni, runigani, au kwenye gazeti kama ni ukweli halisi wa kila jambo, kwa hiyo hata kama tunafanya masihara tusifanye masihara ya hatari namna hiyo, historia ya taifa hili isije ikatuandika kwenye kitabu cheusi.
Mungu ibariki Tanzania

Sosi: Tanzania Daima

kaa chini nenda ukaangalia sheria zote husika za Tanzania kuhusu kumkamata mtu then uje uniambie katika kumkamata je ilikuwa reasonable force mpka ifikie mwanamama wa watu kuvuliwa ushingi ????????????/then ndiyo uilete hii mada tena.UMEELEWA????????
 
Kwa kweli Kibonde kweli ni kibonde!!!!! Hajui kwamba hajui na itakuwa ngumu sana kwa mtu huyu kujua. Jamani mlio karibu naye mshaurini!!! anajichoresha kinoma. Mi binafsi naipenda sana clouds, naskilizaga vipindi vyote frm power breakfast, tena naipenda jahazi mnooo!!! ila jamaa ananinyima raha kishenzi, anankosesha utamu wa redio yangu
 
huyo kibonde anamatatizo sioni uhusiano wa kilemba cha DC na cha mtawa, anauhakika gani kuwa wale walomvua DC the so called hijab ni wakristo, watu wengine sijui wakoje ujinga mtupu
 
Nilikisikiliza kwa makini na mwanzoni Kibonde aliwakandia sana CDM na kutumia maneno yake ya kejeli na kujifanya anajua.
Kibonde aliumbuka muda mfupi baadae wakati akipitia magazeti ya siku hiyo ambapo gazeti la Taifa Tundu Lissu alinukuliwa akitoa majibu na alijaribu kuelezea kuwa hiyo haikuwa hijab ila mtandio.
Alinywea na ikabidi awaelekeze watu waeleze ni nini hijab kupitia address yao ya facebook.
Bibie hakuvaa Hijab ila mtandio na picha zinaonyesha hivyo.
Kuhusu Bakwata narudia tena kuwa nikiwa Muisalmu kuwa njaa itatumaliza.Tuna mambo mazito na ya msingi na sio hili.
Changamoto kwa Bakwata-Tuna Chuo Kikuu kimoja,shule zetu za sekondari zinaongoza kwa kufelisha.
Tuachane na mambo ambao si ya msingi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yaan kibonde upeo wake ni finyu sana namsikilizaga anavyoongea utumbo na kushadadia kwa kudhan kwamba atapata favor flani..pole yake.....m muslim but niwajuwavyo wakristo si watu wa kushadadia vitu ni wastaarabu na wavumilivu,waislam wenzangu kweli aibu yetu hatufanyi uchunguzi twalopoka tuuu....
 
Watangazaji kama hawa dawa yao ni OCAMPO, tena anawahitaji sana! (Hawajifunzi ya wanahabari wenzao wa Rwanda na sasa Kenya!)
 
As-Salamu Alaykum

In Tanzania, and other Swahili speaking countries on the coast of East Africa the term is pronounced "assalamualaikum" followed by a reply of "aleikum-salam", people usually shake hands, hug, and sometimes wave. Typically this greeting remains mainly Islamic related
 
Niliacha kusikiliza clouds fm kwa ajili ya upupu wa huyo kibonde siku nyingi,baada ya kuona post hii leo nimekubali kuwa mashaka yangu juu ya uwezo wa huyo bwana kibonde kielimu na kupambanua mambo hata madogo sana ni finyu mno.TUMPUUZE
 
kaa chini nenda ukaangalia sheria zote husika za Tanzania kuhusu kumkamata mtu then uje uniambie katika kumkamata je ilikuwa reasonable force mpka ifikie mwanamama wa watu kuvuliwa ushingi ????????????/then ndiyo uilete hii mada tena.UMEELEWA????????

Akili yako itakuwa ndo sana

Sasa unataka kusema kuwa majambazi wewe wanajifunga hijabu /mtandio kwenda kuiba ili wasikamatwe???
 
Tanzania hamjawahi kuona vita, itafuteni itakuja - tena kwa mtindo wa ushabiki wa kijinga kijinga - kilemba kinapokuwa hijabu, hijabu inapokuwa mtandio. mimi simo.
 
Ilikuwa bahati mbaya nikiwa natafuta E.A. Radio jana nikamsikia kayanda anatetea ile picha ya J>K, kuwa 50 ndo amemfuata wakapiga picha! ikanibidi nizime kabisa. HEBU MSIKILIZENI KIBWANA DACHI 8:00AM MAGIC FM ni raha kweli.
 
HISTORIA ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.

Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mama Fatma Kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa CHADEMA. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.

Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya BAKWATA na BASUTA kutaka CHADEMA iombe radhi Waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya Kiislamu yanavyowataka wanawake wa Kiislamu wawe).

Kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamii Forum alivyochangia kuwa “Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa Watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiano”

Ninaamini Clouds FM wanalijua hili, lakini katika moja ya vipindi vyao, mtangazaji wao( Epharim Kibonde) akizunguza kuhusu sakata hili la Mkuu wa Wilaya wa Igunga, amenishtua na kwa hakika nimeogopa. Mtangazaji huyo katika moja ya vipindi anapolivisha suala hili sura ya kidini kwa kiwango kile, huku akijua kuwa wasikilizaji wake wana viwango tofauti sana vya uelewa sijui alikuwa anadhamiria kuiambia nini jamii.

Mtangazji huyu amekwenda mbali (mbali sana) kupandikiza hisia za udini wa hali ya juu kwenye suala hili, anapozungumzia habari za kwamba eti Waislamu nao wakifikia hatua ya kuwavua watawa Wakatoliki vilemba vyao kama alivyofanywa mkuu wa wilaya, kwa hakika hii ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa hili.

Maadili ya taaluma hii yanatutaka tusema ukweli tu na ukweli mtupu kwa manufaa ya ustawi na mshikamano wa jamii tuliyomo.
Tukifika mahali tukaanza kuwianisha hisia zetu au ushabiki wetu katika mambo tete na nyeti kama imani za dini tunakuwa hatuitendei haki nchi yetu wala sisi wenyewe.

Kwa sababu, hebu tufikiri pamoja kwa sauti, hivi katika hili Ukatoliki au watawa Wakatoliki wamehusika vipi, Je, mtangazaji huyu anaweza kusema kwa uhakika aliyosema anawasemea Waislamu, amefanya utafiti kiasi gani au akajiridhisha kwa kiwango gani suala hili linahusu Ukristo na Uislamu?

Hapana, tusilifikishe taifa hili mahali ambapo halitakuwa tena taifa moja tunalojivunia sasa kwa ajili tu ya kuwanufaisha watu wachache au kwa maslahi ya nani sijui. Hatimaye Tanzania kwa Watazania ni juu ya kila kitu, utaifa wetu unakuja kwanza na mengine yatakuja baadae, tutumie nafasi zetu na mamlaka tuliyo nayo katika jamii kuhakikisha tunahamasisha umoja zaidi kuliko kupandikiza mbegu za kutugawa, tunaweza kudhani ni mbegu ndogo sana, lakini madhara yake ni makubwa kuliko tunvyoweza kufikiri.
Wapo miongoni mwetu, wanachukulia kitu wanachosikia redioni, runigani, au kwenye gazeti kama ni ukweli halisi wa kila jambo, kwa hiyo hata kama tunafanya masihara tusifanye masihara ya hatari namna hiyo, historia ya taifa hili isije ikatuandika kwenye kitabu cheusi.
Mungu ibariki Tanzania

Sosi: Tanzania Daima

Huu ni wendawazimu,huyu mtangazaji kakosa maadili ya kutosha,atumie akili.
 
Back
Top Bottom