Mzee wa Usafi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 644
- 292
Mimi ni mmoja wapo ya Watanzania wachache tuliobahatika kupata kibaru angalau na kuingia kwenye mfumo rasmi wa kodi...PAYE. Pamoja na hilo pia nimekata health insurance hivyo nikiugua napata tiba kutoka kwa bima yangu... Ili nchi yoyote iendelee ni lazima ikusanye kodi na kuwajibika kutumia vizuri hizo kodi. Najua matumizi ya serikali ya magamba ni ya anasa hata kwa hicho kidogo wanacho kusanya....Nimesikitishwa zaidi na wabunge wetu kwa kushabikia boda boda wasitozwe kodi kisa kipato chao ni kidogo....Mimi nilidhani kuwa kila mtanzania anawajibu wa kulipa kodi kulingana na kipato chake anachopata sasa kwa nini wao wasichangie maendeleo ya nchi yao?. Hao boda boda hawalipa kodi na ndo wanaotumia facilities zote za serikali " hospitali" pale wanapopata ajali ambazo kwa sasa zimekithiri... Hao hao boda boda wanakodi piki piki kwa sh 5000 kwa siku, je kwa nini serikali isiwatoze hata sh 20,000 kwa mwaka. Hawa boda boda wengi wao hawana hata leseni ....ninalipa kodi kwa mwaka sawa sawa na mishahara yangu ya miezi mitatu na nusu ...Kila mtu anawajibu wa kulipa kodi kwa jinsi anavyopata....napinga kwa boda boda kutolipa kodi....