Serekali ya ajabu, Mnakamua kodi kwa wananchi ila swala la Bima kwa afya zao mmeshindwa

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,021
2,296
Kulikua na ile bima ya watoto ya 50400 ilikua inasaidia watu wa kipato cha chini, serekali ikaitoa, wao hawaoni uchungu kwasababu ni mabosi na bima wanalipiwa na maofisi kupitia kodi za wananchi, kwahiyo kutoa hiyo kodi wala haiwahusu.

Kodi na tozo zimezidi kutamalaki ila sijawahi sikia kitu tozo flani ikasaidie swala la bima kwa wananchi, kulipia vile viwango vya bima vikubwa kwa wananchi imekua changamoto kwa mara moja,

Hivi karibuni ndugu zetu wa bajaji na boda boda wamewekewa kodi, ni kweli pesa nzuri itapatikana, ila hata wananchi hawajui itaenda wapi,

Yani vilaza kabisa hawaumizi kichwa kutafuta vyanzo makini vya kodi wameamua kukimbilia kwenye boda boda wakaanze kukimbizana nao mtaani kuhusu kodi, So boda boda atakua na kodi, latra, bima, bado kumlipa boss, bado mafuta, bado hajaacha nyumbani, na bado hapo hajakimbizana na Trafiki, du kazi wanayo na serekali yao hii walioichagua

Katika matozo yote haya na kodi zote wananchi wanazolipa sijasikia hata siku serekali hii ikimfikiria Afya yake huyu mwananchi wa chini kumpatia bima huyu mwananchi aendelee kuzalosha ili kumpatia hizo tozo, serikali ni kukamua tu, akiugua ndugu wana hangishana, akifa afilie mbali,

Tuwe makini na serekali kama hizi
 
Back
Top Bottom