hao ndio waandishi wetu. Mimi nimemsikiliza Ghasia alisema fungu la pesa za kulipa wafanyakazi limeongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana. Hakusema mshahara umeongezeka kwa asilimia 40. Fungu kuongezeka haina maana mshahara umeongezeka, inawezekana madeni ya watumishi ndo mengi, au wafanyakazi walioajiliwa wamwongezeka ikilinganishwa na mwaka jana, au kuna taasisi mpya za serikali zimeongezeka. Ukweli ni kwamba mshahara haujaongezeka alisema serikali itaendelea kurekebisha mishahara ya wafanyakazi kulingana na hali ya maisha. SERIKALI HAINA PESA kwa sasa.
Mzee Avatar yako imenikuna sana kwani imenikumbusha enzi zileee za warant na mabasi ya Tanzania Railways Cooperation (TRC) hapo ilikuwa wapi, Tukuyu au??
Mnyika kasema hawa ni wasanii wanawadanganya watumishi mana hakuna sehemu yoyote inaonyesha kuwa kuna asilimia 40 imeongezeka kwenye mishahara.MAGAMBA wanaipeleka nchi pabaya.
Kwa jinsi nilivyo mpata waziri mwenye dhamana husika akiwasilisha hoja, Ni kwamba fungu zima la bajeti ya mishahara limepanda kwa 40% , sio kwa maana ya mshahara wa mtu mmoja mmoja. Cha msingi ni kusubiri tuone kutoka katika hizo 40% wanazigawa vp kwa mshahara wa mtu mmoja mmoja. Na sio mishahara kupanda tu pia wanaweza kuamua vile vile kutoka katika hilo fungu la 40% waka create ajira mpya. So kwa mantiki hiyo utengezaji wa ajira mpya unaweza ukaathiri kiasi cha ongezeko la mishahara kwa namna moja ama nyingine. Ni hayo tu wakuu, Naomba kuwasisha hoja!
Mtoa mada nadhani hata hukuifuatilia hotuba ya Hawa Ghasia, alisema kuwa bajeti ya wizara ya utumishi wa umma kwa mishahara imepanda kwa 40% na siyo mishahara!!! naomba uisome vizuri hiyo sentesi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.