Bajeti ya Mishahara kupanda kwa zaidi ya asilimia 40!

MS...hakuna kiwango rasmi kilichotangazwa ktk kupandisha mishahara, mtazamo wako ni finyu ktk hili na unapojaribu kuleta thread yenye mlengo wa mtawala unapotosha wananchi. Usiwe kama gazeti la Habarileo au Uhuru wao wanaandika mishahara juuuu! juu ya how much or lini kiwango hicho kitaanza kutumika?
 
hakuna kauli ya moja kwa moja ya kuwa mishahara imepanda au la, usije ukashangaa imepanda kidogo sana
 
hata wakipandisha ni kiduchu saana kumbuka na kodi inapanda ningeomba kuliko kupandisha mishahara bora hata wangepunguza kodi asilimia 14 ni kubwa sana hata iwe asilimia 10 afu wafidie kwa wale wanaosamehewa kodi na haya makato mengine yapunguzwe duh tunakatwa bima ya NHIF hadi leo kadi hamna
 
Sekta binafsi mishahara yao inaratibiwa na wizara ya kazi kwa sasa mama kabaka.

Sijui kama ameshamaliza kujadiliana na ATE ili kupandisha viwango manake hkom kuna mambo ya kiisekta then ndipo waziri atangaze kiwango.

Ila kwa serikali hii ya jk usitarajie lolote jipya kwa mfanyakazi wa sekta binafsi, mawaziri hawa hawa wanaootangaza nyongeza ya mishahara kwenye vyombo vya habari halafu wanawaandikia barua waajiri hao hao wa sekta binafsi kutolipa mmishahara mipya, si unakumbuka maajabu ya kapuya.

Sasa kama wafanyakazi wa serikali ndo hao hawajui wameongezwa kiasi gani hawa sekta binafsi wanaomilikiwa na mabepali watawajali kwa
kuwaongezea mishahara kweli???
 
SERIKALI imetangaza bungeni kuwa itatutumia Sh3.2trilioni katika mwaka wa fedha 2011/12, ambazo pamoja na mambo mengine zitapandisha mishahara ya watumishi wa umma kwa kuzingatia vigezo maalumu, ikiwamo mfumuko wa bei za bidhaa na huduma.

hongera Jk.
CDM walidandia agenda. kama kawaida yao

Huu ni wendawazimu.
Tibiwa upone, unashabikia mwanaume kama wewe ni mwanamke!
 
SERIKALI imetangaza bungeni kuwa itatutumia Sh3.2trilioni katika mwaka wa fedha 2011/12, ambazo pamoja na mambo mengine zitapandisha mishahara ya watumishi wa umma kwa kuzingatia vigezo maalumu, ikiwamo mfumuko wa bei za bidhaa na huduma.

hongera Jk.
CDM walidandia agenda. kama kawaida yao

Malaria Sugu acha propaganda. Usiwadanganye watu. Ongea kwa facts and figures. Serikali haijasema imepandisha mshahara ila imesema bajeti ya mishahara imeongezeka. Kama imepandisha mshahara tuambie imepanda kwa asilimia ngapi? kima cha chini kimepanda kwa asilimia ngapi? na kitakuwa kiasi gani?

Mimi ninavyojua hiyo nyongeza ni kwa ajili ya kulipa malimbikizo pamoja na madeni ya walioajiriwa mwaka jana na waliopandishwa vyeo ambao hawakulipwa mishahara stahiki. na hao wako wengi. Pia kuna ajra mpya na annual increments za mwaka jana na mwaka huu.
 
Hivi haya magazeti ya Uhuru na HabariLeo hayana wahariri??

Yana vichwa vikubwa vya habari eti mishahara ya wafanyakazi juu(40%) ina maana hawakumsikia Hawa Ghasia au??
Kwanini wameshindwa kutumia akili ndogo tu kufikiri hii kitu?? Hii asilimia 40% haijabainishwa hata punje...haijulikani ni kulipa malimbikizo ya wafanyakazi, haijulikani ni kwa ajili ya vigogo wa serikali, haijulikani ni ya wazee RAC, au ni walimu ambao wanaidai serikali zaidi ya Bilioni 13...sasa iweje wanadanganya wafanyakazi kwamba mshahara juu??
This is stupi.d.

Isitoshe wameandika front page kwa kupotosha kwamba bajeti ya Wapinzani imeungana/imekubaliana na serikali kuhusu pesa ya BAE system kulipa kwa serikali...Huu ni ushuzi/uzushi!! wao wamesuggest kufungua account ya Rada watumbukize kule na isije seikalini kwa kuwa iliibiwa hukohuko serikalini...ni aibu magazeti ya magamba!!
 
Hao wanazo akili sana lakini ndiyo walivyo .Wako kama Nkamia Juma yeye anakamia tu .Ukisha kuwa mwandishi wa Uhuru unategemea nini ?
 
Waandishi wasiotafakari waliofukia taaluma zao kwenye michanga wa ajabu sana hivi watakuwa na jibu wafanyakazi watakapoanza kugoma wakidai asilimia 40 ya nyongeza kwenye mishahara yao
 
Nadhani wanawachochea wafanyakazi, asilimia 40 siyo mchezo, kama kweli wamepandisha basi wawe wamejipanga kuilipa lasivyo itakuwa ni malimbikizo tu mpka 2015 na hapo ndipo moto mkali utakapo lipuka.

Sidhani kama inawezekana kupandisha mishahara ya wafanyakazi wote wa umma kwa asilimia 40, haiwezekani labda kwa wale wa kima cha chini na cha kati. Kwa ukata uliopo magogoni hii ni danganya toto lakini kazi kwao maana vyama vya wafanyakazi watakuwa wanalikodolea macho hili!
 
Hivi haya magazeti ya Uhuru na HabariLeo hayana wahariri??

Yana vichwa vikubwa vya habari eti mishahara ya wafanyakazi juu(40%) ina maana hawakumsikia Hawa Ghasia au??
Kwanini wameshindwa kutumia akili ndogo tu kufikiri hii kitu?? Hii asilimia 40% haijabainishwa hata punje...haijulikani ni kulipa malimbikizo ya wafanyakazi, haijulikani ni kwa ajili ya vigogo wa serikali, haijulikani ni ya wazee RAC, au ni walimu ambao wanaidai serikali zaidi ya Bilioni 13...sasa iweje wanadanganya wafanyakazi kwamba mshahara juu??
This is stupi.d.

Isitoshe wameandika front page kwa kupotosha kwamba bajeti ya Wapinzani imeungana/imekubaliana na serikali kuhusu pesa ya BAE system kulipa kwa serikali...Huu ni ushuzi/uzushi!! wao wamesuggest kufungua account ya Rada watumbukize kule na isije seikalini kwa kuwa iliibiwa hukohuko serikalini...ni aibu magazeti ya magamba!!
Wao kazi yao ni kuwasifia mabwana wakubwa wao tu....... hadi wanajisahau na kuandika uwongo
 
ni kitu usichoweza kuamini lakini kuna jamaa yangu baada ya kujiunga huko huwezi hamini, akili imejifunga kabisa!
Hao wanazo akili sana lakini ndiyo walivyo .Wako kama Nkamia Juma yeye anakamia tu .Ukisha kuwa mwandishi wa Uhuru unategemea nini ?
 
Kwa miaka mingi wananchi tumekuwa tunalalamika kuwa serikali inatuhadaa. Lakini sasa tunaelewa magezeti ya serikali hususan Uhuru na Daily News wamekuwa ndio wapotoshaji wakubwa wa kile kinachosemwa na viongozi wa serikali. Kama sio kuwepo kwa LIVE BROADCASTING watu wengeamini kuwa mishahara imepanda kwa 40%. Shame on you Uhuru!
 
Hao ni waandishi misukule.Hata hivyo vipeperushi vyao havina hadhi ya kuitwa magazeti vina hadhi ya karatasi za chooni tuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Jamani sio kosa lao, nahisi ni maelekezo waliyopewa na Makinda kwani siku za hivi karibuni alikaririwa katika vyombo vya habari akitoa muongozo kwa waandishi wapokee taarifa za bunge kupitia kwa wana habari wa Bunge na sio kutokana na uhalisia wa Bunge, so waliowapa maelekezo wanafanya hivyo kusafisha Nyota, Huku wakiwa hawajafikiria kuwa wanajipalia mkaa!
 
Back
Top Bottom