Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
335
Mh. Waziri wa fedha amemaliza kuwasilisha bajeti moja ya kitu kipya ni usajili wa magari kwa namba maalum (ie jina lako)unalipa mill 5, Great Thinkers nini mtazamo wako, je ni kuaisha wenye uwezo waonekane hata katika plate namba za magari yao au lengo ni kukuza mapato ya serikali bila kuangalia mitazamo ya kijamii.
 
Huo ni mkakati wa serikali kujiongezea mapato na wala sio kwa ajili ya watu kujionesha kuw wanapesa...
 
Yote mawili yanawezekana maana alisema kuna watu wanataka plate number ziwe na majina yao na Serikali inataka kutumia mwanya huo huo kupata fedha. Wasanii wanaopenda kujianika kwenye magazeti ya udaku mara kwa mara wakinunua magari au nyumba ni nafasi yao ya kujimwayamwaya sasa.
 
na kweli wale wanopenda kujitofautisha na wakina kayumba wakati ndo huu! Na wale wanopenda kuchukua magar ya watu huku wakidai ni ya kwao imekula kwao.
 
Huu ulimbukeni unaelekea kuua Taifa kwa mtindo huu.
Ya mwaka ujao tusishangae, ikija na style ya vyangu doa na mashoga kupewa lesini na kulipia kodi.
Eeh! Mungu ni chukue mapema kabla maandiko hayajatimia..
 
Hiyo ni style nzuri tu na inatumiwa nchi nyingi sana kama South Africa, Namibia, Lesotho N.K.

Ni njia mojawapo ya "MATOZI" kujionyesha na kuuzia sura huku serikali ikijipatia Fedha zaidi. Mgogoro ni je, pesa hiyo ya ziada ambayo haikuwepo awali inapelekwa wapi?

"WALIOSOMA NI CHAKULA CHA WANASIASA"
 
sitaki kuamini kama itakuwa ni moja kati ya vyanzo vipya vya mapato vilivyobuniwa na sirikali..haya kazi kwao wale wa promo..
 
But five mill, is too much, hiyo gari umeinunua kwa gharama gani? corola ya 7 mill na plate number ya 5mill?

Lazima ada iwe kubwa ili wachache na wenye uwezo ndio wanufaike...kimsingi si jambo lenye athari kwa wananchi,hata mamtoni ipo hivyo. Wenye uwezo waweke tu!
 
sitaki kuamini kama itakuwa ni moja kati ya vyanzo vipya vya mapato vilivyobuniwa na sirikali..haya kazi kwao wale wa promo..

Ninakuhakikishia kitakuwa chanzo kipya cha mapato, TZ ina matozi wengi sana, Mfano angalia wanafunzi wa vyo vikuu maisha wanayoishi vyuoni kisha siku moja pata nafasi ya kutembelea wanakotoka. Kwa ujinga huu, serikali itajipatia kipato cha kutosha tu.
 
Millioni 5? Hapa Maryland tags maalumu unalipa dola 50 tu.

Kumbe Jasusi uko majuu siku zote nilifikiri uko bongo; haya salaam zao vijana wangu nao wako huko Maryland sehemu inaitwa Montgomery village!!Wale mafisadi wetu wenye FERRALI na LAMBOGINI ndio watanunua hivyo vibao vya mill.5!!
 
ulipaji wake umekaaje wakuu.....? Je ukilipa kwa mara ya kwanza mil 5 utaendelea kulipa figure hiyo hiyo au itakuja kwenye rate ya kawaida?
 
ninakuhakikishia kitakuwa chanzo kipya cha mapato, tz ina matozi wengi sana, mfano angalia wanafunzi wa vyo vikuu maisha wanayoishi vyuoni kisha siku moja pata nafasi ya kutembelea wanakotoka. Kwa ujinga huu, serikali itajipatia kipato cha kutosha tu.

ccm sasa itamke wazi kwamba nchi hii si ya mkulima na mfanyakazi bali ni ya matajiri na wafanyabiashara,sina ubaya na mpango huu,lakini nataka neno ujamaa lifutwe kwenye katiba ya ccm maana moja ya miiko ya ujamaa ni kuwewepo kwa kundi la mimi namiliki x na y anamiliki z.pole ccm,nyamala ubepari ndio mpango mzima,kubali yaishe ili wananchi wajue kuliko kuwa msanii.
 
Aaaaaa 5 mil ni three much tena! Ka plate namba chenye jina lako tu? Its just an identity the same as numbers! 5 mil ni nyingi sana ata kama ni kwa kuuza sura
 
Majimbo mengine dola ngapi?
Ritz,
Kila jimbo lina taratibu zake. Kwa mfano NY sales tax ni 12% wakati Maryland ni 5%. Najua tu DC, Virginia na Maryland hazizidi dola 50 kwa hizo vanity tags.
 
Kumbe Jasusi uko majuu siku zote nilifikiri uko bongo; haya salaam zao vijana wangu nao wako huko Maryland sehemu inaitwa Montgomery village!!Wale mafisadi wetu wenye FERRALI na LAMBOGINI ndio watanunua hivyo vibao vya mill.5!!
Bulesi,
Niko njiani kurudi Bongo. Napafahamu sana Montgomevy Village, niliishi hapo kwa miaka 6 nikahamia mashambani zaidi lakini karibu na ufukwe wa bahari nijione kama niko Dar vile.
 
Back
Top Bottom